Wednesday, August 6, 2014



Mmoja wa washiriki wanaounda kikundi cha Street Dance cha Mbagala jijini Dar es salaam, akionyesha umahiri wake wa kudansi wakati wa shindano la robo fainali la Dance 100 lililodhaminiwa na Vodacom Tanzania na kufanyika katika Viwanja vya TCC Sigara Chang’ombe hapo jana.Shindano hilo lilishirikisha makundi 15 kutoka wilaya ya Temeke ,Makundi matano yalichagulia kuingia katika Fainali za shindano hilo ambapo mshindi atajinyakulia kitita cha shilingi Milioni 5.


Kikundi cha Street Dance cha Mbagara jijini Dar es salaam, wakionyesha umahiri wao wa kudansi wakati wa shindano la robo fainali la Dance 100 lililodhaminiwa na Vodacom Tanzania na kufanyika katika Viwanja vya TCC Sigara Chang’ombe hapo jana.Shindano hilo lilishirikisha makundi 15 kutoka wilaya ya Temeke ,Makundi matano yalichagulia kuingia katika Fainali za shindano hilo ambapo mshindi atajinyakulia kitita cha shilingi Milioni 5.

Wachezaji wa kundi la Manuary kutoka Majohe Pugu jijini Dar es salaam, wakicheza wakati wa shindano la robo fainali la Dance 100 lililodhaminiwa na Vodacom Tanzania na kufanyika katika Viwanja vya TCC Sigara Chang’ombe hapo jana.Shindano hilo lilishirikisha makundi 15 kutoka wilaya ya Temeke ,Makundi matano yalichagulia kuingia katika Fainali za shindano hilo ambapo mshindi atajinyakulia kitita cha shilingi Milioni 5.

Vijana wanaounda Kikundi cha G.O.P cha Keko jijini Dar es salaam, wakitoa burudani kali wakati wa shindano la robo fainali la Dance 100 lililodhaminiwa na Vodacom Tanzania na kufanyika katika Viwanja vya TCC Sigara Chang’ombe hapo jana.Shindano hilo lilishirikisha makundi 15 kutoka wilaya ya Temeke ,Makundi matano yalichagulia kuingia katika Fainali za shindano hilo ambapo mshindi atajinyakulia kitita cha shilingi Milioni 5.

Kundi la Butterfly kutoka Keko jijini Dar es salaam, wakitoa burudani kali wakati wa shindano la robo fainali la Dance 100 lililofanyika katika Viwanja vya TCC Sigara Chang’ombe na kudhamiwa na Vodacom Tanzania.Shindano hilo lilishirikisha makundi 15 kutoka katika wilaya ya Temeke ambapo mshindi wa shindano hilo atajinyakulia kitita cha shilingi Milioni tano.


Vijana wanaounda Kundi la Young Dance la Temeke Mikoroshoni jijini Dar es Salaam wakitoa burudani wakati war obo fainali ya shindano la Dance 100 lililodhaminiwa na Vodacom Tanzania na kufanyika katika Viwanja vya TCC Sigara Chang’ombe hapo jana.Shindano hilo lilishirikisha makundi 15 kutoka wilaya ya Temeke ,Makundi matano yalichagulia kuingia katika Fainali za shindano hilo ambapo mshindi atajinyakulia kitita cha shilingi Milioni 5.


Kikundi cha Wazawa kutoka Mbagala jijini wakitoa burudani wakati wa robo fainali ya shindano la Dance 100 liliodhaminiwa na Vodacom Tanzania na kufanyika katika Viwanja vya TCC Sigara Chang’ombe hapo jana.Shindano hilo lilishirikisha makundi 15 kutoka wilaya ya Temeke ,Makundi matano yalichagulia kuingia katika Fainali za shindano hilo ambapo mshindi atajinyakulia kitita cha shilingi Milioni 5.

Kikuindi cha Swaga Don cha Temeke jijini Dar es Salaam wakifanya mambo yao wakati wa robo fainali ya shindano la Dance 100 liliodhaminiwa na Vodacom Tanzania na kufanyika katika Viwanja vya TCC Sigara Chang’ombe hapo jana.Shindano hilo lilishirikisha makundi 15 kutoka wilaya ya Temeke ,Makundi matano yalichagulia kuingia katika Fainali za shindano hilo ambapo mshindi atajinyakulia kitita cha shilingi Milioni 5.

Kikuindi cha Butterfly cha Temeke jijini Dar es Salaam wakifanya vitu vyao wakati wa robo fainali ya shindano la Dance 100 liliodhaminiwa na Vodacom Tanzania na kufanyika katika Viwanja vya TCC Sigara Chang’ombe hapo jana.Shindano hilo lilishirikisha makundi 15 kutoka wilaya ya Temeke ,Makundi matano yalichagulia kuingia katika Fainali za shindano hilo ambapo mshindi atajinyakulia kitita cha shilingi Milioni 5.


Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa albamu ya muziki wa Injili ,Waziri Mkuu mstaafu.Mh.Frederick Sumaye akionesha albamu ya mwanamuziki nyota wa muziki wa injili hapa nchini,Rose Muhando,iliyoitwa Shikilia Pindo la yesu,mara baada ya kuizindua rasmi mbele ya maelfu ya washabiki na wapenzi wa nyimbo hizo za kiroho ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar jana.

Waziri Mkuu mstaafu.Mh.Frederick Sumaye akifungua kasha lenye CD, wakati akizundua rasmi albamu ya mwanamuziki nyota wa muziki wa injili hapa nchini,Rose Muhando,iliyoitwa Shikilia Pindo la yesu,uzinduzi huo umefanyika jana ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee na kuhudhuriwa na maelfu ya watu mbalimbali.Pichani kati ni Mkurugenzi wa Msama Promotions Ltd,Bwa.Alex Msama sambamba na Mwimbaji nyota wa Injili,Rose Muhando wakishuhudia tukio hilo.

Uzinduzi huo ulioandaliwa na kampuni ya Msama Promotions,ulionekana kufana kwa kwa kiasi kikubwa,huku waimbaji balimbali wakiwa wameshiriki onesho hilo,lililokonga washabiki na wapenzi wa muziki huo kwa kiasi kikubwa.


Waziri Mkuu mstaafu.Mh.Frederick Sumaye akisalimiana na mwanamuziki nyota wa muziki wa injili hapa nchini,Rose Muhando,iliyoitwa Shikilia Pindo la yesu,uzinduzi huo umefanyika jana ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee na kuhudhuriwa na maelfu ya watu mbalimbali.

Baadhi ya Wadau wa Muziki wa Injili wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye uzinduzi huo uliofana kwa kiasi kikubwa.

Sehemu ya umati ya watu waliofika kwenye uzinduzi huo

Mwimbaji wa nyimbo za Injili,Rose Muhanda akiwa na skwadi lake jukwaani wakiimba mbele ya umati mkubwa wa watu (hawapo pichani),wakati wa uzinduzi wa albamu yake mpya,uliofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee hapo jana,ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu Mstaafu,Mh Frederick Sumaye.

Rose Muhando akiimba kwa hisia

Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria uzinduzi huo

Mwimbaji wa nyimbo za Kiroho,Upendo Kilahilo,akiimba jukwaani.

Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka nchini Kenya,Sara K akiimba


Waziri Mkuu Mstaafu,Mh Frederick Sumaye na wadau wengine wakishuhudia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo wakati wa uzinduzi wa albamu mpya ya Rose Muhando iliyojulikana kwa jina la Shikilia Pindo la Yesu.


Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria onesho hilo.

Washabi na wapenzi wa muziki wa injili wakiendelea kushuhudia yaliyokuwa yakijiri kwenye uzinduzi wa albamu ya Rose Muhando.

Palikuwa hapatoshi jukwaani

Mwimbaji John Lissu akiimba sambamba na skwadi lake

Mwenye kuguswa alijikuta akisimama na kuimba

Mwimbaji mahiri wa nyimbo za Injili kutoka nchini Zambia Ephraim Sekelet akiimba mbele washabi na wapenzi wa muziki huo,waliokuwa wamefurika ukumbini humo.

Rose Muhando akiimba sambamba washabiki wake jukwaani


Future doubt:  Arturo Vidal's move to Manchester United and Juventus could still go ahead
Hatima yake shakani: Bado dili la Man United kuendelea kumsajili Arturo Vidal linaendelea.



UHAMISHO wa Arturo Vidal kutoka klabu ya Juventus kwenda Manchester United umeingia shakani kwa sababu nyota huyo wa Chile hayupo fiti, hii ni kwa mujibu wa kocha wa timu ya taifa ya Chile.
Jorge Sampaoli, alikaririwa huko El Mercurio, akisema bosi wa Man United, Louis Van Gaal anaogopa kutumia paundi milioni 47 kumsajili kwasababu kiungo huyo ana matatizo ya goti.
Vidal kwa muda mrefu amekuwa akiwaniwa na Man United na ripoti zinasema kuwa dili hilo linakaribia kukamilika majira haya ya kiangazi.
Fitness worry: Chile boss Jorge Sampaoli says Louis van Gaal has doubts about the midfielder's knee injury
Hayupo fiti: Bosi wa Chile, Jorge Sampaoli anasema Louis van Gaal anaogopa kumsajili Vidal kwasababu ya majeruhi.

'Najua tatizo kubwa katika uhamisho wa Vidali wa dola za kimarekani milioni 80 (paundi milioni 47) kutoka Juventus kwenda Man United, ni Louis van Gaal kuwa na wasiwasi wa kuimarika kwa goti la Vidal,' Sampaoli aliliambia gazeti la Chile.
Vidal alifanyiwa upasuaji wa goti mwezi mei mwaka huu na aliharakishwa kupata matibabu ili kucheza fainali za kombe la dunia majira ya kiangazi mwaka huu nchini Brazil.




SIMBA SC imefanya mkutano mkuu wa kawaida wa wanachama Agosti 3 mwaka huu katika ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi, Osterbay, jijini Dar es salaam ambapo Agenda 13 zilijadiliwa.
Moja ya Agenda muhimu katika mkutano huo ilikuwa ile ya wanachama 72 waliosimamishwa uanachama akiwemo Michael Richard Wambura na mabadiliko ya katiba.
Kabla ya kufanya uchaguzi mkuu wa Simba juni 29 mwaka huu uliomuingiza madarakani Rais Evans Elieza Aveva, klabu hiyo ilifanya mabadiliko ya katiba yake.
Katika mabadiliko hayo kiliwekwa kipengele cha kumruhusu mtu aliyewahi kufungwa huko nyuma kupata nafasi ya kugombea. Watu wengi yawezekana hawafahamu siri iliyofichika katika mabadiliko  ya kipengele hiki.
Baadhi ya wanachama walioona umuhimu wa Zacharia Hans Poppe ambaye aliwahi kufungwa huko nyuma kwa makosa ya uhaini, waliweka kipengele kwamba mtu aliyefungwa agombee kwenye katiba ya Simba.
katika mkutano mkuu wa mabadiliko ya katiba, wanachama wakapitisha kipengele hicho, lakini ilipofika TFF kule, kile kipengele kikaminywa na hakikupitishwa.
Kwa utaratibu, Katiba inatakiwa TFF waipitishe, lakini ilipoenda kule wakabana kipengele hicho na hii ni kwasababu TFF kuna viongozi wa Simba ambao hawakutaka Hans Poppe apate nafasi ya kugombea.
Baadhi ya watu waliokuwa na nia ya kugombea nafasi za uongozi wa juu, hawakupendezewa na kipengele hicho kuwekwa ambacho kilikuwa kinamruhusu mwenyekiti wa kamati ya usajili wa klabu hiyo, Keptein wa zamani wa Jeshi la wananchi Tanzania, (JWTZ), Zacharia Hans Poppe kugombea.
Mkutano mkuu wa mabadiliko ya katiba ya Simba ulipitisha kipengele cha kuruhusu mtu aliyefungwa huko nyuma kugombea, lakini TFF waligoma kukupitsiaha

Hans Poppe ni mtu anayestahili kuwa kiongozi wa Simba kwasababu ana sifa zote. Ni mwanachama halisi, anajitolea kwa moyo wote kuisaidia klabu, yaani ana mapenzi ya dhati. Yupo tayari kuisaidia timu bila kunufaika na chochote.
Yeye ni tofauti na wale ambao wanajihusisha na timu ili waweze kufanya biashara zao. Hans Poppe hahitaji kufanya biashara na Simba zaidi ya kujitolea na kuisaidia timu kutokana na mapenzi ya dhati aliyokuwa nayo.
Kilichonikera mimi, ni kitendo cha wanachama hao hao wa Simba na baadhi ya watu ambao ni mahiri kabisa kujifanya wanaipenda Simba, lakini kumbe hawaitakii Simba mema na wapo kwa ajili ya kupata umaarufu au manufaa mengine kwa kutumia fursa ya kuwepo klabuni hapo.
Ule mkutano mkuu wa katiba ulipitisha kipengele cha kumruhusu Hans Poppe aweze kugombea, lakini kuna watu TFF wakaamua kuweka zengwe na kugoma kupitisha.
Zacharia Hans Poppe ana sifa zote za kuwa kiongozi wa Simba sc

Nimesema awali kuwa kule TFF kuna viongozi wa Simba ambao walikuwa na nia ya kugombea Urais, kwahiyo wakabana kupitisha kipengele cha kumruhusu Hans Poppe kwasababu waliona atakuwa ni kikwazo kwao.
Wakaenda mbali zaidi na kuweka kipengele katika katiba ya Simba kuwa hata wale wajumbe watano watakaoteuliwa na Rais, lazima wawe na sifa kama zile za wajumbe waliochaguliwa na wanachama.
 Uchaguzi ukafanyika na Hans Poppe akatolewa. Lakini Hans Poppe huyo huyo pamoja na kufanyiwa hizo hila, alionesha kuwa yeye ni mwanachama halisi na mpenzi wa Simba na alitoa milioni 20 kwa ajili ya kuendesha mkutano  mkuu wa uchaguzi wa Simba.
Ule mkutano mkuu wa Simba usingefanyika kama Hans Poppe asingetoa hela hizo.  Aliyafanya haya wakati tayari alishawekewe mizengwe na angekuwa mtu mwingine, angesusa na kuondoka zake, lakini alisaidia uchaguzi ufanyike.
Unafiki wa viongozi wa mpira wa Tanzania, uongozi uliokuwepo madarakani chini ya mwenyekiti wake, Ismail Aden Rage,  kwenye mkutano ule wa uchaguzi ulisema kwamba umeacha hela kwenye akaunti na hauna madeni, lakini kiuhalisia uongozi huo ulikuwa unadaiwa na Hans Poppe zaidi ya milioni 250 na mpaka sasa hajaidai klabu.
Hizi ni pesa ambazo alikuwa akizitoa kwa ajili ya kusaidia masuala ya usajili kwasababu yeye alikuwa mwenyekiti wa kamati hiyo na zingine ilikuwa ni kwa ajili ya kuendesha shughuli za kila siku za klabu.
Kabla ya uchaguzi, vilitengenezwa vipengele vya kumruhusu Hans Poppe kugombea na katiba ilipofika TFF wakaminya, lakini baada ya malengo yao kufanikiwa kwa kumuwekea vigingi, sasa wanaona aibu na kuitisha mkutano mkuu wa wanachama ili kufanya mabadiliko ya katiba, ikiwa ni siku chache tu baada ya kuingia madarakani.
Zacharia Hans Poppe (wa kwanza kulia) alikuwepo katika uongozi uliomaliza muda wake chini ya mwenyekiti Ismail Aden Rage.

Huo mkutano ulikuwa ni kubadili kipengele kimoja tu ili kuweza kumsafisha Hans Poppe aweze kuwa na sifa ya kuteuliwa kwenye kamati ya utendaji.
Kwahiyo kile kipengele kilichowekwa kwa ajili ya kumruhusu na kikaminywa,  ndio kile kile kikasababisha uitishwe mkutano mkuu ili kirekebishwe na kumpa Rais mamlaka ya kuteua wajumbe wa kamati ya utendaji pasipo kuzingatia sifa za hapo awali.
Kipengele kinabadilishwa na wale wanaohitaji ‘mahela’ ya Hans Poppe ili awasajilie wachezaji, lakini anarudije wakati amewekewa kipengele cha kumzuia?
Hapo ndipo mkutano wa wanachama uliitishwa ili kutegua ule mtego tena. Wanahangaika kutegua mtego ili Hans Poppe awe huru na kuweza kuingia kamati ya utendaji.
Simba hao hao wakiwa kule TFF walimuweka kwenye mtego wa Panya, na sasa wanahangaika kuutegua ili aweze kutoka. Simba walidhani Hans Poppe ni panya, lakini wamekuja kugundua sio panya.
Zacharia Hans Poppe akiwa ofisini kwake

Mimi binafsi namkubali Hans Poppe, bila mizengwe, chuki wala fitina, na naamini ana sifa za kuwa kiongozi wa Simba
ni aina ya watu wanaostahili kuiongoza Simba, lakini kuna watu wengine ambao hawahitaji kuona maslahi ya Simba na wanamuona yeye kama kikwazo.
Wanahangaika kumrejesha, kwahiyo wanang`ata huku na kupuliza. Huu ni unafiki usiotakiwa kuwepo na wakubali kuwa Hans Poppe anastahili kuwepo Simba na wasiweke mizengwe, wabadili kabisa katiba na kumfanya siku za usoni awe Rais wa timu kwasababu ana uwezo.
Isije ikafika muda wa uchaguzi, wakaitisha tena mkutano wa kufanya mabadiliko ya katiba ili Hans Poppe asigombee.
Halafu kuna kipengele kingine cha nafasi ya wazee wa klabu. Katiba ya Simba inasema, lazima mmoja wa wazee wa klabu aingie katika kamati ya utendaji, lakini wazee wote wa Simba waliopo, yawezekana hawana sifa kama zile za wagombea.
Kwahiyo wanatoa kipengele hicho ili kuruhusu mmoja wa wazee kuingia kwenye kamati ya utendaji.
Ina maana hao wazee wa Simba ambao hawana sifa wamezaliwa wao tu na hakuna nafasi ya kutafuta wazee wengine ambao wana sifa kama za wagombea?
Ina maana wazee wote wanaoipenda Simba hawajamaliza kidato cha nne? Yaani wazee wote duniani ambao wamejitolea kwa ajili ya Simba hawana vyeti vya kidato cha nne?
Au kwanini wasifanye mabadiliko ya katiba kama wanagundua kuwa wazee hawana sifa zile za wagombea ili iwe kwamba, sio lazima kwenye kamati ya utendaji awepo mzee.
Kiukweli hakuna mashiko kwa kipengele hiki cha wazee. Hapa ni kujaribu kuficha ukweli, sababu ya mabadiliko ya katiba itabaki kuwe ile ile ya kutafuta namna ya kumuingiza kwenye mfumo Hans Poppe.
Binafsi bila kumung`unya maneno, Zacharia Hans Poppe ana kila sifa ya kuwa kiongozi ndani ya klabu ya  Simba.
Umefika  muda sasa wa Unafiki, mizengwe, uzandiki kupigwa vita na kukemewa michezoni kama kweli tuna nia ya dhati ya kuendelea kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali.
Moja kati ya sababu kubwa inayokwamisha sola la Tanzania kuendelea ni unafiki na uzandiki uliojaa kwa viongozi wa nchi hii.



FRANK James Lampard, mwenye miaka 36, mpaka sasa amecheza mechi 973 kwa klabu na nchi yake katika maisha ya soka.
Anahitaji mechi 27 tu kufika digiti nne na kitu hicho anaweza kufanya kupitia michuano ya ligi kuu soka nchini England baada ya kujiunga na Manchester City kwa mkopo kutoka klabu ya New York City mwezi huu.
Kiungo huyo mkongwe ataitumikia Man City mpaka mwezi Januari mwakani ambapo ataende NYCFC kujiandaa na michuano ya ligi kuu nchini Marekani.
Atakuwepo kwa michezo 23 ya ligi kuu, mechi sita za ligi ya mabingwa, ataanza kombe la Capital One na FA na mechi ya Ngao ya Hisani itakayopigwa siku ya jumapili.
Lampard ambaye bado hajastaafu soka la kimataifa, ana nafasi kubwa ya kuongeza mechi zake 106 alizocheza kwa timu ya taifa baada ya kurudi ligi kuu.
Lampard ndiye mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi kwa taifa lake. Pia alicheza England B na alicheza mara 19 katika timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 19.
Kiungo huyo alicheza mechi 187 akiwa na Westaham, klabu yake ya kwanza na alicheza mechi 11 akiwa kwa mkopo Swansea kabla ya kwenda kucheza mechi 649 katika miaka 13 aliyocheza Chelsea, na kujiweka katika nafasi ya tatu ya kucheza mechi nyingi klabuni hapo nyuma ya Peter Bonetti na mchezaji anayeshikilia rekodi Ron Harris.
Mchezaji wa mwisho wa England kufikisha mechi 1,000 katika timu ya wakubwa alikuwa kocha msaidizi wa Manchester United, Ryan Giggs ambapo alifikisha idadi hiyo mwaka 2013 kwenye mechi za ligi ya mabingwa dhidi ya Real Madrid.

Kocha wa sasa wa Fleetwood, Graham Alexander, ambaye aliichezea Scunthorpe United, Luton Town, Preston North End na Burnley alifikisha mechi 1,00 mwezi aprili 2011.

waliotembelea blog