Baadhi ya wachezaji wa Taifa Stars kutoka kulia Farid Mussa, Mrisho Ngassa, Mwinyi Hajji Mngwali, Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta |
TANZANIA
itahitimisha mechi za mzunguko wa kwanza wa Kundi G kufuzu Fainali za
Mataifa ya Afrika 2017 Machi mwakani, itakapoifuata Chad.
Taifa Stars Jumamosi imejiweka njia panda katika mbio za AFCON 2017, baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na Nigeria, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Taifa Stars sasa inakamilisha mechi mbili za Kundi G bila ushindi, baada ya awali kufungwa mabao 3-0 na Misri mjini Alexandria Juni mwaka huu, wakati Nigeria inafikisha pointi nne baada ya awali kushinda 2-0 dhidi ya Chad.
Misri watakuwa wageni wa Chad Jumapili kukamilisha raundi ya pili ya Kundi G. Wote Tanzania na Nigeria wataiombea mabaya Misri Jumapili ifungwe ili isipae zaidi katika kundi hilo.
Lakini Misri wanapewa nafasi kubwa ya kushinda na matokeo mabaya sana kwao yanaweza kuwa sare, kwani Chad si timu ya kubeza sana.
Tanzania bado ina nafasi japo finyu ya kwenda Gabon mwaka 2017, iwapo itashinda mechi zake zilizobakia kuanzia ya Machi 25 mwakani dhidi ya Chad.

MSIMAMO WA KUNDI G
Na | Timu | P | W | D | L | GF | GA | GD | Pts |
1 | Nigeria | 2 | 1 | 1 | 0 | 2 | 0 | 2 | 4 |
2 | Misri | 1 | 1 | 0 | 0 | 3 | 0 | 3 | 3 |
3 | Tanzania | 2 | 0 | 1 | 1 | 0 | 3 | -3 | 1 |
4 | Chad | 1 | 0 | 0 | 1 | 0 | 2 | -2 | 0 |
0 maoni:
Post a Comment