Tuesday, December 8, 2015



DROO ya Raundi ya 3 ya Kombe kongwe Duniani, FA CUP, ambalo sasa linaitwa Emirates FA Cup kwa sababu za kiudhamini, itafanyika Leo na kuzihusisha Klabu za Ligi Kuu England na Daraja la Championship ambazo huanzia hapa. Droo ya Leo, ambayo itafanyika huko Sport Wales National Centre Mjini Cardiff, itahusisha Timu 64 na Mechi zake kuchezwa kati ya Ijumaa Januari 8 na Jumatatu Januari 11.
Arsenal ndio Mabingwa Watetezi baada ya kulitwaa Kombe hili kwa mara ya pili mfululizo Mwezi Mei Mwaka huu.
Droo ya Raundi
Timu zilizopo na Namba za Droo:

1 AFC Bournemouth
2 Arsenal
3 Aston Villa
4 Birmingham City
5 Blackburn Rovers
6 Bolton Wanderers
7 Brentford
8 Brighton & Hove Albion
9 Bristol City
10 Burnley
11 Cardiff City
12 Charlton Athletic
13 Chelsea
14 Crystal Palace
15 Derby County
16 Everton
17 Fulham
18 Huddersfield Town
19 Hull City
20 Ipswich Town
21 Leeds United
22 Leicester City
23 Liverpool
24 Manchester City
25 Manchester United
26 Middlesbrough
27 Milton Keynes Dons
28 Newcastle United
29 Norwich City
30 Nottingham Forest
31 Preston North End
32 Queens Park Rangers
33 Reading
34 Rotherham United
35 Sheffield Wednesday
36 Southampton
37 Stoke City
38 Sunderland
39 Swansea City
40 Tottenham Hotspur
41 Watford
42 West Bromwich Albion
43 West Ham United
44 Wolverhampton Wanderers
45 Bradford City
46 Newport County
47 Peterborough United
48 Portsmouth
49 Eastleigh
50 Northampton Town
51 Exeter City
52 Doncaster Rovers
53 Grimsby Town or Shrewsbury Town
54 Yeovil Town
55 Bury
56 Carlisle United
57 Leyton Orient or Scunthorpe United
58 Wycombe Wanderers
59 Colchester United
60 Chesterfield or Walsall
61 Sheffield United
62 Salford City or Hartlepool United
63 Dagenham & Redbridge or Whitehawk
64 Oxford United


Manchester United: Should the club sack Van Gaal to get Guardiola?
 KIKOSI KILICHOKWENDA KUCHEZA NA TIMU YA WOLFSBURG KESHO JUMANNE KWENYE UEFA CHAMPIONS LEAGUE. David De Gea, Sergio Romero; Paddy McNair, Chris Smalling, Guillermo Varela, Cameron Borthwick-Jackson, Daley Blind, Matteo Darmian; Bastian Schweinsteiger, Michael Carrick, Sean Goss, Nick Powell, Ashley Young, Jesse Lingard, Andreas Pereira, Juan Mata; Memphis Depay, Marouane Fellaini, Anthony Martial.

VAN GAAL ABEBA WACHEZAJI 19 KWENDA KUCHEZA NA WOLFSBURG HUKO GERMANY!
MENEJA wa Manchester United Louis van Gaal Leo amesafiri kwenda Germany na Wachezaji 19 kwa ajili ya Mechi yao ya mwisho ya Kundi B la UEFA CHAMPIONS LIGI, UCL, ambayo itaamua kama watasonga Raundi ya Mtoano au watatupwa EUROPA LIGI.


Man United hawawezi kutupwa nje kabisa ya Ulaya kwani matokeo ya aina yeyote ama yatwabakisha UCL au kupelekwa EUROPA LIGI wakimaliza katika Nafasi ya 3 ya Kundi B.

Katika Kikosi hicho cha Wachezaji 19 hayupo Kepteni Wayne Rooney na Kiungo Morgan Schneiderlin ambao ni Majeruhi na wanaungana na Majeruhi wengine Marcos Rojo, Ander Herrera, Phil Jones, Luke Shaw na Antonio Valencia.

UEFA CHAMPIONS LIGI
KUNDI: B:

PSV Eindhoven (Pointi 7) v CSKA Moskva (4)
Wolfsburg (9) v Manchester United (8)
-Wolfsburg watafuzu wakipata Sare na watachukua Nafasi ya Kwanza wakishinda.
-Man United watasonga wakishinda na kuwa Washindi wa Kundi.
-PSV watafuzu wakishinda au wakidroo ikiwa Man United itafungwa
-CSKA watatwaa Nafasi ya 3 wakiifunga PSV.


Miongoni mwa Kikosi hicho wapo Chipukizi kadhaa akiwemo Paddy McNair ambae alitolewa Haftaimu kwenye Droo na West Ham Majuzi na nafasi yake kuchukuliwa na Chipukizi wa Uruguay Guillermo Varela ambae nae yupo safarini.

Chipukizi wengine Kikosini ni Nick Powell, ambae muda mrefu hajajumuika katika Kikosi cha Kwanza na pia wapo Kiungo Sean Goss na Beki Cameron Borthwick-Jackson.

Kikosi kamili: David De Gea, Sergio Romero; Paddy McNair, Chris Smalling, Guillermo Varela, Cameron Borthwick-Jackson, Daley Blind, Matteo Darmian; Bastian Schweinsteiger, Michael Carrick, Sean Goss, Nick Powell, Ashley Young, Jesse Lingard, Andreas Pereira, Juan Mata; Memphis Depay, Marouane Fellaini, Anthony Martial.

Mechi za Mwisho za Makundi
RATIBA
Mechi zote kuanza Saa 4 Dak 45 Usiku

Jumanne Desemba 8
KUNDI A

Paris St Germain v Shakhtar Donetsk
Real Madrid v Malmö FF

KUNDI B
PSV v CSKA
VfL Wolfsburg v Man United

KUNDI C
Benfica v Atletico Madrid
Galatasaray v FC Astana

KUNDI D
Man City v Borussia Mönchengladbach
Sevilla v Juventus
 

Jumatano Desemba 9
KUNDI E

Bayer Leverkusen v Barcelona
Roma v BATE Borislov

KUNDI F
Dinamo Zagreb v Bayern Munich
Olympiakos v Arsenal

KUNDI G
Chelsea v FC Porto
Dynamo Kiev v Maccabi Tel Aviv

KUNDI H
KAA Gent v Zenit Saint Petersburg
Valencia v Lyon
 


Meneja  wa Arsenal Arsene Wenger amethibitisha Santi Cazorla atakuwa nje ya Uwanja kwa muda unaoweza kufika Miezi mitatu baada ya kufanyiwa Operesheni ya Goti lake Ijumaa iliyopita.
Cazorla, Mchezaji wa Kimataifa wa Spain mwenye Miaka 30, aliumia Kipindi cha Pili cha Mechi yao ya Ligi Kuu England waliyotoka Sare 1-1 na Norwich City Jumapili Novemba 29 lakini alicheza hadi mwisho.
Wakati huo haikujulikana kama aliumia vibaya lakini baada ya kwenda kwa Mtaalam huko kwao Spain ikagundulika kuna kamba ngumu ya Musuli ndani ya Goti imekatika na alipaswa kufanyiwa upasuaji.
Wenger ameeleza: “Santi alitaka amalize tatizo lake haraka ili apone mapema na akaamua kupasuliwa mara moja. Yule Mtaalam alisema ni wazi lipo tatizo hilo na akashauri upasuaji. Santi akakubali moja kwa moja bila kutafuta ushauri mwingine wa Kidaktari ili asicheldewe kupona haraka!”

Wenger amesema kupona kwa Cazorla kutachukua Miezi 3 au 4 ili arejee Uwanjani na si Msimu wote.
Majeruhi wengine wa muda mrefu wa Arsenal ni Mikel Arteta, Danny Welbeck, Tomas Rosicky na Francis Coquelin.


BAADA ya Sare nyingine tena ya 0-0 hiyo jana Uwanjani Old Trafford waliyotoka na West Ham na kuporomoka hadi Nafasi ya 4 kwenye Ligi Kuu England, Louis van Gaal amejikuta akishambuliwa vibaya na Mashabiki wa Manchester United kwenye Miatandao ya Kijamii.

Kwenye Mtandao wa Twitter, Mashabiki wa Man United wamedai Van Gaal, Meneja wa Man United, anaivuruga Timu yao na kuiharibu Historia yao.

Hivi karibuni, Man United wamekuwa wakipata shida kufunga Mabao na tangu waichape Everton 3-0 huko Goodison Park hapo Oktoba 17 kwenye Ligi, zikafuata Sare za 1-1 na CSKA Moscow kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI, UCL, Sare 3 za 0-0 na Man City, Middlesbrough, kwenye Capital One Cup ambayo walitolewa kwa Penati 3-1 na Crystal Palace kwenye Ligi.

Baada ya hapo wakazifunga CSKA Moscow 1-0 kwenye UCL, WBA 2-0 kwenye Ligi, Watford 2-1 kwenye Ligi na kuanza Sare nyingine za 0-0 na PSV kwenye UCL, 1-1 na Leicester kwenye Ligi na hii 0-0 na West Ham.
0 comments

Monday, December 7, 2015


Ikiwa ni siku kadhaa tangu Rais wa awamo ya tano Dk.John Magufuli kutoa tamko la hakutakua na sherehe za kitaifa December 9 na badala yake watu watatumia siku hiyo kufanya usafi katika maeneo yao.
Sasa time hii headlines za usafi zimewagusa wasanii na mkuu wa wilaya ya Kinondoni, DC Paul Makonda ambapo tarehe 9 December wataungana kuhakikisha wilaya ya Kinondoni usafi unafanyika kwenye maeneo mbalimbali.
Akiongea na ripota wa millardayo Steve Nyerere alisema..’Kutakuwa na wasanii mbalimbali ambao tutaungana siku ya usafi katika wilaya ya Kinondoni pamoja na mkuu wa wilaya ya Kinondoni, watu wengi wanaamini usafi ni lazima ma hospitali lakini usafi unaanzia nyumbani kwako, masoko na sehemu mbalimbali zinazomzunguka mwanadamu’ – Steve Nyerere
‘Napenda kusema kwamba siku hiyo wasanii pamoja na wananchi tujitokeze kutekeleza kile kilichosemwa na Mh Rais wa awamo ya tano Dk.John Pombe Magufuli tujitokeze kwa wingi  kufanya usafi huu ni mfano wa kuigwa kwenye mataifa haya ya Afrika’>> Steve Nyerere
‘Wapo wasanii kama 180  mimi nikiwa kama kiongozi wao na Mh DC Paul Makonda  tumechagua wasanii mbalimbali wakiwemo wasanii wa Bongo Movie, Bongo Fleva, wanenguaji kwa hiyo tumechagua vitengo vyote vya sanaa kuhakikisha usafi unafanyika katika wilaya ya Kinondoni’>> Steve Nyerere

Ikiwa ni siku kadhaa tangu Rais wa awamo ya tano Dk.John Magufuli kutoa tamko la hakutakua na sherehe za kitaifa December 9 na badala yake watu watatumia siku hiyo kufanya usafi katika maeneo yao.
Sasa time hii headlines za usafi zimewagusa wasanii na mkuu wa wilaya ya Kinondoni, DC Paul Makonda ambapo tarehe 9 December wataungana kuhakikisha wilaya ya Kinondoni usafi unafanyika kwenye maeneo mbalimbali.
Akiongea na ripota wa millardayo Steve Nyerere alisema..’Kutakuwa na wasanii mbalimbali ambao tutaungana siku ya usafi katika wilaya ya Kinondoni pamoja na mkuu wa wilaya ya Kinondoni, watu wengi wanaamini usafi ni lazima ma hospitali lakini usafi unaanzia nyumbani kwako, masoko na sehemu mbalimbali zinazomzunguka mwanadamu’ – Steve Nyerere
‘Napenda kusema kwamba siku hiyo wasanii pamoja na wananchi tujitokeze kutekeleza kile kilichosemwa na Mh Rais wa awamo ya tano Dk.John Pombe Magufuli tujitokeze kwa wingi  kufanya usafi huu ni mfano wa kuigwa kwenye mataifa haya ya Afrika’>> Steve Nyerere
‘Wapo wasanii kama 180  mimi nikiwa kama kiongozi wao na Mh DC Paul Makonda  tumechagua wasanii mbalimbali wakiwemo wasanii wa Bongo Movie, Bongo Fleva, wanenguaji kwa hiyo tumechagua vitengo vyote vya sanaa kuhakikisha usafi unafanyika katika wilaya ya Kinondoni’>> Steve Nyerere

waliotembelea blog