Rais
wa shirikisho la kandanda ulimwenguni, FIFA, Sepp Blatter,
amethibitisha ilikuwa kosa kuchagua Quatar kuwa mwenyeji wa kombe la
dunia la mwaka wa 2022. Katika mahojiano na televisheni nchini Uswisi,
Sepp Blatter aliulizwa iwapo kuiruhusu Qatar kuwa mwenyeji wa kombe hilo
ambalo huchezwa kati ya mwezi Juni na Julai ilikuwa kosa, hasa
ikizingatiwa kuwa hali ya hewa katika nchi hiyo hufikia hadi nyuzi joto
50 wakati huo. Alijibu kwa kukiri na kuongeza kuwa kila mtu hukosea
maishani. Alipinga madai kwamba taifa hilo lilikuwa limelipia michezo
hiyo. Aliongeza kuwa kamati inayojumuisha maafisa wa FIFA walikuwa
wamekubali uwezekano wa taifa hilo kuwa mwenyeji ijapokuwa walikuwa
wamepokea taarifa kuhusu vipimo vya juu vya joto. Alisema kwamba michezo
hiyo badala yake inaweza kusogezwa hadi miezi ya mwisho wa mwaka,
wakati vipimo vya joto vitakuwa vimepungua.
0 maoni:
Post a Comment