Tuesday, December 9, 2014


MANCHESTER UNITED wameendelea kugawa dozi mfululizo baada ya leo tena kuichapa bao 2-1 timu ya Watakatifu Southampton kwenye Uwanja wao wa Saint Mary. Bao za United zilifungwa zote na Mshambuliaji wao Matata Robin Van Persie. bao la kwanza lilifungwa dakika ya 12 kipindi cha kwanza baada ya kuwatoka Mabeki wa Southampton na kufunga bao hilo. Nao Southampton waliongeza mashambulizi kipindi cha kwanza dakika ya 31 Graziano Pelle aliwasawazishia bao Southampton dakika ya 31 na kufanya 1-1. Hadi mapumziko Southampton 1-1 na Man United. Kipindi cha kwanza pia hakikumalizika vyema kwani Kijana wa Van Gaal Chris Smalling aliondoshwa njee baada ya kuumia mguu na kulazimika kutoka na nafasi yake kuchukuliwa na John Evens.Kipindi cha pili United walifanya mabadiliko na dakika ya 71 baada ya kupigwa frii kiki na van Persie kuunganisha mpira huo hadi nyavuni na kufanya 2-1 dhidi ya wenyeji Southampton ambao kipigo hiki ni cha tatu mfululizo. Ushindi huu umeifanya man united kupanda hadi nafasi ya tatu wakiwa na point 28, Kileleni akiwepo Chelsea mwenye pointi 36 na nafasi ya pili ni Man city mwenye pointi 33.Graziano Pelle aliwasawazishia bao Southampton dakika ya 31 na kufanya 1-1.Rooney akiwa kwenye patashika za kukabana na mchezaji wa Southampton Steven Davis kwenye Uwanja wa Saint Mary usiku huu.
Robin van Persie aliwapachikia bao mapema dakika ya 12 baada ya kuwatoka mabeki wa Southampton.VIKOSI:
  • Manchester United substitutes: Lindegaard, Evans, Fletcher, Herrera, Januzaj, Wilson, Falcao.
  • Manchester United (3–4-1-2): De Gea; McNair, Smalling, Rojo; Valencia, Fellaini, Carrick, Young; Mata; Rooney, Van Persie.
  • Southampton substitutes: K. Davis, Targett, Gardos, Isgrove, Reed, Hesketh, Mayuka.
  • Southampton (4-2-3-1): Forster; Clyne, Fonte, Yoshida, Bertrand; S. Davis, Wanyama; Tadic, Long, Mane; Pelle.
0 comments

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog