Saturday, October 19, 2013


Kikosi cha Young Africans kilichoanza katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar
Baada ya kujiandaa kwa takribani wiki moja sasa kwa ajili ya mchezo wa siku ya jumapili dhidi ya watani wa jadi Simba SC, mabingwa watetezi timu ya Young Africans leo wanarejea jijini Dar es salaam wakitokea kisiwani Pemba ambako walikuwa wameweka kambi ya maandalizi ya mchezo huo.
Kikosi cha Young Africans ambacho kinashika nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi kikiwa na pointi 15, alama tatu nyuma ya vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Simba SC kitashuka dimbani siku ya jumapili kwa lengo la kusaka pointi tatu muhimu na kujiweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo.
Young Africans ambayo inanolewa na kocha mholanzi Ernie Brandts imefanya mazoezi ya mwisho leo asubuhi ikiwa ni maandalizi ya mwisho kwa ajili ya mchezo huo na hakuna ripoti ya mchezaji mgonjwa hata mmoja kuelekea kwenye mtanange huo.
"Sisi tumejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo huo, vijana wangu wapo safi kiafya, kifikra na morali ni ya hali ya juu, hivyo tuna kila sababu ya kuendeleza wimbi la ushindi ukizingatia uwezo wa kikosi chetu kwa ujumla hivi sasa" alisema Brandts 
Aidha Brandts alisema anatambua michezo ya watani wa jadi duniani kote huwa ni migumu lakini kwa sasa haoni sababu itakayowazuia kuibuka na ushindi katika mchezo huo japokuwa Simba timu nzuri pia.
Ushindi kwetu siku ya jumapili ni muhimu, ni muhimu kwa sababu tunapigania kutetea tena ubingwa wetu kwa awamu ya pili mfululizo, kikubwa tunawaomba wapenzi, washabiki na wanachama waje kwa wingi kuwashangilia vijana wao watakpokuwa wanapeperusha bendera ya watoto wa jangwnai.
Tayari shirikisho la soka nchini TFF imeshatangaza viingiilio vya mchezo huo ambavyo ni:
VIP A tshs 30,000/=
VIP B ths 20,000/=
VIP C tshs 15,000/=
Orange tshs 10,000/=
Blue tshs 7,000/=
Green tshs 5,000/=
"MUNGU IBARIKI YANGA"  
"DAIMA MBELE NYUMA MWIKO"

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog