Sunday, November 3, 2013



HUKU akiwa na majonzi ya kuondokewa na baba yake mzazi, Balozi Isaac Abraham Sepetu aliyefariki dunia Jumapili iliyopita kwa ugonjwa wa kisukari, baadhi ya wasanii wanaounda Klabu ya Bongo Movie (muvi) Unity wanadaiwa kuchekelea kifo hicho na kumsusia msiba mwingizaji mwenzao, Wema Isaac Sepetu.

Habari kutoka chanzo chetu makini zilidai kuwa hoja dhaifu iliyo
tumiwa na wahusika hao ni kwamba Wema huwa haendi kwenye misiba ya wenzake hivyo naye amzike baba yake mwenyewe.
MFANO; MSIBA WA SAJUKI

Ulitolewa mfano wa msiba wa aliyekuwa staa wa filamu za Kibongo, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ aliyefariki dunia Januari 2, mwaka huu ambapo Wema alidaiwa alishindwa kufika kwa sababu alikuwa studio akirekodi wimbo wake mpya ambao haujatoka hadi leo.

Wapo waliokwenda mbele zaidi na kudai kuwa hata ukifunua madaftari yao wanapopatwa na misiba huwezi kukuta jina la Wema akiwa amesaini wala kufika.

SHARO, KANUMBA
“Kwa njia moja au nyingine, Wema bwana huwa hashiriki sana katika misiba ya wasanii wenzake, kuna mtu muhimu sana na ana sauti pale Bongo Movie amesema kuwa katika misiba iliyotokea ameshiriki misiba miwili tu, wa marehemu Sharo Milionea (Hussein Mkieti) na (Steven) Kanumba kwa sababu alikuwa mtu wake.

Wanadai mara nyingi amekuwa akijitenga na misiba ya wenzake na wala huwa hatoi hata pole kwa wafiwa kama wafanyavyo wengine wanaposhindwa kufika msibani kutokana na sababu mbalimbali hasa za kimajukumu au kuwa safarini,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:

“Kuna habari za chinichini kuwa walikaa kikao na kukubaliana kutohudhuria msiba wa Wema. Ilitengenezwa meseji ikatumwa kwa memba wote.

Chanzo hicho kiliendelea kudai kuwa kiongozi wa kundi hilo (jina tunalihifadhi kwa sasa) ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa uhamasishaji watu wasiende msibani kwa kigezo cha Wema kutojumuika na watu wengine katika matatizo yao.

WEMA ANASEMAJE?

Akizungumzia ishu hiyo ya kususiwa msiba wa baba yake Wema alisema: “Nimesikitishwa na kitendo hicho. Nahisi siyo sahihi kwa kuwa nimekuwa nikihudhuria misiba ya watu mbalimbali.

“Hawakuwa sahihi kunifanyia hivyo katika kipindi hiki kigumu, hata hivyo, wangekuja kwanza tumzike baba ndiyo nijifunze ila kutokuja kwao hakujanipunguzia chochote.”
Kitendo hicho kilitafsiriwa kuwa ni kama kumuongezea machozi mara mbili kwani tayari alikuwa na chozi la kuondokewa na baba yake kipenzi na la pili likawa ni kususiwa msiba.

Baada ya habari hizo kujaa tele, wanahabari wetu walizungumza na baadhi ya mastaa wanaounda Bongo Muvi juu ya kumsusia msiba Wema ambapo kila mmoja alikuwa na utetezi wake;

Ray: Mh! Kweli Wema haendagi kwenye misiba ya watu hata mimi sikumuona kwa Sajuki ingawa sijui kama alionekana baadaye ila kwa sasa niko sehemu mbaya nitakupigia baadaye tuongee kwa kirefu.

Halima Yahya ‘Davina’: Sikwenda msibani kwa sababu na-shoot na nina mambo yangu ya kifamilia ila niliambiwa nisiende.

Steve Nyerere: Mi nilifiwa na mwanangu sikumuona Wema, tunaangalia kwenye kumbukumbu za wasanii wanaofariki dunia Wema hajawahi kuonekana. Mi’ naomba wasanii wapendane kikweli siyo kinafiki.

William Mtitu: Niko shooting wiki nzima ila kama Wema hakuonekana kwenye misiba ya watu hasa kwa Sajuki alikuwa anakosea sana. Pia alikosea kwa kuwakandia wasanii kwenye vyombo vya habari, kama walikosea angekaa nao akawaambia.

Kulwa Kikumba ‘Dude’: Nilikwenda msibani kutoa pole kwa sababu wale ni ndugu zangu lakini nilivyofiwa na mama yangu Wema hakuonekana wala hakunipa pole na huwa haonekani kwenye misiba ya wengine kama ilivyotokea kwa Sajuki ingawa mimi siwezi kulipa kisasi.
 
ZANZIBAR; DIAMOND NDANI
Kutoka visiwani Zanzibar alikozikwa baba Wema Jumatano iliyopita, ripota wetu alimshuhudia mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiungana na wasanii wengine waliokuwa bega kwa bega kumfariji mrembo huyo.

Habari za kina zilidai kwamba kwa kuwa Diamond hakufika kwenye msiba nyumbani kwa akina Wema, Sinza-Mori, Dar ilibidi aungane na mrembo huyo visiwani Zanzibar kwani naye amekuwa akimendewa na kashfa hiyo ya kuhudhuria misiba mikubwa na kupotezea ya watu wa kawaida.

Aidha, wasanii wengine walioamua kwenda msibani bila kujali onyo la kutokwenda ni pamoja na Yobnesh Yusuph ‘Batuli’, Elizerbeth Michael ‘Lulu’, Kajala Masanja, Mahsein Awadhi ‘Dokta Cheni’, Salumu Mchoma


0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog