Saturday, September 13, 2014



Aliyekuwa Rais wa Bongo Movie, Steve Nyerere.
Rais wa Bongo Movie, Steve Nyerere ametangaza kujiuzulu cheo hicho kupitia ukurasa wake wa instagram. Amedai kuna mbinu chafu dhidi yake.

MENEJA wa Swansea City Garry Monk ameshinda Tuzo ya Wadhamini Barclays ya Ligi Kuu England na kutajwa ndie Meneja Bora wa Mwezi baada ya kuongoza Timu yake kushinda Mechi zote Tatu za Ligi Kuu England.
Swansea wamefungana kileleni na Chelsea ambao wako juu kwa ubora wa Magoli na Meneja wao Jose Mourinho alikuwemo kwenye kugombea Umeneja Bora wa Agosti.


Diego Costa akiwa amebeba tuzo yake ya Mwezi Agosti
Kwa upande wa Wachezaji Straika wa Chelsea Diego Costa, ambae ameifungia Timu yake Bao katika kila Mechi ya Ligi waliyocheza, ndie amechaguliwa Mchezaji Bora na kumbwaga mwenzake wa Chelsea Cesc Fabregas na Nathan Dyer pamoja na Gylfi Sigurdsson wa Swansea, na Andreas Weimann wa Aston Villa.

Jumamosi Swansea na Chelsea zitakutana USO KWA USO huko Stamford Bridge.

WACHEZAJI WALIOKUWA WANAGOMBEA NAFASI HIYO:
Diego Costa (Chelsea)
Cesc Fabregas (Chelsea)
Nathan Dyer (Swansea)
Gylfi Sigurdsson (Swansea)
Andreas Weimann (Aston Villa)


LOUIS van Gaal amesema Danny Welbeck aliuzwa Arsenal kwasababu hakuwa mzuri sana kwa Manchester United, lakini amekataa kuwa klabu imeharibu sera yake ya soka la vijana.
Majira ya kiangazi, United walitumia paundi milioni 150 katika usajili wa wachezaji wapya, wakiwemo Angel di Maria na Radamel Falcao.
Kitendo hicho kimezua maswali kuwa klabu hiyo imewageuzia mgongo wachezaji vijana waliokulia katika akademi yao, hususani baada ya kumuuza mshambuliaji wa England, Welbeck kwenda klabu ya Arsenal kwa dau la paundi milioni 16.

Lakini katika mkutano na waandishi wa habari wa kuwatambulisha Falcao na Daley Blind jana alhamisi, Van Gaal alidai kuwa United bado itajikita kuwakuza wachezaji vijana.


Wachezaji wapya waliosajiliwa na Arsenal (kutoka kushoto) Mathieu Debuchy, Calum Chambers, David Ospina, Danny Welbeck na Alexis Sanchez katika uwanja wa mazoezi wa London Colney jana alhamisi. 
Van Gaal alieleza sababu za kumuuza Mzaliwa wa Manchester, Welbeck ambaye ameichezea klabu hiyo toka utotoni, akisema kuwa rekodi ya mshambuliaji huyo ya mabao 29 katika mechi 142 haikaribiani na ya Wayne Rooney au Robin van Persie.
"Niliwapa wachezaji wote nafasi ya kunishawishi," alisema Van Gaal. "Unapouliza kuhusu Welbeck, alikuwepo hapa tangu akiwa na miaka 9 na baada ya kwenda kwa mkopo Sunderland, alicheza misimu mitatu United, lakini hajawa na rekodi kama ya Van Persie au Rooney. Ndio maana tulimuacha aende".


Rio Ferdinand will return to former club Manchester United with Queens Park Rangers on Sunday
Kesho jumapili, Rio Ferdinand atarudi katika klabu yake ya zamani, Manchester United akiichezea Queens Park Rangers 

RIO Ferdinand anarudi Manchester United kwa mara ya kwanza kesho jumapili, lakini amelalamika kuwa klabu hiyo aliyoichezea kwa miaka 12 kamwe haikumpa nafasi ya kuaga kabla ya kujiunga na QPR.
Ferdinand aliichezea United mechi 455 na alitoa mchango mkubwa katika mafanikio ya Sir Alex Ferguson, lakini Mkurugenzi msaidizi Ed Woodward alimuambia baada ya mechi ya mwisho dhidi ya Southamptom msimu uliopita kuwa hataongezewa mkataba.
Baada ya kuambiwa hivyo, beki huyo mwenye miaka 35 aliondoka Old Trafford na kujiunga na QPR mwezi julai mwaka huu.
"Nilikuwa na mafanikio makubwa Old Trafford," alisema Ferdinand. "Sijawahi kupata nafasi ya kuaga nilipoondoka. kilikuwa kitendo kibaya, kwahiyo nitapata fursa ya kuwaaga watu wengi walionisapoti na kunisaida"
The defender linked up with Harry Redknapp at Loftus Road in the summer after 12 years at Old Trafford
Beki huyu alijiunga na Harry Redknapp katika dimba la Loftus Road majira ya kiangazi baada ya kutumika kwa miaka 12 Old Trafford
Ferdinand represented Man United with distinction for over a decade, winning six Premier League titles
Ferdinand aliiwakilisha vyema Manchester United  kwa muongo mmoja na alibeba makombe sita ya ligi kuu 

Friday, September 12, 2014


 
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
YANGA SC itakutana na Azam fc katika mchezo mkali wa Ngao ya Jamii kuashiria kupenuliwa kwa pazia la ligi kuu soka Tanzania bara jumapili (septemba 14 mwaka huu) uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam.
Kuelekea katika mchezo huo, mshambuliaji Jeryson Tegete hayuko fiti kucheza kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya nyonga.
Mbali na nyota huyo mzaliwa wa Mwanza, mshambuliaji mwingine wa Yanga, Mbrazil, Andrey Coutinho yupo hatarini kukosa mechi hiyo kutokana na majeruhi ya mguu aliyoyapa jumatano ya wiki hii katika mechi ya kirafiki dhidi ya Polisi Dar es salaam.
Mechi hiyo iliyomalizika kwa suluhu pacha ya bila kufungana ilipigwa uwanja wa Shule ya Sekondari, Loyola, Mabibo jijini Dar es salaam.
Kwa sasa Yanga wameweka kambi katika Hoteli ya Tansoma, iliyopo eneo la Gerezani, Dar es salaam.
Baada ya Coutinho kuumia siku hiyo, leo hii Polisi Dar wamesikitishwa na majeruhi hayo  na kumuombea dua njema ili awe fiti kwa ajili ya mechi ya keshokutwa uwanja wa Taifa.
Kocha na mratibu wa Polisi Dar, Kennedy Mwaisabula ‘Mzazi’ kwa niaba ya klabu hiyo amemtakia afya njema Coutinho akimuombea apone haraka.
“Kama kocha na mratibu wa Polisi Dar,  kwa niaba ya timu yetu tunamtakia afya njema na apone haraka Andrey Coutinho mchezaji wa Yanga,  Raia wa Brazil aliyeumia kwa bahati mbaya mno dhidi ya  mechi yetu siku ya jumatano.” Amesema Mwaisabula dakika chache zilizopita kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii ya facebook.
Coutinho ameonekana kuwateka mashabiki wa Yanga kwa uwezo wake wa kupiga mashuti ya mbali, kumiliki mpira, kupiga mipira ya adhabu ndogo na kupiga pasi za uhakika.
Nyota huyo amemzidia kete, Mbrazil mwenzake, Geilson Santos Santana ‘Jaja’ ambaye mpaka sasa hajakubalika miongoni mwa mashabiki wa Yanga wakidai ni mzito sana anapokuwa uwanjani.


Daniel Sturridge is out for three weeks after getting injured during training on England duty
Daniel Sturridge atakaa nje ya uwanja kwa wiki tatu baada ya kupata majeruhi katika mazoezi ya England

BRENDAN Rodgers ameponda matibabu wanayotoa England kwa mshambuliaji wake Daniel Sturridge baada ya kupata majeruhi ya mguu.
Sturridge aliumia ijumaa iliyopita, saa 48 baada ya kucheza dakika 89 katika ushindi wa England wa bao 1-0 dhidi ya Norway katika mechi ya kimataifa ya kirafiki.
Nyota huyu alikosa mechi ya kuwania kufuzu Euro 2016 dhidi ya Uswizi ambapo England ilishinda mabao 2-0 na sasa yuko nje ya uwanja kwa wiki tatu.
Rodgers amechukia sana kwasababu mshambuliaji wake hakupewa muda mzuri wa kupumzika.
"Tumekatishwa tamaa sana kwasababu tunadhani majeruhi yake ingetibiwa haraka," Bosi wa Anfield alisema.

Daniel Sturridge's thigh strain in camp with the national team could have been avoided, says Brendan Rodgers+5
Daniel Sturridge amemtia hasara kocha wake Brendan Rodgers
Daniel Sturridge shows his skills in training for England against Phil Jones just before going down injured
Daniel Sturridge akionesha ufundi wake katika mazoezi ya England dhidi ya Phil Jones kabla ya kuumia


Oscar Pistorius has been found GUILTY of the manslaughter of girlfriend Reeva Steenkamp
Oscar Pistorius amekutwa na hatia ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp

MWANARIADHA  Oscar Pistorius anakabiliwa na kifungo gerezani baada ya kukutwa na hatia ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp.
Jaji wa mahakamu kuu ya Afrika kusini, Thokozile Masipa mapema laisema siku ya wapendanao 'Valentine Day' mwaka jana, Pistorius alimpiga risasa mpenzi wake huyo.
Mara zote Pistorius amekuwa akikiri kuhusika na kifo chake nyumbani kwake mjini Pretpria, lakini alisema hakukusudia kumpiga risasi mpenzi wake na  alimpiga risasi nne kwa bastola yake.
Oscar Pistorius arriving in the dock as he awaited the second day of his verdict
Oscar Pistorius akiwasili mahamani siku ya pili leo kujibu mashitaka yake 

Judge Thokozile Masipa declaring that Pistorius was found not guilty for premeditated murder on Thursday+11
Jaji Thokozile Masipa akitangaza kuwa Pistorius hajakutwa na hatia ya kuuza kwa kukusudia jana alhamisi.

Mwanariadha huyo alikuwa anakabiliwa na kesi ya kuua kwa kukusudia, lakini ushindi juu ya hilo haukujitosheleza.
Kwa mara ya pili leo, Pistorius  alisimama kizimbani kujibu shitaka lake, lakini hakuonekana kuwa na hisia zozote.
Jaji Masipa aliiambia mahakama: " Kwa kuzingatia ushahidi wote uliowasilishwa katika mahakama: Kosa la kwanza, muuaji hajakutwa na hatia ya kuua kwa kukusudia na anaachiwa huru kwa hilo".
"Badala yake amekutwa na hatia ya kuua"

waliotembelea blog