Steven
Gerard alifunga mikwaju miwili ya penalty na kukosa ya tatu Liverpool
ikiendelea kuimarisha matokeo yake baada ya kuwacharaza mabingwa
watetezi wa ligi ya uingereza Machester United tatu bila katika uga wao
wa nyumbani Old Trafford.
Katika
kile kilichoonekana kama harakati za kushinda taji lao la kwanza tangia
mwaka 1990,Liverpool ilipita mtihani wao kwa kuonyesha mchezo mzuri
dhidi ya timu ya Manchester United ambayo haikuweza kuwadhibiti
wapinzani wao na hivyobasi kusogea hadi nafasi ya pili na pointi nne
nyuma ya viongozi wa ligi hiyo Chelsea.
Nahodha wa Liverpool Gerard alionyesha uongozi wake huku wakifazawadiwa mikwaju ya penalty katika vipindi vyote viwili huku timu hiyo ya meneja Brenda Rodgers ikitawala dhidi ya timu ya Machester ambayo inahitaji marekebisho makubwa.
Nahodha wa Liverpool Gerard alionyesha uongozi wake huku wakifazawadiwa mikwaju ya penalty katika vipindi vyote viwili huku timu hiyo ya meneja Brenda Rodgers ikitawala dhidi ya timu ya Machester ambayo inahitaji marekebisho makubwa.
Kutokana
na mechi hizo za leo Chelsea iko katika nafasi nzuri ya kushinda taji
hilo kwa alama 66 ikiwa imecheza mechi 30 huku timu za liverpool na
Arsenal zikiwa na pointi 62 kila mmoja, lakini liverpool inashikilia
nafasi ya pili kwa wingi wa mabao.
Arsenal ni ya tatu huku Manchester City iliocheza mechi 27 ikiwa na pointi 60 na hivyobasi ikifunga udhia wa time nne boraKipindi cha pili Dakika ya 46 Liverpool wanapata penati nyingine, Ni baada ya Jones kumfanyia rafu kwa kumwangusha Allen chini. Steven Gerrard anawapachika bao kwa mkwaju huo na kufanya bao 2-0 dhidi ya Manchester United kwenye uwanja wa Old Trafford.
Dakika ya 77 Nemanja Vidic aliondoshwa nje kwa kadi nyekundu baada ya kufanya rafu kwa Sturridge na mwamuzi kumtoa kwa kadi hiyo nyekundu huku Vidic akimlalamikia kwamba kajiangusha na
Dakika ya 78 Steven Gerrard alikosa penati hiyo iliyogonga mwamba na kurudi ndani na mchezaji wa Man United kuuondosha.
Dakika ya 84 Luis Suárez alipachikia bao la tatu Liverpool na kufanya 3-0 dhidi ya United baada ya mabeki wa United kupitiwa wakidhani ni faulu.Ushindi huu wa Majogoo Liverpool unawapandisha hadi nafasi ya pili wakiwa na pointi 62, Nyuma ya pointi 4 ya vinara Chelsea wenye pointi 66 waliofungwa jana na Aston Villa.Steven Gerrard (kushoto) akishangilia bao lake
Van Persie chupu chupu atupie bao hapa!!
0 maoni:
Post a Comment