Tuesday, February 18, 2014


Baada ya mara mbili kushindwa kuvuka Hatua ya Makundi ya UCL, Msimu huu Manchester City wamemudu kuvuka hatua hiyo lakini sasa wapo kwenye lindi la Vigogo wa Bara la Ulaya, Barcelona, ambao mashambulizi yao yanaongozwa na Masupastaa wa Argentina na Brazil, Lionel Messi na Neymar.
Man City walimaliza Kundi lao la UCL wakiwa nyuma ya Mabingwa Watetezi Bayern Munich na watatinga kwenye Mechi hii bila ya Straika wao kutoka Argentina, Sergio Aguero, ambae ni Majeruhi ingawa sasa ameanza tena Mazoezi.
Pia, huenda City ikamkosa Kiungo wa Brazil, Fernandinho, ambae alikuwa Majeruhi lakini habari njema kwao ni kupona kwa Kiungo wao, Samir Nasri, ambae Juzi alirudi Uwanjani kwa kupiga Bao walipoichapa Chelsea 2-0 na kuibwaga nje ya FA CUP.
Kurudi kwa Nasri kunaweza kumfanya Meneja wa City, Manuel Pellegrini, aamue kutumia Mfumo wa 4-5-1 na kumfanya Alvaro Negredo kuwa Straika pekee akisaidiwa kwa nyuma na Viungo Samir Nasri na David Silva.
Nao, Barcelona, ambao wametwaa Kombe hili mara 4, wamepata nguvu zaidi baada ya Neymar kupona na Juzi kucheza Mechi ya La Liga na kufunga Bao moja wakati Barca inainyuka Rayo Vellacano Bao 6-0 kwenye Mechi ambayo Messi alifunga Bao 2 na kumfanya awe Mfungaji wa juu kabisa huko Spain alipoivuka Rekodi ya Mchezaji wa Athletic Bilbao Telmo Zarra.
Katika Mechi hiyo, Xavi, Kiungo wa Miaka 34, alipumzishwa lakini ni wazi wakicheza na Man City, atachezeshwa.
Timu hizi hazijakutana katika Mashindano rasmi lakini zimeshacheza Mechi za Kirafiki mara 6.


Barca walishinda Mechi 3 za kwanza, wakafungwa ya nne kwa Penati baada ya Sare ya 1-1 na Man City kushinda Mechi mbili za mwisho ikiwemo ile ya Tarehe 10 Agosti 2003 , Siku ya Ufunguzi wa City of Manchester Stadium, na City kushinda Bao 2-1 kwa Bao za Nicolas Anelka na Trevor Sinclair na la Barca kufungwa na Javier Saviola.
Kwenye Kikosi cha Barca Siku hiyo walicheza Carles Puyol na Xavi Hernández na Iniesta kuingia Kipindi cha Pili.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog