Sunday, March 9, 2014



Mchezaji wa Valladolid Fausto Rossi akishangilia bao lake baada ya kuinyuka Barcelona leo hii.BAO la Dakika ya 17 la Fausto Rossi limewapa ushindi Real Valladolid, waliokuwa Nyumbani, wa Bao 1-0 dhidi ya FC Barcelona na kuwanyima Mabingwa hao wa Spain Nafasi ya kushika uongozi wa La Liga.
Kipigo hiki kimewabakiza Barca Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 1 nyuma ya Real Madrid ambao wanacheza Jumapili na Levante.
Ushindi huu umewapandisha Real Valladolid Nafasi 1 na sasa wako Nafasi ya 17.
Baadae Leo Atletico Madrid wapo Ugeni kucheza na Celta de Vigo na ushindi kwao utawashusha Barca hadi Nafasi ya Tatu.


Rossi, Kulia akishangilia bao lake baada ya kumfunga kipa wa Barca Victor Valdes

S

J
Meneja wa  Barcelona Gerardo Martino akiwanyooshea mkono Valladolid
RATIBA/MATOKEO:
Jumamosi Machi 8

Real Valladolid 1 vs  Barcelona 0
20:00 Real Betis vs Getafe CF
22:00 Celta de Vigo v Atletico de Madrid
23:59 Granada CF v Villarreal CF Jumapili Machi 9 14:00 RCD Espanyol v Elche CF 19:00 UD Almeria v Sevilla FC 21:00 Real Madrid CF v Levante 23:00 Valencia v Athletic de Bilbao Jumatatu Machi 10 22:00 Osasuna v Malaga CF 23:59 Real Sociedad v Rayo Vallecano

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog