Msanii
wa Muziki wa Kizazi kipya, Kala Jeremiah akiongea na waandishi wa
habari ili kuwaelezea onyesho lao la bure wanalotarajia kulifanya Agosti
23, 2015 Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala kuwahamasisha
mashabiki wao kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais,
Wabunge na madiwani wa Oktoba 25, 2015. Pembeni ni Joseph Haule
“Professa J”, Juma Kassim “Sir Nature” pamoja na Msagasumu.
Msanii
wa Muziki wa Kizazi kipya, Joseph Haule “Professa J” akionyesha
msisitizo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya onyesho
lao la bure wanalotarajia kulifanya Agosti 23, 2015 Jumapili kwenye
viwanja vya Zakhem, Mbagala kuwahamasisha mashabiki wao kujitokeza
kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba
25, 2015.
Msanii
wa Muziki wa Kizazi kipya, Juma Kassim “Sir Nature” akionyesha
msisitizo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya onyesho
lao la bure wanalotarajia kulifanya Agosti 23, 2015 Jumapili kwenye
viwanja vya Zakhem, Mbagala kuwahamasisha mashabiki wao kujitokeza
kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba
25.
Tanzania Oyeeeee! Tanzania Oyeeee! ndiyo wasanii hawa walivyokuwa wakitia msisitizo.
Baadhi
ya wasanii watakaowasha moto Agosti 23, 2015 Jumapili kwenye viwanja
vya Zakhem, Mbagala kuwahamasisha mashabiki wao kujitokeza kupiga kura
kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25, 2015.
Mwandishi wa habari wa Times Fm, akifanya mahojiano na Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Joseph Haule “Professa J”.
……………………………………………….
Na Mwandishi Wetu.
Wasanii
nyota wa muziki wa kizazi kipya na baadhi ya nyota wa Bongo Movie
watafanya onyesho la bure Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala
kuwahamasisha mashabiki wao kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu
wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25.
Wasanii
hao wataongozwa na Mbunge wa Mbeya mjini kupitia Chama Cha Demokrasia
na Maendeleo (Chadema), Joseph Mbilinyi “Sugu” na nyota wengine kama
Juma Kassim “Sir Nature”, Joseph Haule “Professa J” na Kara Jeremiah.
Wengine
ni watakaopanda jukwaani siku kuanzia saa 8.00 mchana ni Msaga Sumu,
Baba Haji na waigizaji nyota wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper na Auntie
Ezekiel.
Akizungumza
jijini jana, Professa J alisema kuwa sababu kubwa ya kufanya onyesho
hilo ni kutoa elimu kwa mashabiki wao kuhusiana na zoezi la upigaji kura
kuchagua viongozi bora wan chi hii wataodumu kwa miaka mitano.
Professa
alisema kuwa wanataka kutoa mwamko kwa mashabiki wao kushiriki kwa
wingi katika zoezi hilo ili kutumia demokrasia yao kumchagua kiongozi
wanayemtaka.
“Tumejiandaa
vilivyo kutoa elimu, lengo ni kuwahamasisha mashabiki wetu kufanya kile
wanachokiona kinafaa ili kutimiza malengo yao ya kikatiba,” alisema
Professa J.
Alisema kuwa mbali ya Dar es Salaam, onyesho hilo pia litafanyika katika mikoa mengine mbalimbali.
Akizungumza
katika mkutano huo, Nature aliwaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi ili
kupata elimu hiyo ambayo wasanii wameamua kuitoa.
“Hii
siyo kampeni ya kisiasa, sisi ni wasanii tumeamua kujitolea kufanya
kazi ambayo wasanii wengi duniani wameifanya, lazima tutumie kazi yetu
kutoa elimu kwa mashabiki ili wajue wajibu wao katika mambo mbali mbali
pamoja na uchaguzi mkuu,” alisema Nature.