Friday, March 27, 2015

Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana (hawapo pichani) kuhusu maandalizi ya tamasha hilo litakalofanyika Aprili 5, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe. Kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi, Jimmy Charles. (Picha na Francis Dande)
Msama akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya tamasha hilo.

Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Jimmy Charles akifafanua jambo.
********************
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Pasaka litakalofanyika Aprili 5 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi, Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema maandalizi ya tamasha hilo yamekamilika kwa asilimia 97 hivyo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi siku hiyo.
Alisema wameshakamilisha maandalizi ya tamasha hilo, ila kinachosubiriwa ni waimbaji wa kimataifa Ephraim Sekeleti wa Zambia, Ifeanyi Kelechi kutoka Uingereza, Rebeca Malope na Thori Mahlangu wote kutoka Afrika Kusini pamoja na Faustine Munishi ‘Malebo’ kuanza kuwasili nchini.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog