KLABU ya
Simba imeendeleza wimbi la ushindi kwenye mechi za kirafiki baada ya
kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya URA ya Uganda.
Kwenye
mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam mabao ya Simba
yalifungwa na Kelvin Ndayisenga kwenye dakika ya nne ya mchezo huo na bao la
pili likiwekwa kimiani na beki Juku Mushood kutoka Uganda.
Bao la la
URA lilifungwa na Kalanda Frank kwenye dakika ya 19 baada ya kutokea piga
nikupige kwenye lango la Simba na mfungaji kupiga mpira uliompita kipa Peter
Manyika na kuzaa bao hilo.
Mchezo huo
ulianza kwa kasi huku timu zote zikishambuliana kwa zamu ingawa waliwa Simba
waliotangulia kufunga kwenye dakika ya nne na mchezaji wao mpya Kelvin
Ndayisiyenga kuiandikia timu hiyo bao la kuongoza.
Hata hivyo
bao hilo lilidumu kwa dakika 15 kwani URA walifanikiwa kusawazisha kupitia kwa
mshambuliaji wake Kalanda Frank baada ya kutokea piga nikupige kwenye lango la
Simba.
Baada ya bao
hilo timu hizo zilishambuliana kwa zamu na dakika ya 36 Simon Sserunkuma
anakosa bao la wazi lakini mpira alilopiga lilikwenda pembeni ya lango la URA
kabla ya shuti dhaifu la Abdi Banda kudakwa na kipa wa URA Mwete Brian.
Kalanda
Frank alikaribia kuifungia URA bao la pili lakini shuti lake liligonga mwamba
na kuokolewa na mabeki wa Simba na dakika ya 42 Kagimu Fatiq alipiga mpira
ulioishia mikononi mwa kipa Peter Manyika.
Kipindi cha
pili kilianza kufanya mabadiliko saba kwa kuwapumzisha Awadh Juma na kuingia
Said Ndemla, Abdi Banda akaingia Justice Majibva, Issa Abdallah akaingia Mwinyi
Kazimoto, Emery Nimuboma akaingia Ramadhani Kessy, Samih Nuhu akaingia Mohamedi
Hussein, Simon Sserunkuma akaingia Peter Mwalyanzi na Said Issa akaingia Hassan
Isihaka.
0 maoni:
Post a Comment