Nahodha mpya wa Uholanzi, Arjen Robben alitoka uwanjani baada ya dakika 27 tu kufuatia kuumia nyonga PICHA ZAIDI GONGA HAPA
TIMU
ya taifa ya soka ya Iceland imejisogeza kukata tiketi ya kufuzu kucheza
mchuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya, Euro 2016 baada ya ushindi wa
penalti ya utata ya Gylfi Sigurdsson w 1-0 dhidi ya Uholanzi waliomaliza
pungufu ya mchezaji mmoja usiku wa jana.
Refa Milorad Mazic wa Serbia, aliyemtoa kwa kadi nyekundu Martins Indi dakika ya 33, aliwazawadia
mkwaju wa penalti Iceland dakika ya 51 ingawa Gregory van der Wiel
alionekana kuuwahi moira wakati anapambana na Birkir Bjarnason.
Sigurdsson
akaenda kufunga penalti hiyo akimtungua kipa Jasper Cillessen na
kuiweka Iceland katika mazingira mazuri ya kukata tiketi ya kwanza ya
fainali za michuano mikubwa.
Matokeo
hayo yanaiweka Uholanzi katika mazingira magumu kidogo katika kundi
hilo A kutokana na Iceland kutimiza pointi 18, mbili zaidi ya Jamhuri ya
Czech wanaoshika nafasi ya pili. Uholanzi inabaki na pointi zake 10.
Iceland sasa wanaweza kujihakikishia kucheza Euro 2016 iwapo tu watashinda mchezo wa nyumbani dhidi ya Kazakhstan Jumapili.
Kipigo
hicho kinamuweka pabaya kocha mpya wa Uholanzi, Danny Blind. Kocha
aliyetangulia Guus Hiddink alilazimika kujiuzulu kwa sababu ya matokro
mabaya hususan baada ya timu hiyo kufungwa mabao 2-0 nchini Iceland
mwezi Oktoba.
Mshambuliaji
Robin van Persie, ambaye aliiongoza safu ya ushambuliaji ya timu hiyo
katika fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil zaidi ya mwaka mmoja
uliopita, jana aliwekwa benchi na kocha Blind.
Kikosi
cha Uholanzi kilikuwa; Cillessen, Van der Wiel, De Vrij, Martins Indi,
Blind, Wijnaldum/Promes dk80, Klaassen, Robben/Narsingh dk31, Sneijder,
Depay na Huntelaar/Bruma dk40.
Iceland;
Halldorsson, Saevarsson, Arnason, Ragnar Sigurdsson, Ari Freyr
Skulason, Bodvarsson/Finnbogason dk78, Gylfi Sigurdsson,
Gunnarsson/Olafur Ingi Skulason dk86,Birkir Bjarnason, Gudmundsson na
Sigthorsson/Gudjohnsen dk64).
0 maoni:
Post a Comment