Friday, October 9, 2015



Baada ya klabu ya Liverpool kumfukuza kazi aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Brendan Rodgers kutokana na mwenendo mbovu wa timu yao, watu mbalimbali katika uchambuzi wa masuala ya soka wamekuwa wakizungumza mitazamo tofauti tofauti kuhusiana na maamuzi hayo.
October 9 kocha wa klabu ya Arsenal ya Uingereza Arsene Wenger amezungumzia kuhusiana na mtazamo wake juu ya uamuzi wa viongozi wa Liverpool kumfuta kazi Brendan Rodgers, Wenger ambaye timu yake ya Arsenal iliwahi kupitia katika wakati mgumu kwa miaka kadhaa ila hakufukuzwa kazi.
2D3C29B300000578-0-image-a-27_1444390674750
Wenger na Rodgers wakipeana mikono katika mechi timu zao zilipo kutana.
Wenger ana amini Rodgers angepewa zaidi ya mechi nane za kuendelea kuifundisha timu hiyo ili klabu iweze kuamua >>>”walikuwa katika nafasi nzuri ya kuwania ubingwa katika miaka miwili iliyopita lakini sasa sielewi kwa nini wamefanya hivi, sioni sababu za msingi za kufanya uamuzi wa haraka namna hii, kwangu mimi ni ngumu kuelewa”
2D2D6C4A00000578-3266324-image-a-1_1444399238639
Klabu ya Liverpool ya Uingereza haijawahi kutwaa ubingwa wa Uingereza toka mwaka 1990, lakini katika historia imetwaa taji hilo mara 18, lakini klabu hiyo ni moja kati ya vilabu vilivyotwaa taji la Ligi Kuu Uingereza mara nyingi zaidi. Hivyo kwa sasa klabu ya Liverpool imemchagua Jurgen Klopp.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog