Kocha
Mkuu wa Twiga Stars, Rogasian Kaijage amesema kikosi chake kiko tayari
kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC) dhidi
ya Zambia itakayochezwa keshokutwa (Ijumaa) jijini Lusaka.
Akizungumza
kwenye hafla ya kuiaga timu hiyo iliyofanyika leo (Februari 12 mwaka
huu) kwenye ofisi za TFF jijini Dar es Salaam, Kocha Kaijage amesema
wachezaji wake wako vizuri, ingawa hakuwa tayari kutoa ahadi kuhusu
matokeo.
“Vijana
wako vizuri, lakini sitaki kutoa ahadi. Watanzania watuombee, watuunge
mkono ili tuweze kufanya vizuri,” amesema Kocha Kaijage katika hafla
hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki
Tanzania (TOC), Filbert Bayi.
Twiga
Stars inaondoka na kikosi cha wachezaji 19 na benchi la ufundi lenye
watu watano kwa ndege ya Fastjet kwa ajili ya mechi hiyo itakayooanza
saa 9 kamili kwa saa za Zambia. Msafara wa timu hiyo unaongozwa na
mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF).
Wachezaji
waliopo kwenye kikosi hicho chini ya nahodha Sophia Mwasikili ni Amina
Ali, Anastazia Katunzi, Asha Rashid, Donisia Minja, Esther Chabruma,
Etoe Mlenzi, Everine Sekikubo, Fatuma Issa, Fatuma Makusanya, Fatuma
Mwisendi, Fatuma Omari, Happiness Mwaipata, Maimuna Mkane, Mwapewa
Mtumwa, Sherida Boniface, Therese Yona, Vumilia Maarifa na Zena Said.
Wakati
huo huo, timu ya Azam imeondoka leo alfajiri (Februari 12 mwaka huu)
kwenda Beira, Msumbiji kwa ajili ya mechi ya marudiano ya Kombe la
Shirikisho dhidi Ferroviario da Beira itakayochezwa Jumamosi. Msafara wa
timu hiyo unaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, James
Mhagama.
Naye
mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Nassib Ramadhan ataongoza msafara
wa timu ya Yanga inayoondoka kesho mchana kwenda Comoro kwa ajili ya
mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Komorozine
itakayochezwa Jumamosi.
0 maoni:
Post a Comment