Afrika
inasherehekea miaka 50 ya umoja wa kisiasa na uchumi unaonawiri, ambapo
bara hilo kwa muda mrefu sasa linaangaliwa kama eneo la neema kubwa,
licha ya ukuaji huo wa kiuchumi kuwa na walakini.
Bara la
Afrika linasherehekea hivi sasa miaka 50 ya Umoja wa Afrika kwa ufanisi
tangu wa kisiasa mpaka wa kiuchumi. Bara hilo linajitokeza kama eneo
lenye fursa kubwa ya kuwavutia wawekezaji. Baada ya "Chui wa Asia" sasa
Simba wa Afrika wananguruma.
Takwimu
zinadhihirisha uchumi utakuwa mwaka huu kwa 7% au zaidi katika robo ya
mataifa yote ya eneo la kusini mwa jangwa la Sahara. Wakati huo huo,
mengi ya mataifa hayo yamo katika lile kundi la mataifa ambayo uchumi
wake unakuwa haraka kupita kiasi.
0 maoni:
Post a Comment