Masaa machache baada ya Rais wa FIFA Sepp Blatter kusimamishwa kuliongoza shirikisho hilo, kiongozi wa shirikisho la soka Afrika Issa Hayatou kutoka Cameroon amepewa jukumu la kuongoza shirikisho hilo kwa muda.
Hayatou atachukua nafasi hiyo kufuatia kusimamishwa kazi kwa Rais wa
FIFA Sepp Blatter kwa muda wa siku 90 na Kamati ya Maadili ya shirikisho
hilo.Hayatou, ambaye aliongoza CAF tangu mwaka 1988, pia alikuwa makamu wa rais katika kamati ya utendaji ya Fifa aliyehudumu muda mrefu zaidi.
Blatter amesimamishwa kwa muda wa siku 90 kufuatia kashfa mpya ambayo imeibuka hivi karibuni ndani ya shirikisho hilo ikihusisha malipo ya fedha ambazo ziliandikishwa kwa akaunti ya rais wa shirikisho la vyama vya soka barani Ulaya Michel Platinni
Rais mpya wa FIFA atapatikana Februari 26, 2016.
0 maoni:
Post a Comment