Uchaguzi Mkuu wa Rais Burundi umefanyika tayari japo kulikuwa na mvutano mkubwa sana kutokana na ishu ya kuonekana Rais Pierre Nkurunziza kugombea kwa mara ya tatu ilikuwa ni kwenda kinyume na kanuni za nchi hiyo.
Matokeo yametolewa July 24 2015 na matokeo yameonesha Rais Nkurunziza ameshinda tena Uchaguzi huo kwa kupata 69.4% ya kura na kumshinda mpinzani wake wa karibu Agothon Ruwasa aliyepata 18.9 %.
Kulikuwa na jumla ya Wagombea nane kwenye nafasi hiyo lakini Wagombea wengine walijitoa kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi huo.
0 maoni:
Post a Comment