Yanga SC wanafungua dimba na Gor Mahia ya Kenya leo Kombe la Kagame |
KIPYENGA cha michuano ya 40 ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame kinapulizwa leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kutakuwa na mechi tatu katika siku ya kwanza leo kwenye viwanja viwili tofauti, kwanza KMKM ya Zanzibar na Telecom ya Djibouti kuanzia Saa 8:00 mchana na baadaye wenyeji Yanga SC dhidi ya Gor Mahia ya Kenya Saa 10:00 jioni Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, muda ambao pia APR ya Rwanda itamenyana na Al Shandy ya Sudan Uwanja wa Karume.
Waziri wa Ujenzi, Dk John Pombe Joseph Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa michuano hiyo na mgombea huyo wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (CCM) atawasili muda mfupi kabla ya mechi rasmi ya ufunguzi wa Kagame ya 40 kuanza, kati ya Yanga na Gor.
Michuano hiyo ina makundi matatu, A likijumuisha timu za Yanga SC, KMKM, Telecom na Gor Mahia wakati wenyeji wengine, Azam FC wapo Kundi C pamoja na Malakia ya Sudan Kusini, Adama City ya Ethiopia na KCCA ya Uganda na Kundi B kuna APR ya Rwanda, Al-Shandy ya Sudan, LLB AFC ya Burundi na Heegan FC ya Somalia.
Azam FC itafungua dimba na KCCA Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Saa 10: 00 jioni mchezo utakaotanguliwa na mechi nyingine kati ya Adama City na Malakia utakaonza Saa 8:00 mchana, wakati jioni Saa 10:00 Uwanja wa Karume, LLB AFC itamenyana na Hegaan FC.
Mabingwa wa michuano hiyo, El Merreikh ya Sudan hawakuja kutetea taji, kwa sababu wapo kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Washindi wa pili wa Ligi Kuu ya Sudan, El Hilal pia nao hawajaja kwa kuwa wapo kwenye hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Simba SC ndiyo timu iliyotwaa mara nyingi zaidi Kombe la Kagame |
0 maoni:
Post a Comment