Wachezaji wa Timu ya Simba na baadhi ya viongozi wao wakipozi na kombe lao baada ya kukabidhiwa kwa kuifunga Timu ya Yanga Mabao 3-1 katika mchezo wa Nani Mtani Jembe, jiji DAR ES SALAAM
Meneja wa Yanga, Afidh Ally akipokea mfano wa hundi ya zaidi sh. 98 milioni Kwa kuibuka washindi katika shindano la Nani Mtani Jembe kwa kupata kura nyingi katika unywaji wa bia ya Kilimanjaro.
Hundi ya Simba ilisomeka hivi pamoja na Ushindi Mkubwa walioupata dhidi ya wapinzani wao.
Mgeni Rasmi katika Mchezo huo,Waziri wa Sheria na Katiba,Mh. Mathias Chikawe akikabidhi Kombe la Ushindi wa Nani Mtani Jembe kwa Nahodha wa Timu ya Simba mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa,Jijini Dar es Salaam.
Mshambuliaji wa Timu ya Yanga,Mrisho Ngassa (17),akiwa mpiga chenga ya Mwili Beki wa Timu ya Simba,Donald Mtosi wakati mchezo wao wa Nani Mtani Jembe unaoendelea hivi sasa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Hadi hivi sasa Simba wanaongoza kwa Bao 1-0 na tayari dakika 35 za mchezo zishakatika.Picha zote na Othman Michuzi.
Nahodha wa Timu ya Simba,Henry Joseph Shindika akikabiliana na Mpinzani
wake wakati wa Mtanange wa Nani Mtani Jembe uliopigwa Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam,jioni ya leo.
TIMU ya Simba leo imeifunga Yanga mabao
3-1 kwenye mchezo wa nani mtani jembe na kuondoka na kitita cha milioni
100, medali za dhahabu na kombe.
Simba ambayo haikupewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo kabla ilianza kuandika bao la kwanza kupitia kwa Amis Tambwe aliyefunga mawili huku Juma Awadh akipigilia msumari wa mwisho.
Katika mchezo huo Simba ilianza kuhesabu bao lake la kwanza katika dakika ya 13 lilofungwa na Tambwe baada ya kazi nzuri ya Ndemla.
Wakati Yanga ikijaribu kutaka kusawazisha bao hilo, Simba ilifunga bao la pili kwa mkwaju wa penalti dakika ya 42 iliyofungwa na Tambwe baada ya David Luhende kumuangusha Ramadhani Singano eneo la hatari.
Katika kipindi cha pili, uzembe wa golikipa mpya wa Yanga, Juma ulimuwezesha Awadh Juma kuifungua kirahisi Simba bao la tatu.
Yanga ilipata bao lake la kufutia machozi kupitia kwa mchezaji aliyesajiliwa hivi karibuni, Emmanuel Okwi aliyefunga kwa kichwa dakika ya 89 akiunganisha krosi ya Haruna Niyonzima.
Timu zote zilifanya mabadiliko ya wachezaji katika kipindi cha pili, ambapo Simba iliwatoa, Henry Joseph, Ndemla, Chanongo, Awadh na Ramadhani Redondo, huku nafasi zao zikichukuliwa na Singano, Seleman Uhuru, Zahoro Pazi na Humud.
Huku Yanga ikiwatoa, Athuman Idd ‘Chuji’, Hamisi Kiiza, Didier Kavumbagu, Haroub Cannavaro na Mrisho Ngassa, huku nafasi zao zikichukuliwa na Emmanuel Okwi, Simon Mvusa, Dilunga,Juma Abdul na Jerryson Tegete.
Katika mchezo huo, Yanga ilimpoteza Kelvin Yondani aliyooneshwa kadi nyekundu kwa kumchezea vibaya, Singano.

0 maoni:
Post a Comment