JANA Usiku huko Marrakech, Nchini Morocco, ndani ya Le Grand Stade de Marrakech
Unaopakia Watu 45240, Mabingwa wa Ulaya Real Madrid wameichapa San Lorenzo ya Argentina Bao 2-0 na kutwaa Kombe la Dunia kwa Klabu.
Hii ni mara ya kwanza kwa Real kutwaa Kombe hili ambalo ni Mashindano ya FIFA ingawa wameshawahi kutwaa Intercontinental Cup mara 3 ambalo lilikuwa likifanana na hili ingawa hilo lilishindaniwa na Mabingwa wa Ulaya dhidi ya Mabingwa wa Marekani ya Kusini tu.
Bao za Real hapo Jana zilifungwa na Sergio Ramos na Gareth Bale huku Mchezaji Bora Duniani, Cristiano Ronaldo, akipata nafasi moja tu ya kufunga ambayo Kipa Torrico aliakoa.
Hivi sasa Real wapo kwenye wimbi la ushindi wa Mechi 22 mfululizo na wanaikimbiza Rekodi ya Dunia ya kushinda Mechi 24 mfululizo inayoshikiliwa na Klabu ya Brazil, Curitiba, waliyoiweka Mwaka 2011.
Real pia wamekamataTaji lao la 4 kwa Mwaka 2014 kitu ambacho walikuwa hawajahi kukifanya baada ya kuwahi kutwaa Mataji Matatu tu ndani ya Mwaka mmoja lakini Mwaka huu 2015 wamefanikiwa kubeba UEFA CHAMPIONS LIGI, Copa del Rey, UEFA SUPER CUP pamoja na Kombe la FIFA la Klabu Bingwa Duniani.
Vile vile wamemaliza Mwaka 2014 kwa kuwa Vinara wa Ligi ya kwao Spain La Liga wakiwa Pointi 1 mbele ya Mahasimu wao FC Barcelona ambao wamecheza Mechi moja zaidi.
Mapema hiyo Jana, kwenye Mechi ya kusaka Mshindi wa 3, Auckland City ya New Zealand iliishinda Cruz Azul kwa Mikwaju ya Penati 4-2 baada ya Sare ya Bao 1-1.
0 maoni:
Post a Comment