Promota
wa Ngumi za Kulipwa, Shomari Kimbau (katikati) akiwa ameshika mkanda
ambao utapiganiwa na bondia Abdallah Pazi (kushoto) na Iman Mapambano
(kulia) kwenye ukumbi wa Vijana Kinondoni siku ya Idd pili katika uzito
wa kilo 76 light heavy raundi 10. (Picha na Rahel Pallangyo)
BONDIA Abdallah Pazi anatarajiwa kupanda ulingoni Idd Pili kwenye ukumbi wa Vijana Kinondoni kuchuana na Iman Mapambao katika pambano la ubingwa wa Taifa lililoandaliwa na promota mkongwe Shomari Kimbau chini ya Chama cha Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC).
Akizungumza na waandishi wa habari jana Kimbau alisema Pazi atapambana na Mapambao katika uzito wa kilo 76 light heavy raundi 10 ambapo mshindi atapambana na Mkenya Daniel Wanyonyi katika pambano la Afrika Mashariki litakalofanyika mwezi ujao.
“Maandalizi yanakwenda vizuri, tunategemea pambano litakuwa la kuvutia kutokana na kuwaleta mabondia vijana wenye uwezo ambao watakuwa tegemeo baadaye katika mapambano ya kimataifa,”alisema.

0 maoni:
Post a Comment