MCHEZAJI ghali wa Arsenal, Mesut Ozil ameendelea kulipa Pauni Milioni 43 zilizotolewa kumnunua kutoka Real Madrid baada ya kutoa pasi zote za mabao matatu, The Gunners ikishinda 3-0 Uwanja wa Emirates dhidi ya Stoke City na kupanda kileleni mwa Ligi Kuu ya England.
Aaron Ramsey alifunga bao lake la saba msimu huu dakika ya
tano baada ya akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Ozil, lakini Geoff
Cameron akaisawazishia Stoke dakika ya 26.
Ozil akadhihirisha yeye ni mkali, baada ya mpira wa kona
aliopiga kuunganishwa kimiani kwa kichwa a Mjerumani mwenzake, beki Per
Mertesacker dakika ya 36 kuipa Arsenal bao la kuongoza.
Ozil tena akamtengenezea Bacary Sagna nafasi ya kufunga bao la tatu dakika ya 72.
Huu unakuwa ushindi wa saba mfululizo kwa Arsenal tangu
wafungwe 3-1 nyumbani na Aston Villa katika mchezo wa ufunguzi wa ligi
hiyo.
Kikosi cha Arsenal kilikuwa: Szczesny, Sagna, Mertesacker,
Koscielny, Gibbs, Flamini, Wilshere/Monreal dk73, Ramsey, Gnabry/Ryo
dk73, Ozil/Arteta dk81, Giroud.
Stoke: Begovic, Cameron, Shawcross, Huth, Pieters/Palacios
dk67, Wilson, N’Zonzi, Adam/Ireland dk59, Walters, Arnautovic,
Jones/Pennant dk75.
0 maoni:
Post a Comment