Kipindi
cha Pili Man United walianza kwa kumtoa Ander Herrera na kumwingiza
Marouane Fellaini ambae aliwapa manufaa makubwa kwa kusawazisha kwa Bao
safi katika Dakika ya 48 na hilo ni Bao lake la kwanza kwa Man United
katika Ligi.
Lakini
udhaifu wa Difensi ya Man United, wakati wakiwa wanatawala Gemu,
uliwapa WBA mwanya mkubwa kupiga Bao la Pili Dakika ya 66 kupitia Saido
Berahino.
Man
United waliweza kusawazisha Dakika ya 87 baada ya Krosi ya Rafael
kuokolewa na kumkuta Daley Blind aliepiga kiakili kufunga. Sare hii
imewaweka Man United Nafasi ya 6 wakiwa Pointi 10 nyuma ya Vinara
Chelsea ambao Jumapili ijayo watatua Old Trafford kuivaa Man United
katika mtanange unaongojewa kwa hamu.
Fellaini akishangilia na Van Persie jana walipoingia na kutupia bao la kusawazisha..
0 maoni:
Post a Comment