TP Mazembe, wakiwa kwao Stade du TP Mazembe Lubumbashi, Congo DR, wamenyakua Ubingwa wa Afrika baada ya kushinda Mechi ya Pili ya Fainali ya CAF CHAMPIONZ LIGI kwa kuitwanga Union Sportive Medina d’Alger Bao 2-0 huku Straika mahiri wa Tanzania Mbwana Samatta akifunga Bao la Kwanza.
TP Mazembe imenyakua Ubingwa huu wa Afrika, ikiwa ni mara yao ya 5, kwa Jumla ya Mabao 4-1 baada ya pia
kuwa washindi wa Bao 2-1 toka Mechi ya Kwanza ambayo Bao la ushindi lilifungwa na Straika wetu, Mbwana Samatta.
Hii Leo Samatta alifunga Bao lake Dakika ya 74 kwa Penati baada ya Zinedine Ferhat kumchezea Faulo Roger Assale ambae pia aliipa TP Mazembe Bao la Pili katika Dakika ya 90.
Bao lake la Leo Samatta limemfanya afikishe Bao 8 katika CAF CHAMPIONZ LIGI Msimu huu na kuibuka ndie Mfungaji Bora wa Michuano hii.
Mbali ya Samatta, Leo hii TP Mazembe pia walikuwa na Fowadi mwingine kutoka Tanzania ambae ni Thomas Ulimwengu alieng’ara katika pambano hili.
Baada ya kutwaa Taji hili, TP Mazembe wamezoa Donge la Dola Milioni 1.5 na pia wataiwakilisha Afrika kwenye Mashindano ya FIFA ya Klabu Bingwa Duniani huko Japan Mwezi Desemba.
0 maoni:
Post a Comment