Thursday, October 22, 2015


MASTAA wa zamani wa Manchester United, Paul Scholes na Rio Ferdinand, wamesikitishwa na jinsi Timu yao ilivyocheza huko Moscow Jumatano Usiku na kutoka Sare 1-1 na CSKA Moscow katika Mechi ya Kundi B la UEFA CHAMPIONS.
Katika Mechi hiyo, Man United walicheza ovyo Kipindi cha Kwanza na kufungwa Bao la Penati lakini Kipindi cha Pili Man United walizinduka na kusawazisha kwa Bao la Chipukizi Anthony Martial.
Scholes na Rio, wakiwa Wachambuzi wa Mechi hiyo kwenye TV ya BT Sport huko England, walisikitishwa na uchezaji wa Man United na Scholes kutaja kasoro za Kepteni wao Wayne Rooney ambae alidorora kabisa.

Katika Mechi hiyo Rooney alicheza kama Sentafowadi na pembeni kushoto alicheza Martial na kulia Jesse Lingard.
Scholes alieleza: "Rooney si mzuri kama hana Watu wenye kasi wanaomzunguka. Hata mie nilikuwa hivyo!"
Hata hivyo, Scholes alikiri kupata Sare kwenye Uwanja wenye baridi kali mno huko Moscow si matokeo mabaya.
Nae Rio Ferdinand alisema; "Tulipatwa na wasiwasi jinsi Man United walivyocheza Kipindi cha Kwanza. Walipooza, hawakuwa na spidi wala mashambulizi!"
Lakini Rio alisifia uchezaji wa Kipindi cha Pili ambapo Wachezaji waliongeza bidii, spidi ikaonekana na kuingia kwenye boksi mara kwa mara.
Wachambuzi hao walibainisha kuwa kwenye Mechi hiyo Rooney aligusa Mpira mara 40 tu ukilinganisha na mara 47 za Fellaini alieingizwa Kipindi cha Pili.
Mechi ijayo kwa Man United ni huki Old Trafford hapo Jumapili Oktoba 25 ikiwa ni

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog