Monday, July 13, 2015



TP Mazembe imecheza mechi ya pili mfululizo bila ya ushindi, baada ya usiku wa jana kulazimishwa sare ya bila kufungana na wenyeji Moghreb mjini Tetouan, Morocco katika mchezo wa Kundi A Ligi ya Mabingwa Afrika.
Watanzania Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta wote walicheza mechi hiyo ya ugenini.
Ulimwengu alicheza dakika zote 90 akionyeshwa kadi ya njano dakika ya 77, wakati Samatta alitolewa dakika ya 83 kumpisha Jonathan Bolingi.
Matokeo hayo yanakuja wakati Al Hilal ya Sudan iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Smouha ya Misri mjini Omdurman jana pia.
Hilal ambayo ililazimisha sare ya 0-0 na Mazembe katika mchezo wa kwanza mjini Lubumbashi, sasa inapanda kileleni mwa kundi hilo kwa pointi zake nne, ikifuatiwa na Smouha pointi tatu.
Mazembe inashika nafasi ya tatu kwa pointi zake mbili, wakati Moghreb Tetouan yenye pointi moja inashika mkia.
Mechi za kundi B, ES Setif iliwafunga Waalgeria wenzao MC Eulma 1-0 wakati El Merreikh ilifungwa 1-0 na USM Alger ya Algeria pia.
Sasa USM Alger inaongoza kundi hilo kwa pointi zake sita, ikifuatiwa na El Merreikh pointi tatu sawa na ES Setif wakati MC Eulma haina pointi baada ya kupoteza mechi zote mbili za mwanzo.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog