













Alisema wakati walipoanza kuidhamini Taifa Stars mwezi Mei mwaka jana na kuwekeza zaidi ya shilingi bilioni mbili kwa mwaka, kwa muda wa miaka mitano, walikuwa na malengo kadhaa ikiwemo kuinua hadhi ya Timu ya Taifa, kuhakikisha wanaingia kambini kwa muda unaotakiwa, wanalipwa vizuri, wanakula na kulala vizuri na kusafiri vizuri.
“Tumejitahidi kufanya mambo haya kwani wachezaji sasa hivi wana DVD zenye maelezo yao, tumewapa suti mpya na za kisasa na pia tumewapa basi jipya la kisasa. Mambo haya yote pamoja na mambo wanayofundishwa na Mwalimu Kim Poulsen yamesaidia kuleta mabadiliko kwa timu ya Taifa,” alisema.

Alisema kuna mafanikio mazuri ya timu ya taifa ambayo watanzania lazima wayakumbuke kama kuzifunga timu kama Zambia, Cameroon, Morocco na Kenya .
Kwa mujibu wa Meneja huyo walipoanza udhamini Tanzania ilikuwa katika nafasi ya 145 kwa mujibu wa FIFA lakini sasa imesogea hadi 109. “Haya ni mafanikio makubwa kwani tumesogea hatua zaidi ya 40,” alisema.
Alisema safari ya mafanikio katika mpira ni ndefu na inahitaji uvumilivu wa hali ya juu na kuongeza kuwa Kocha Kim Poulsen anafanya kazi nzuri ya kuibua vijana.

“Kocha anahitaji kuungwa mkono na sisi sote kuanzia kwa TFF, sisi wadhamini na watanzania wote. Tunahitaji kuangalia picha kubwa,” alisema na kuongeza,”Nawaomba watanzania tuwe wazalendo wakati huu hii ni timu yetu na tunatakiwa kujivunia. Vyombo vya habari pia viwe mstari wa mbele kuonesha uzalendo.”
Alisema mechi dhidi ya Gambia itakayochezwa mwezi wa 9 ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia ni muhimu hata kama Tanzania haisongi mbele kwani itasaidia katika ngazi za FIFA.


0 maoni:
Post a Comment