Libya imepata ushindi wake wa
kwanza wa kombe la taifa bingwa Afrika kwa mikwaju ya penalti 4-3 dhidi
ya Ghana mjini Cape Town Afrika Kusini.
Mechi ya fainali kati ya nchi hizo mbili
ilikamilika kwa sare tasa kabla ya Joshua Tijani wa Ghana kukosa bao la
penalti na kuipa Libya ushindi wake.Abdul Mohamed wa Ghana alikuwa na fursa nzuri zaidi kuipa timu yake ushindi katika dakika za ziada za mechi hiyo baada ya dakika 90.
Walinda lango wa timu zote mbili waliokoa mabao mawili kila mmoja kabla ya Tijani kukosa bao lake.
Mechi sita katika kipindi cha siku 20 ikiwemo dakika za ziada kwa kila mechi ya nusu fainali iliyochezwa Jumatano, iliwachokesha wachezaji hao kwani walishindwa kabisa kuiongiza mabao wakati wa mechi kiasi cha kuenda penalti.
Timu zote mbili zilikuwa na nafasi nzuri kupata ushindi katika kipindi cha pili cha mchezo huo ingawa hakuna aliyefanikiwa.
Ikizingatiwa historia ya michuano kati ya nchi hizo mbili, kipindi cha ziada hakikuwa,jambo la ajabu.
Mechi zao mbili walizocheza mwaka huu na katika michuano ya mwaka 2009 iliisha kwa sare ya bao moja. Ghana ilishinda michuano ya mwaka 1982 baada ya timu kwenda sare ya bao moja hadi dakika ya tisini.
Nigeria iliicharaza Zimbabwe 1-0 kuchukua nafasi ya tatu
0 maoni:
Post a Comment