Monday, June 22, 2015



Simba SC imeingia mkataba na kocha Dylar Kerr Raua wa England kuifundisha klabu hiyo kongwe nchini ambayo ilimaliza Ligi ikiwa katika nafasi ya tatu.

Kerr atasaini mkataba wa mwaka mmoja kuinoa Simba mkataba ambao una kipengele cha kuongeza mwaka mwingine kama atafanya vizuri.

Kocha huyo anakuja Simba SC akitokea klabu ya Ligi Kuu ya Vietnam, Hai Phong aliyojiunga nayo Januari mwaka 2014.

Amezaliwa January 14 mwaka 1967 katika kitongoji cha Valletta nchini England

Kerr amewahi kucheza katika ligi kuu ya England hususani vilabu vya Sheffield Wednesday na Leeds United akicheza kama beki wa kushoto.


Kipa wa Chelsea Petr Cech anakaribia kuhamia Arsenal kwa mujibu wa ripoti za kuaminika huko England.
Cech, mwenye Miaka 33, ameshaafikiana maslahi yake binafsi na Arsenal na kilichobaki ni kusawazisha mvutano kati ya Chelsea na Arsenal kuhusu Ada ya Uhamisho huku pande hizo mbili zikikubaliana kuendelea na mazungumzo.
Cech amebakiza Mwaka mmoja katika Mkataba wake na Chelsea na ameruhusiwa rasmi na Mmiliki wa Klabu hiyo, Roman Abramovich, kuhamia Klabu yeyote anayotaka baada ya kusugua Benchi Msimu uliopita akiwa Kipa Namba mbili nyuma ya Thibaut Courtois.

Cech alijiunga na Chelsea Mwaka 2004 akitokea Klabu ya France Rennes na kuidakia Chelsea Mechi 333. Ingawa Cech mwenyewe anapendelea kubakia London na hivyo kujiunga na Arsenal, Meneja wa Chelsea Jose Mourinho hataki hilo na alipendelea Kipa huyo wa Kimataifa kutoka Czech Republic ahamie kwa Mabingwa wa France Paris Saint-Germain.
Lakini Karata ya Trufu ya Mmiliki Roman Abramovich ndiyo imemtoa kapa Jose Mourinho na kumpa mtaji Kipa Mkongwe Petr Cech.

England, wakicheza Mechi yao ya pili ya Fainali za Mashindano ya Mataifa ya Ulaya kwa Vijana chini ya Miaka 21, EURO U-21, Leo wameifunga Sweden 1-0 huko Ander Stadium, Olomouc Nchini Czech Republic. 

Katika Mechi yao ya kwanza ya Kundi B England walifungwa 1-0 na Portugal lakini Leo mkombozi wao alikuwa Jesse Lingard, Chipukizi wa Manchester United, alieingizwa Dakika ya 55 kumbadili Pritchard na kufunga Bao pekee na la ushindi kwa Shuti kali kufuatia Kona.
England watamaliza Mechi yao ya mwisho ya Kundi C kwa kucheza na Italy hapoKikosi cha Timu ya England U21Kikosi kikiomba kabla ya MtanangeHarry Kane akiachia shuti kaliJesse Lingard kwenye mbio kuukimbiza mpira
Jesse Lingard akifunga bao
Kwenye raha za kupata baoWakimpongeza mwenzao



Kipa wa Manchester United David de Gea amewaambia wachezaji wenzake katika kilabu hiyo ya Old Trafford kwamba anataka kuihama kilabu hiyo na kujiunga na Real Madrid.
Kulingana na gazeti la mail online,hatma ya kipa huyo katika klabu ya Manchester United haijulikani huku Madrid ikiwa na hamu ya kumsajili kipa huyo aliyeisaidia manchester United kupanda hadi nafasi ya nne.

Raia huyo wa Uhispania amewaambia wenzake kwamba anataka kurudi katika klabu ya Madrid kabla ya kuanza kwa msimu ujao.


Arsenal itapuuzilia mbali hamu ya Manchester City ya kutaka kumsajili kiungo wake wa kati Jack Wilshere kwa kumpatia mkataba mwengine wa miaka mitano pamoja na kuongeza mshahara wake mara mbili ya anavyopata.
Kulingana na gazeti la the Mirror, Manchester City ambayo ilishindwa kutetea taji lake la ligi msimu uliopita ina hamu ya kuimarisha safu yake ya kati kwa kununua wachezaji wa Uingereza katika uwanja wa Etihad na Wilshere ni miongoni mwa wachezaji inaowalenga pamoja na Raheem Sterling wa Liverpool na Fabian Delph wa Aston Villa.
Lakini the Gunners wako tayari kumzuia Wilshere mwenye umri wa miaka 23 ambaye amekuwa kiungo muhimu cha timu hiyo na taifa lake.

Baada ya kukaa nje kwa miaka miwili na jeraha,Wilshere ameonyesha kwamba yuko imara kwa mara nyengine tena baada ya kuifungia Uingereza mabao 2 dhidi ya Slovenia katika mechi ya kufuzu kwa michuano ya Ulaya.
Iwapo Manchester City itashindwa kumpata Wilshere basi Sterling atakuwa windo lake.
Lakini Arsenal inajua hatari ya kumkosa mchezaji huyo na tayari imeanza mazungumzo ya kumpatia mkataba mpya.
Wilshere bado ana miaka mitatu ya mkataba wake katika uwanja wa Emirates lakini Arsenal iko tayari kuimarisha malipo yake na kufikia pauni 100,000 kwa wiki ili kuhakikisha kuwa anasalia.


Hii Ndio Ratiba ya Bongo Star Search 2015 ... Mwanza, Arusha, Mbeya na Dar es Salaam. ‪#‎JukwaaNiLako‬ ‪#‎KuwaOriginal‬ Save The Date!
 

 Share artwork hii kwenye page yako ukiambatanisha na hashtag hii #JukwaaNiLako
Mwenye LIKES nyingi zaidi atajishindia zawadi mbalimbali kutoka Bongo Star Search. Mshindi atatangazwa siku ya Jumatano. ‪#‎BSS2015‬


Hii ndio ratiba ya Bongo Star Search 2015 ... Mwanza, Arusha, Mbeya na Dar es Salaam. Follow BSS2015 Twitter @BstarSearch | Instagram @BongoStarSearch | Facebook www.fa


Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika kikao chake cha leo pamoja na mambo mengine kilipitia mwenendo wa timu ya Taifa (Taifa Stars) ikiwa ni pamoja na kuhudhuria mchezo kati ya Tanzania na Uganda, kama sehemu ya tathmini ya mwenendo wa timu.
Kamati ya Utendaji kwa kauli moja imeamua yafuatayo;

1. Ajira ya Kocha Mkuu Maart Nooij inasitishwa mara moja kuanzia Juni 21, 2015.
2. Benchi lote la ufundi la Taifa Stars limevunjwa kuanzia Juni 21, 2015.
3. Uongozi wa TFF utatangaza punde benchi jipya la ufundi la timu ya Taifa.

waliotembelea blog