Sunday, October 4, 2015


Sergio Agüero Alifunga tena bao mbili haraka dakika ya 49 na 50 na kujifanyikia kupata hat-trick yake kwa kupiga bao tatu na kufanya bao ziwe 3-1. Bao la nne lilifungwa na Kevin De Bruyne dakika ya 53 na tena dakika ya 60 Sergio Agüero alifunga bao la tano na kisha dakika ya 62 Sergio Agüero akafunga la 6 na kufanya matokeo kuwa 6-1.Raha  ya bao!Sergio Agüero dakika ya 42 aliwasawazishia bao Man City na kufanya mtanange kwenda mapumziko zikiwa sare ya bao 1-1, Bao la Newcastle United lilifungwa na Aleksandar Mitrovic mapema dakika ya 18'
Man City wametwaa uongozi wa Ligi Kuu England baada ya Leo kuichapa Newcastle Bao 6-1 Uwanjani Etihad huku Straika wao Sergio Aguero akipiga Bao 5.
City walitanguliwa Bao 1-0 kwa Bao la Dakika ya 18 la Aleksandar Mitrovic lakini Aguero alisawazisha Dakika ya 42 na Mechi kwenda Haftaimu ikiwa 1-1.
Kipindi cha Pili, Aguero aliongeza Bao 4 katika Dakika za 49, 50, 60 na 62 wakati Kevin De Bruyne akifunga katika Dakika ya 53.
Ushindi huu umewapa uongozi wa Ligi City wakiwa na Pointi 18, Pointi 2 mbele ya Man United ambao kesho wako Emirates kucheza na Arsenal.

Aguero alipofunga bao la kwanzaPisha njia!
VIKOSI:
Man City:
Hart, Zabaleta, Otamendi, Mangala, Kolarov, Fernando, Fernandinho, De Bruyne, Silva, Sterling, Aguero.
Subs: Sagna, Caballero, Bony, Jesus Navas, Demichelis, Iheanacho, Garcia.
Newcastle: Krul, Janmaat, Mbemba, Coloccini, Mbabu, Sissoko, Wijnaldum, Anita, Gouffran, Mitrovic, Perez.
Subs: Williamson, Cisse, De Jong, Lascelles, Thauvin, Elliot, Tiote.
Referee: Kevin Friend

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog