Sunday, October 4, 2015


Jose Mourinho akichachamaa!!3-1Mabingwa CHELSEA wakicheza kwao Darajani mbele ya mashabiki 41642, wamefungwa na Southampton bao 3-1. Kipindi cha kwanza kilimalizika 1-1 na kipindi cha pili Sputhampton walifunga bao mbili dakika ya 60 na dakika ya 72. Chelsea bao lao lilifungwa na Willian dakika ya 10 na dakika ya 43 Steven Davi aliisawazishia bao Southampton kwa kufanya 1-1. Sadio Mane dakika ya 60 na lile la Graziano Pellé dakika ya 72 na mtanange kumalizika dakika 90 Southampton wakiibuka kidedea kwa bao 3-1 dhidi ya Mabingwa hao.Pelle akifanya mavitu
3-1Shangwe!Jose akishangaa shangaa leo DarajaniBao!Mane akishangilia bao lake Mane akitupia..1-1Asante Willian!! Akipongezwa na wenzake!1-0Willian akishangilia kwa kupetaMbele ya MashabikiFalcao alipojitupa chini kwenye 18 na kupewa kadi ya njano!Aaaah!
VIKOSI:
Chelsea starting XI
: Begovic, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Ramires, Fabregas, Willian, Oscar, Hazard, Falcao
Chelsea subs: Zouma, Baba, Pedro, Remy, Matic, Blackman, Loftus-Cheek
Southampton starting XI: Stekelenburg, Cedric Soares, Fonte, van Dijk, Bertrand, Romeu, Wanyama, Mane, Steven Davis, Tadic, Pelle
Saints subs: Kelvin Davis, Yoshida, Long, Rodriguez, Martina, Ward-Prowse, Juanmi


 Sevilla FC waliofnga bao ni Michael Krohn-Dehli dakika ya 52 na lile la Vicente Iborra dakika ya 58 na kufanya bao kuwa 2-0.
Barcelona  walifungiwa bao lao na Neymar dakika ya 74 kwa mkwaju wa penati na mtanange kumalizika Sevilla wakiwa kidedea kwa bao 2-1 dhidi ya Barcelona.Sevilla wakishangilia bao mbele ya Mashabiki waoIborra alipotupia baoNeymar Suarez akishangaa shangaa baada ya kukosa bao la waziChupuchupu! Suarez afunge bao!


Sergio Agüero Alifunga tena bao mbili haraka dakika ya 49 na 50 na kujifanyikia kupata hat-trick yake kwa kupiga bao tatu na kufanya bao ziwe 3-1. Bao la nne lilifungwa na Kevin De Bruyne dakika ya 53 na tena dakika ya 60 Sergio Agüero alifunga bao la tano na kisha dakika ya 62 Sergio Agüero akafunga la 6 na kufanya matokeo kuwa 6-1.Raha  ya bao!Sergio Agüero dakika ya 42 aliwasawazishia bao Man City na kufanya mtanange kwenda mapumziko zikiwa sare ya bao 1-1, Bao la Newcastle United lilifungwa na Aleksandar Mitrovic mapema dakika ya 18'
Man City wametwaa uongozi wa Ligi Kuu England baada ya Leo kuichapa Newcastle Bao 6-1 Uwanjani Etihad huku Straika wao Sergio Aguero akipiga Bao 5.
City walitanguliwa Bao 1-0 kwa Bao la Dakika ya 18 la Aleksandar Mitrovic lakini Aguero alisawazisha Dakika ya 42 na Mechi kwenda Haftaimu ikiwa 1-1.
Kipindi cha Pili, Aguero aliongeza Bao 4 katika Dakika za 49, 50, 60 na 62 wakati Kevin De Bruyne akifunga katika Dakika ya 53.
Ushindi huu umewapa uongozi wa Ligi City wakiwa na Pointi 18, Pointi 2 mbele ya Man United ambao kesho wako Emirates kucheza na Arsenal.

Aguero alipofunga bao la kwanzaPisha njia!
VIKOSI:
Man City:
Hart, Zabaleta, Otamendi, Mangala, Kolarov, Fernando, Fernandinho, De Bruyne, Silva, Sterling, Aguero.
Subs: Sagna, Caballero, Bony, Jesus Navas, Demichelis, Iheanacho, Garcia.
Newcastle: Krul, Janmaat, Mbemba, Coloccini, Mbabu, Sissoko, Wijnaldum, Anita, Gouffran, Mitrovic, Perez.
Subs: Williamson, Cisse, De Jong, Lascelles, Thauvin, Elliot, Tiote.
Referee: Kevin Friend


Yohan Cabaye alipatia bao la pili na kufanya 2-0 dhidi ya West Brom kwa mkwaju wa penati baada ya  Zaha kuangushwa ndani ya 18.
Ushindi huu umeipandisha Timu hiyo ya Palace juu nafasi ya tatu na wakiwa na pointi 15.
Yannick Bolasie alitupia bao dakika ya 68 kipindi cha pili na kuwapa nguvu ya kuongoza kwa bao 1-0 dhidi ya West Brom Albion.Zaha akiendesha mpiraYohane akipiga penati!Pongezi!

waliotembelea blog