Thursday, July 17, 2014


Greet: Van Gaal (centre) meets assistant manager Ryan Giggs (left) and executive vice-chairman Ed Woodward
Salamu: Van Gaal (katikati) amekutana na msaidizi wake  Ryan Giggs (kushoto) na makamu mwenyekiti Ed Woodward.

Imechapishwa Julai 16, 2014, saa 2:14 usiku

KOCHA wa Manchester United, Louis van Gaal amewasili katika uwanja wa mazoezi wa Carrington leo jumatano kuanza kazi yake mpya.
Mholanzi huyo alipigwa picha akiwa geti kubwa, lakini baadaye klabu iliposti picha katika mtandao wake wa Twita akiwa na msaidizi wake Ryan Giggs na makamu mwenyekiti wa klabu hiyo,  Ed Woodward.
Van Gaal alitaka kuonana na wachezaji wake baada ya kombe la dunia pamoja na viongozi wa klabu hiyo.
Underway: The Dutchman has returned from Brazil after leading Holland to a third-place finish
Van Gaal amerudi baada ya kuiongoza Uholanzi kushika nafasi ya tatu ya kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil. 
Discussions: Giggs, Van Gaal and Clive Woodward have work to do to return United regular success
Majadiliano: Giggs, Van Gaal na Clive Woodward wana kibarua kikubwa cha kuirudisha United katika hadhi yake.

Van Gaal ametua kazini siku nne tu tangu aiongoze Uholanzi kushika nafasi ya tatu na kwa maana hiyo amejinyima mapumziko.
Kocha huyo mwenye miaka 62, ni kocha wa kwanza kuiongoza Man United kutoka nje ya British,na hatakuwa na muda wa kupoteza katika harakati zake za kuijengga United.
Kesho alhamisi, atatangazwa rasmi katika mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari kabla ya kuanza safari ya kwenda nchini Marekani kuweka kambi ya maandilizi ya kabla ya msimu.
United itacheza mechi dhidi ya Los Angeles Galaxy, Roma, Inter Milan na  Real Madrid, wakati mechi ya kwanza ya Van Gaal katika dimba la Old Trafford itakuwa ya kirafiki dhidi ya Valencia  Agosti 12 mwaka huu.
Siku nne baadaye United wataanza ligi kuu kwa mchezo wa nyumbani dhidi ya Swansea.
Pairing: United will embark on a US tour in the coming days, and Giggs is happy with training so far
Watu wa kazi: Giggs (kushoto) na Van Gaal watafanya kazi pamoja kufuta majanga ya David Moyes msimu uliopita.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog