Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Ufaransa Thierry Henry, ameongea maneno ya kumtetea kocha wa Arsenal Arsene Wenger baada ya kufungwa kwa dirisha la usajili. Henry ambaye ana heshima kubwa katika klabu hiyo amemkingia kifua Wenger juu ya lawama za kuto sajili.
Licha ya kuwa Henry kauli yake ya mwanzoni ilikuwa ni kumshawishi Wenger asajili mshambuliaji wa kati mmoja mahiri, akiwa anaamini kuwa Arsenal haiwezi twaa taji la Ligi Kuu Uingereza kwa Olivier Giroud pekee, sasa ana kauli tofauti kidogo, kwani baada ya dirisha la usajili kufungwa Henry ana mtetea Wenger na kusema ana kikosi imara.
”
Sifikirii kama Wenger hakutaka kusajili wachezaji wengine kama ndivyo
hilo lingekuwa suala jingine lakini alisema kama mipango yake itakuwa
imekamilika atajaribu kusajili, lakini unampataje Benzema kutoka Real
Madrid ambapo anacheza kila wiki na Cavani kutokea PSG ambaye anafunga
magoli? ni ngumu”>>> Henry
“Sifikirii
kama hakutaka kusajili mchezaji yoyote, alitaka kusajili kama
tulivyokuwa tunajua ila suala hilo halikutokea. Sioni kama wanaelekea
kuchukua ubingwa wa Ligi msimu huu, lakini nafikiri Wenger anaamini
atashinda ubingwa wa Ligi akiwa na timu hiyo ni nzuri kwa mtazamo
wake”>>> Henry
Arsenal ambayo ipo nyuma ya Manchester City kwa point tano haijafanya usajili wowote mkubwa katika dirisha hili la usajili zaidi ya kumsajili aliyekuwa golikipa wa Chelsea Peter Cech. Hivyo wapenzi na mashabiki wa klabu hiyo hawana imani na mwenendo wa sasa wa timu yao.
0 maoni:
Post a Comment