BENDI ya muziki wa Dansi ya Malaika chini ya Christian Bella ‘Obama’ usiku huu ilitoa Burudani kali ya kukata na shoka kwenye ukumbi wa Lina's Night Club Bukoba ikiwa ni kumalizia sikukuu za X-mass siku ya Boxing Day" na kuwapagawisha mashabiki kwa shoo kali na ya nguvu.
Onyesho hilo lililoanza saa mbili usiku ambapo Malaika Bendi walikuwa wakiwapa ladha mashabiki kwa kupiga kopi mbalimbali ya nyimbo za Kikongo zinazobamba.
Ilipofika saa nne na nusu ukumbi ulilipuka kwa shangwe baada ya kiongozi wa bendi hiyo Christian Bella kupanda jukwaani kwa wimbo wake wa Yako Wapi Mapenzi ambao ulisababisha mashabiki kuinuka katika viti vyao na wale ambao walikuwa wakinyemelewa na usingizi kuamka.
Bella alizidi kuwapagawisha mashabiki kwa kupiga nyimbo kali mfululizo ambazo zinatamba katika redio na vyombo mbalimbali vya habari ukiwemo Nani Kama Mama, Yako wapi Mapenzi, Msaliti, Usilie na nyingine kibao.
Boxing Day Ijumaa.

Dada nao hawakuwa nyuma


Jamal na Mkewe nao walikuwepo ukumbin Lina's Night Club kushuhudia Bendi hiyo Live


Mtu wa Watu Ben Mulokozi













Wadau wa Muziki wa Dansi...Bendi..


Wafanyakazi wa shirika la Cosad nao walitokelezea kwa namna yao siku ya Boxing Day na hapa walipata picha na Bella









0 maoni:
Post a Comment