Hetitriki ya Sergio Aguero imeweka hai matumaini ya Man City kufuzu kuingia Raundi ya Mtoano baada ya kuwafunga Mtu 10 Bayern Munich Bao 3-2 huku Aguero akipiga Bao 2 Dakika 5 za mwisho wakati Bayern walikuwa mbele 2-1.
Man Citywalipewa Penati Dakika ya ya 20 kufuatia Sentahafu Medhi Benatia kumwangusha Sergio Aguero ambae alifunga Penati hiyo huku Benatia akipewa Kadi Nyekundu.
Bayern walisawazisha kwa Bao la Alonso Dakika ya 40 na Robert Lewandowski kuwapa Bao la Pili Dakika ya 45.
Bao 2 nyingine za Aguero zilifungwa Dakika za 85 na 90.
Kwenye Mechi ya awali iliyochezwa huko Moscow, AS Roma waliongoza kwa Bao la Francesco Totti katika Dakika ya 43 lakini CSKA walisawazisha Dakika za Majeruhi kwa bahati tu kupitia Berezutski.
Bao za Bayern Munich zilifungwa na Xabi Alonso dakika ya 40 kwa frii kiki na bao la pili kufungwa na Robert Lewandowski katika dakika ya 45 kwa kichwa safi.
0 maoni:
Post a Comment