Klabu ya Manchester United ya Uingereza ni moja kati ya vilabu vilivyotumia fedha nyingi katika dirisha la usajili lililofungwa mwezi August 2015. Toka kocha Louis van Gaal ajiunge na klabu ya Man United, uongozi wa klabu hiyo umetumia zaidi ya pound milioni 250 kwa ajili ya kusajili wachezaji.
Man United inaonekana kufanya usajili kwa malengo ya baadae zaidi kwani imekuwa ikisajili wachezaji wenye umri mdogo kama Memphis Depay, Anthony Martial na Morgan Schneiderlin. Stori kutoka kwa makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Ed Woodward kuhusu matumizi hayo ya fedha yaliyotumika katika usajili.
Ed Woodward amekiri kuwa bado Manchester United itaendelea na matumizi ya fedha nyingi kwa ajili ya kuimarisha kikosi chake, Ed Woodward amesema Man United
katika dirisha la usajili lililofungwa mwezi August walikuwa
wakihusishwa kutaka kusajili wachezaji wengi zaidi lakini walifanikiwa
kusajili sita. Hivyo Man United bado itaendelea kutumia fedha nyingi
katika usajili ili kuimarisha kikosi.
0 maoni:
Post a Comment