Akizungumza na Mwanaspoti, Coutinho raia wa Brazil alisema kwa sasa bado
hawezi kusema moja kwa moja kuwa ana uhakika wa kuingia katika kikosi
cha kwanza cha Yanga kwa vile hajajua uwezo wa wenzake wanaocheza nafasi
kama yake ambao wapo katika vikosi vya mataifa yao.
KIUNGO wa Yanga, Mbrazil Andrey Coutinho
(pichani )amesema anafurahia zaidi staili ya uchezaji ya kiungo Nizar
Khalfan na kwamba ndiye kiungo anayejua zaidi wapi kwa kumwekea mpira
anapokuwa akikimbia.
Coutinho aliliambia Mwanaspoti kuwa, “ Yanga ina
viungo wengi na wote wazuri lakini nimependa jinsi Nizar anavyocheza
kwani anaonekana kujua jinsi mimi ninavyotaka kupewa pasi nikiwa
nakimbia.
“Kwanza naona ana nguvu lakini pili anapiga pasi
kwa kukuwekea pale ulipo, napenda hata kwenye mazoezi niwe napangwa naye
kwani ananifanya nicheze kwa ufasaha zaidi na kufanya malengo yangu
kutimia vizuri.
“ Pia ana uwezo mzuri wa kupiga pasi pia kupiga
mashuti ya nguvu ambayo yanaweza kuwa na faida pale kipa anapotema na
straika wetu akanasa mpira,” alisema.
Katika hatua nyingine kiungo huyo amesema kuwa
bado hajawa mpenzi wa vyakula vya Kitanzania kwa kuwa hapendezwi sana na
ulaji wa vyakula vingi vya Kitanzania vya asili.
“Vyakula vya asili sijavizoea, nimevizoea vya
kwetu kule Brazil, huku Tanzania napenda zaidi kula kuku, nyama ya
kusaga ‘Beef’ na tambi pamoja na wali kwani ndiyo vyakula ambavyo
utakavyoweza kuvikuta kwetu Brazil,” alisema
RSS Feed
Twitter
6:20 AM
Unknown
0 maoni:
Post a Comment