Saturday, October 17, 2015


Kocha wa Manchester United Louis van Gaal anadhani umefika wakati wa Wayne Rooney kuanza kuonyesha cheche zake tena kwenye Uwanja wa Goodison Park ambao ndio alichomoza na kuwa Staa wa Dunia.
Rooney alianza kuichezea Timu ya Kwanza ya Everton tangu 2002, akiwa Kijana wa Miaka 17, na kwa Miaka Miwili alizoa kila sifa lakini Mwaka 2004 alihamia Man United kwa Dau la Pauni Milioni 30 na kuzua chuki toka kwa Mashabiki Goodison Park.
Rooney hana raha tena na Goodison Park ambako huzomewa na kutukanwa n ahata Magoli kwake Uwanja hapo ni nadra kwake.
Rooney amefunga Bao 2 tu katika Mechi 10 alizoichezea Man United Uwanjani Goodison Park.
Lakini Van Gaal hajakata tamaa na Jana alisema: “Pengine dhidi ya Everton wastani wake si mzuri. Sasa umefika wakati abadilishe hilo. Sijui kwa nini amekuwa na shida pengine muulizeni yeye. Mimi ni Meneja ninae tathmini wapinzani na kumpa ushauri njia bora kuvunja difensi nap engine atafunga.”
Kabla Msimu huu kuanza, Rooney aliahidi atafunga Bao 30 lakini hadi sasa amefunga Bao 1 tu la Ligi katika Mechi 7.
Hivi sasa Rooney sie Straika mkuu wa Kikosi cha Van Gaal baada ya jukumu hilo kupewa Chipukizi mpya Anthony Martial na Rooney kucheza nyuma yake lakini Van Gaal anaamini bado mchango wa Kepteni wake Rooney ni muhimu.
Van Gaal ameeleza: “Yeye ni Straika wetu wa pili. Namba 10 ni Straika wa pili.”
Ameongeza: “Rooney anaweza kucheza nafasi nyingi na kwangu si muhimu nani anafunga ili mradi tufunge Goli nyingi.”
Van Gaal haamini kuwa mzigo wa kuwa Nahodha umemwelemea Rooney kwani Kepteni wake huyo anauweza kutokana na tabia yake.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog