Saturday, August 16, 2014


KIUNGO wa Argentina Javier Mascherano amekubali kusaini Mkataba mpya na Klabu yake Barcelona utakaomweka huko Nou Camp hadi Mwaka 2018.
Habari hizi zimetangazwa na Klabu ya Barcelona hii Leo na pia wamethibitisha Mchezaji huyo amesharudi Mazoezini baada ya kupewa muda zaidi wa kupumzika kufuatia Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil ambapo Argentina ilifungwa 1-0 na Germany kwenye Fainali Julai 13.
Imedokezwa kuwa ndani ya Mkataba huu mpya wa Mascherano kipo Kipengele kinachotaka ilipwe Euro Milioni 100 ikiwa atatakiwa kuhama kabla Mkataba wake kumalizika.
Mascherano ameichezea Barcelona Mechi 184 tangu ahamie hapo kutoka Liverpool Agosti 2010.

Mara nyingi Barcelona imekuwa ikimtumia kama Sentahafu licha ya yeye kuwa Kiungo mahiri kutokana na Barcelona kuwa na mapengo kwenye safu yao ya Difensi kutokana na majeruhi na kukosa Wachezaji wa Akiba wazuri wa nafasi hiyo.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog