Kikosi cha TP Mazembe
Klabu ya soka ya TP Mazembe ya nchini Congo jana imechezea kipigo cha
bao 1-0 kutoka kwa El Hilal Omdurani ya Sudan katika mchezo wa kwanza
wa hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Afrika.
El Hilal walianza kutibua mipango ya Mazembe katika dakika ya 51
baada ya Salah Al Jizoli kuandika bao la kuongoza kufuatia kumalizia
pasi nzuri ya Bakri Babeker.
Kipigo hicho cha bao 1-0 kimewafanya Mazembe kuanza vibaya michuano
hiyo na sasa watahitaji kufanya vizuri mchezoz unaofuata, huku wakiwa
katika kundi A pamoja na wapinzani wao wakubwa AS Vita.
Washambuliaji wote wawili wa Tanzania wa TPM walicheza, Mbwana
Samatta akianza na Thomas Ulimwengu akitokea benchi dakika ya 66 kwenda
kuchukua nafasi ya Rainford Kalaba.
Samatta na Ulimwengu wanatarajiwa kuondoka asubuhi kuja Dar es Salaam
kujiunga na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwa ajili ya mchezo
wa Jumapili dhidi ya Zimbabwe, kuwania hatua ya makundi ya kuwania
tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani nchini Morocco