Jumamosi
Mei 30, Uwanjani Wembley, Jijini London kuanzia Saa 1 na Nusu Usiku,
Arsenal na Aston Villa zitagombea FA CUP kwenye Fainali na tayari
vijembe vishaanza kutembea. Mchezaji wa Aston Villa, Ashley Westwood, ameonya kuwa Wachezaji wa Arsenal hivi sasa hawapati usingizi kwa kumwota Straika hatari wa Villa Christian Benteke.
Westwood amesema: "Benteke sasa amerejea katika ubora wake. Arsenal hawatapenda kucheza nae."
Mwanzoni mwa Msimu, chini ya Meneja alietimuliwa Paul Lambert, Benteke alififia na kisha kuandamwa na Majeruhi lakini sasa chini ya Meneja mpya, Tim Sherwood, Straika huyo ameibuka upya.
RSS Feed
Twitter
8:21 AM
Unknown
0 maoni:
Post a Comment