Saturday, March 8, 2014


Manchester United wanapata bao kupitia kwa Phil Jones bao la kichwa baada ya Robin Van Persie kuachia shuti kali la frii kiki, Katika dakika ya 34. Phil Jones likiwa ni bao lake la tatu kwa msimu huu. Kipindi cha kwanza Man United wanaenda mapumziko wakiwa mbele ya bao 1-0 dhidi ya wenyeji West Brom. Kipindi cha pili dakika ya 63 United wanafanya mabadiliko Robin van Persie anatoka na nafasi yake inachukuliwa na Danny Welbeck. Kipindi cha pili United wanaongeza bidii na kasi na hatimae dakika ya 65 Wayne Rooney anaipachikia bao la pili na kufanya 2-0 bao la kichwa baada ya mpira kupigwa kama kona na Rafael na Rooney kujitwisha mpira huo kiurahisi mpaka langoni mwa timu ya West Brom Albion. Dakika za mwishoni dakika ya 82 Mchezaji wa United aliyetokea benchi na kuchukua nafasi ya Van Persie Danny Welbeck akaiongezea bao la tatu United kwa kufanya 3-0 baada ya kutanguliziwa pasi safi na Wayne Rooney.
Kocha wa Man United David Moyes akiingia uwanjani Hawthorns.
Mashetani wekundu wakipongezana 
Kushinda ni raha!! David MoyesRooney akichuana na mchezaji wa West Brom Gareth
Januzaji akifanya mambo yake...Wayne Rooney akifunga bapo la kichwa kipindi cha pili...
VIKOSI:
West Brom: West Brom: Foster; Reid, McAuley, Olsson, Ridgewell; Yacob, Mulumbu; Amalfitano, Gera, Brunt, Anichebe
Substitutes: Morrison, Myhill, Vydra, Dawson, Sessegnon, Berahino, Koulossa
Manchester United: De Gea; Rafael, Jones, Smalling, Evra; Carrick, Fellaini; Mata, Rooney, Januzaj; van Persie
Substitutes: Giggs, Lindegaard, Vidic, Young, Welbeck, Fletcher, Kagawa


Nightmare: Torres has struggled to make an impact since £50m switch from Liverpool
Klabu ya Inter Milan imetoa ofa ya paundi mil 20 kwa Chelsea ili kumsajili mshambuliaji wake mkongwe Fernando Torres. Milan wamefikia uamuzi huu baada ya maneno ya Mourinho aliyoyatoa wiki mbili zilizopita kuwa anahitaji kusajili mshambuliaji mpya kutokana na ubutu wa washambualiaji alionao. Kutokana na kauli hii ya Mourinho mshambualiji huyu amekuwa hana raha ikizingatiwa kuwa Eto'o ndiye anapewa nafasi zaidi kwenye mechi nyingi kubwa. Uwezekano wa mchezaji huyu kwenda Inter Milan msimu ujao ni mkubwa kutokana na mipango mikubwa ya klabu hii kutaka kujiimarisha na kurudisha jina lake. Inter Milan tayari imeshamsajili Nemanja Vidic na itaendelea kutafuta wachezaji wengine wenye majina.


Hair today, gone tomorrow: Willian prepares for Chelsea's clash against Spurs with a haircut
Willian akiwa salon 

All smiles: Willian shares a joke with Cesar Azpilicueta (left) in Chelsea's training session at Stamford Bridge



Driven to succeed: Rio Ferdinand arrives at training as United look to turn their season around
 Rio Ferdinand

Motoring: Robin van Persie will hope to get back in the goals
Robin van Persie

All white on the night: Fringe players Shinji Kagawa (left) and Alexander Buttner drive in
Shinji Kagawa na Alexander Buttner

Miles on the clock: Veteran Ryan Giggs will be hurting at how United's season has gone
Ryan Giggs

Good engine: Wayne Rooney looks on as he arrives at Carrington
 Wayne Rooney

Get back on the right road: Michael Carrick will hope his and United's form recovers
Michael Carrick


Wang’amuzi vipaji 28 wanakutana Lushoto mkoani Tanga kwa siku saba katika mpango maalumu wa maboresho ya Taifa Stars ambapo watatoka na orodha ya mwisho ya wachezaji waliopatikana katika mechi za maboresho hayo zilizochezwa nchi nzima.

Katika kikao hicho, wang’amuzi hao watapitia majina ya wachezaji walioteuliwa ikiwemo kuwaangalia tena kwenye video kwa vile mechi zote zilirekodiwa. Wachezaji watakaoteuliwa katika mpango huo baadaye wataingia kambini mkoani Mbeya.

Wang’amuzi vipaji ambao wanaoondoka Machi 9 mwaka huu kwenda Lushoto ni Abdul Mingange, Boniface Pawasa, Charles Mkwassa, Dan Korosso, Dk. Mshindo Msolla, Edward Hiza, Elly Mzozo, Hafidh Badru, Hamimu Mawazo, John Simkoko, Jonas Tiboroha, Juma Mgunda na Juma Mwambusi.

Kanali mstaafu Idd Kipingu, Kenny Mwaisabula, Madaraka Bendera, Madaraka Selemani, Mbarouk Nyenga, Mohamed Ally, Mussa Kissoky, Nicholas Mihayo, Peter Mhina, Salum Mayanga, Salvatory Edward, Sebastian Nkoma, Sekilojo Chambua, Selemani Jabir na Shabani Ramadhan.

Wengine ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi, Kidao Wilfred, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Vijana, Ayoub Nyenzi, Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi, Salum Madadi na Mshauri wa Rais (Ufundi), Pelegrinius Rutayuga.


Rank
Teams
PlayedWinsDrawLostGDGoal scorePoints
1Azam FC181170233540
2Yanga SC171151294138
3Mbeya City2099282436
4Simba SC20983173835
5Kagera Sugar2078521829
6Coastal Union19510451425
7Ruvu Shooting19676-52125
8Mtibwa Sugar1967602325
9JKT Ruvu207112-141622
10Prisons FC17386-31517
11Mgambo Shooting194510-171117
12JKT Oljoro20299-151415
13Ashanti UTD193511-191514
14Rhino Rangers192710-111213


Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeipiga faini ya jumla ya sh. milioni moja klabu ya Simba kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo vitendo vinavyoashiria ushirikina uwanjani. Simba ilifanya vitendo hivyo katika mechi yake dhidi ya Mbeya City ambapo imepigwa faini ya sh. 500,000. Pia imepigwa faini nyingine ya sh. 500,000 kwa makocha wake Loga, Selemani Matola na Idd Pazi kuingia uwanjani na kumzonga mwamuzi kwenye mechi hiyo. Naye mshambuliaji wa Simba, Amisi Tambwe amepigwa faini ya sh. 500,000 kwa kushangilia bao alilofunga kwenye mechi hiyo kwa kuonesha ishara ya matusi kwa kidole.

Mbeya City imepigwa faini ya sh. 300,000 kwa washabiki wake kuingia uwanjani kwenye mechi dhidi ya Kagera Sugar iliyochezwa mjini Bukoba. Klabu za Yanga na Coastal Union zimepigwa faini ya sh. 500,000 kila moja kwa washabiki wao kurusha chupa za maji uwanjani wakati timu hizo zilipopambana jijini Tanga.

Kiungo wa Mtibwa Sugar, Shabani Nditi amepigwa faini ya sh. 500,000 kwa kumpiga mchezaji wa Simba, wakati Salvatory Ntebe pia wa Mtibwa Sugar amepigwa faini ya sh. 500,000 kwa kumtukana refa kwenye mechi dhidi ya Mbeya City.

Pia mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Musa Mgosi amepigwa faini ya sh. 500,000 kwa kosa la kupiga uwanjani kwenye mechi dhidi ya Ashanti United ambapo vilevile atakosa mechi tatu za ligi. Coastal Union imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa washabiki wake kumrushia chupa za maji kipa wa Mbeya City.

Nayo JKT Ruvu imepigwa faini ya sh. 300,000 kwa kuchelewa kufika uwanjani kwenye mechi dhidi ya Simba iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Vilevile wamiliki wa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga wameandikiwa barua ya kufanya marekebisho ya vyumba vya wachezaji, kwa vile havina hewa ya kutosha.

Kwa upande wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) klabu zilizopigwa faini kutokana na makosa mbalimbali ni Friends Rangers (sh. 200,000), Lipuli (sh. 200,000), Majimaji (sh. 400,000), Polisi Morogoro (sh. 400,000) na Transit Camp (sh. 200,000).

Kocha Msaidizi wa Polisi Morogoro, John Tamba atapelekwa kwenye Kamati ya Maadili kutokana na vitendo visivyo vya kimaadili katika mechi dhidi ya Burkina Faso.

Kiongozi wa Lipuli, Hamis Kiemba na wachezaji Boniface Sawaka, George Enock na Green Paul watapelekwa katika Kamati ya Nidhamu kutokana na utovu wa nidhamu waliofanya kwenye mechi dhidi ya Kimondo.

Naye mchezaji Sangalau Nyamoka wa JKT Kanembwa aliyelalamikiwa uhalali wake na Polisi Tabora suala lake linapelekwa Kamati ya Nidhamu.


montage barcelone Chelseas David Luiz and Spurs Jan Vertonghen on Barcelona list to replace Carles Puyol [Mundo Deportivo]
Jumla ya wachezaji watatu wametajwa kwenye orodha ya wachezaji ambao wapo kwenye rada ya Barcelona kusajiliwa mwishoni mwa msimu. Wachezaji hao ni David Luiz (chelsea), Jan Vertonghen (spurs) na Mats Hummels (Dortmund). Kati ya wachezaji hawa mmoja ndiye atakayeweza kusajiliwa na Barcelona ili kuziba pengo la Carles Puyol ambaye ameshatangaza kuondoka Barca kutokana na kuwa majeruhi muda mrefu. Mwishoni mwa mwaka jana Barcelona ilikuwa na nia ya kumsajili Luiz, lakini Mourinho aliweka ngumu hivyo usajili huu ulishindikana. Jambo hili linategemewa kutokea tena mwishoni mwa msimu huu kwani Mourinho na Barcelona ni maadui wa damu. Kutokana na hali hii, Barcelona wana nafasi kubwa kuwasajili Vertonghen na Hummels kuliko Luiz.

waliotembelea blog