
Mwakilishi
wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ambaye pia ni
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko (kushoto)
akisalimiana na baadhi ya Wanamichezo waliokuwa kwenye Mashindano ya
Jumuiya ya Madola mjini Glasgow Scotland mara walipowasilia katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
jana.

Kaimu
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Bibi. Juliana Yassoda akiwaelekeza jambo baadhi ya
Wanamichezo waliwakirisha Tanzania kwenye Mashindano ya Jumuiya ya
Madola mjini Glasgow Scotland mara walipowasilia katika Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana.

Katibu
Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Bw. Filbert Bayi akifurahia
jambo na baadhi ya wanamichezo walikuwa wamewakilisha nchini katika
mashindano ya Jumuiya ya Madola mjini Glasgow Scotland mara baada ya
kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini
Dar es Salaam jana.

Mkurugenzi
wa Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Profesa Hermas Mwansoko Akizungumza kwa niaba ya Serikali na
wanamichezo waliokuwa kwenye Mashindano ya Jumuiya ya Madola mjini
Glasgow Scotland mara wakati wa hafla fupi ya mapokezi iliyofanyika
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jan.Kulia ni Katibu wa Kamati ya
Olimpiki Tanzania (TOC) Bw. Filbert Bayi.
Katibu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Bw. Filbert Bayi akizungumza
na wanamichezo waliokuwa kwenye Mashindano ya Jumuiya ya Madola mjini
Glasgow Scotland wakati wa hafla fupi ya mapokezi iliyofanyika jana
katika Ukumbi uliopo Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.wa tatu kutoka
kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermas
Mwansoko, Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Bibi. Juliana Yassoda
na Meneja wa Uwanja wa Taifa Bw. Rish Urio

Mwakilishi
wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ambaye pia ni
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko
akikabidhiwa Bendera ya Taifa na Kapteni wa Timu ya Taifa iliyoshiriki
mashindano ya Jumuiya ya Madola Bw. Seleman Kidunda, mara baada ya
kurejea nchini jana jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia kutoka kushoto
ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Bibi. Juliana Yassoda,
Meneja wa Timu hiyo Muharami Mchume na Katibu wa Kamati ya Olimpiki
Tanzania (TOC) Bw. Filbert Bayi
Baadhi
ya wanamichezo walioshiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola mjini
Glasgow Scotland, wakiwa nje ya uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius
Nyerere mara baada ya kuwasili nchini jana jijini Dar es Salaam.
0 maoni:
Post a Comment