Thursday, December 10, 2015



Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno anayekipiga katika klabu ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo, usiku wa December 8 katika mchezo dhidi ya Malmoe FF wa kuhitimisha mechi za Makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya alivunja rekodi yake mwenyewe aliyoiweka msimu uliyopita, kabla ya mchezo huo uliyomalizika kwa Real Madrid kuibuka na ushindi wa goli 8-0, Ronaldo alikuwa anashikilia rekodi ya kuongoza kwa kufunga magoli mengi katika mechi za Makundi, kwani alifunga magoli 9 msimu uliyopita.
Usiku wa December 8 aliingia uwanjani akiwa tayari kafunga jumla ya magoli 7 katika mechi 5 zilizopita za hatua ya makundi, hivyo kufunga kwake goli nne katika mchezo dhidi ya Malmoe FF kulimfanya afikishe jumla ya magoli 11 na kuvunja rekodi yake ya msimu uliyopita, rekodi ambayo hakuna mchezaji aliyekuwa kaifikia. Mtu wangu wa nguvu hiyo sio rekodi ya kwanza ya Ronaldo, naomba nikusogezee rekodi 10 kali za Ronaldo.
1- Wakati akicheza Man United Ronaldo alifanikiwa kuvunja rekodi ya mkongwe wa timu hiyo George Best ya ufungaji wa magoli 33 katika msimu wa 1967/1968 na kumfanya Ronaldo kuwa mchezaji wa kwanza wa Ureno kucheza kwa mafanikio Man United.
epa04477463 Real Madrid's Portuguese forward Cristiano Ronaldo gives thumbs up after receiving the Golden Boot award as top scorer in all European soccer leagues of the 2014-2015 season during a ceremony in Madrid, Spain, 05 November 2014. Cristiano also won the Golden Boot award in the 2007/2008 and 2010/2011 seasons. EPA/JUAN CARLOS HIDALGO
2- Ronaldo aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Ligi kubwa za Ulaya kufunga magoli 50 na zaidi katika msimu mmoja. rekodi ambayo aliiweka kwa kufunga magoli katika mashindano matano tofauti.
3- Staa huyo pia anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga magoli 100 ya Ligi katika kipindi kifupia, kitendo ambacho kimemfanya kuwa mchezaji wa kwanza wa Real Madrid kufanya hivyo, Hata hivyo magoli hayo yalimfanya Ronaldo kuwa mchezaji wa kwanza wa Laliga kuzifunga timu zote 19 za Laliga zilizocheza dhidi ya Real Madrid.
4- Ronaldo anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga magoli 17 katika msimu mmoja wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, alifanya hivyo katika msimu wa 2013/2014.
Cristiano-Ronaldo-is-Now-Tenth-Top-Scorer-in-La-Liga-History
5- Ronaldo aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga goli 200 za haraka za Laliga katika jumla ya michezo 178 December 2014. Alifunga hat-trick dhidi ya Celta Vigo na kufikisha jumla ya hat-trick 23 zilizoingia katika rekodi ya Laliga.
6- Ronaldo alifunga jumla ya hat-trick 8 katika msimu mmoja wa 2014/2015 na kuweka rekodo ya kufunga hat-trick nyingi zaidi kuwahi kufungwa katika msimu mmoja wa Ligi.
7- Aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Sporting Lisbon kucheza katika vikosi vya (U-16), (U-17), (U-18), timu B na kikosi cha kwanza cha kwanza cha Sporting Lisbon yote hiyo amecheza katika msimu mmoja.
ronaldoget_2327179b
8- Wakati anacheza Man United Ronaldo aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa tatu wa Ligi Kuu Uingereza kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi mara mbili mfululizo, alifanya hivyo mwaka 2006 kwa kutwaa tuzo hiyo mwezi November na December. Wengine waliowahi kufanya hivyo ni Robbie Fowler mwaka 1996 na Dennis Bergkamp mwaka 1997.
9- Ronaldo ni mchezaji wa pili kutwaa tuzo ya Ballon d’Or mara nyingi, ametwaa mara tatu mwaka 2008, 2013 na 2014, anayeongoza kwa rekodi hiyo ni Lionel Messi aliyetwaa mara nne.
cristiano-ronaldo-ballon-2014
10- Ronaldo ndio mchezaji wa kwanza Ligi Kuu Uingereza kuwahi kutwaa tuzo nne za PFA na FWA kwa msimu mmoja, Ronaldo alifanya hivyo mwaka 2007 akiwa katika klabu ya Man United.



Baada ya mechi za hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kumalizika usiku wa December 9 na kushuhudia vilabu 16 vikitinga hatua ya 16 bora na vilabu vingine 16 vikiaga mashindano hayo, December 10 ilikuwa ni zamu ya kushuhudia mechi za Europa League, miongoni mwa mechi za Europa League zilizochezwa usiku wa December 10 ni mchezo kati ya FC Sion ya Uswiss dhidi ya Liverpool ya Uingereza.
2831
FC Sion ndio walikuwa wenyeji wa Liverpool katika dimba lao la Stade de Tourbillon na kuwakaribisha Liverpool, licha ya kuwa FC Sion walikuwa katika uwanja wao wa nyumbani walionekana kutawaliwa na Liverpool kimchezo kwa  dakika zote 90, hata hivyo mchezo huo ulimalizika kwa sare 0-0.
3206
Hadi dakika 90 zinamalizika klabu ya Liverpool inayonolewa na kocha wa Kijerumani aliyewahi kuifundisha klabu ya Borussia Dortmund ya kwao Ujerumani Jurgen Klopp, walionekana kuutalawa mchezo kwa asilimia 61 na FC Sion ikimiliki mpira kwa asilimia 39 pekee. Liverpool licha ya kuutawala mchezo walishindwa kupata goli hata moja.
2754




Mwanamuziki na mtangazaji wa redio, Roberto Chindaba Banda 'maarufu Roberto Amarula kutoka nchini Zambia (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana , kuhusu onyesho lake atakalolifanya leo katika fukwe za Escape One Mikocheni jijini Dar es Salaam na kesho ukumbi wa Ngalawa Pub mkoani Dodoma katika Tamasha la Instagram Party Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Freconic Ideaz, Fred Ngimba ambao wamemleta msanii huyo hapa nchini kwa kushirikiana na Kampuni ya C&G Solutions na kulia ni Mwanamuzi David Banda 'General Ozzy kutoka Zambia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Freconic Ideaz, Fred Ngimba (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
Meneja Mawasiliano wa Freconic Ideaz, Krantz Mwantepele (kushoto), akizungumza katika mkutano huo ambapo alisema kampuni yao itaendelea kuleta wanamuziki wengine kutoka pande mbalimbali za dunia kama walivyofanya kwa Robarto Amarula.
Mwanamuzi David Banda 'General Ozzy kutoka Zambia (kulia), akizungumza na wanahabari.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mwanamuziki na mtangazaji wa Redio, Roberto Chindaba Banda 'maarufu Roberto Amarula kutoka nchini Zambia, akifanya vitu vyake mbele ya wanahabari.


Mwanamuzi David Banda 'General Ozzy, akiimba mbele ya wanahabari. Mwanamuziki huyu atamsindikiza Roberto Amarula wakati wa shoo yao.
Mwanamuziki, Clinton Nyirongo kutoka Zambia naye atakuwepo kutoa burudani.


MWANAMUZIKI wa Zambia anayetamba na wimbo maarufu wa Amarula, Robert Banda ‘Roberto Amarula’, kesho anatarajia kufanya shoo kubwa na ya aina yake katika Ufukwe wa Escape One uliopo Mikocheni, jijini Dar es Salaam kabla ya kufanya hivyo mjini Dodoma kesho kutwa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo asubuhi, Roberto Amarula, ameahidi kutoa burudanio ya aina yake kwa wakazi wa Dar es Salaam na Dodoma, akiwataka mashabiki wa muziki na burudani kujitokeza kwa wingi kwenye shoo zake hizo.

“Nimefurahia sana kuja Dar es Salaam na ninaahidi kutoa shoo ya aina yake kesho (leo) na Dodoma ili kuwaburudisha Watanzania, lakini pia nitatembelea vituo vya watoto yatima ili kuwafariji na kuwapa nguvu wajione nao ni sehemu ya jamii ya Watanzania na Afrika kwa ujumla,” alisema aliyeambatana na wasanii wenzake wa Zambia, David Banda ‘General Ozzy’ na Clinton Ntirongo ‘Mandela’.


Kwa upande wake, Mkugenzi wa Freconic Ideaz, Fred Ngimba, alisema kuwa shoo ya leo itawahusisha pia wasanii wa Tanzania kama Ben Pol, Roma Mkatoliki, Fred Swag, Msouth na wengine wengi na kwamba onyesho la Dodoma litafanyika kwenye ukumbi wa Ngalawa Pub, ikiwa ni sehemu ya tamasha la Instagram Party. 

Kwa upande wake, Meneja Mawasiliano wa Frecon Ideaz, Krantz Mwantepele, alisema: “Tunafahamu kiu ya Watanzania katika suala zima la burudani ndio maana tumewaletea msanii huyu ambaye kwa sasa ni maarufu mno Afrika na kwingineko tukiahidi kuwaleta wasanii zaidi wakubwa Afrika na hata Marekani ili kukata kiu ya mashabiki wa muziki hapa nchini.

Ziara ya Roberto Amarula ambaye ni mshindi wa tuzo za uandishi bora, mwanamuziki, mtayarishaji muziki na mtangazaji wa redio, iliyoratibiwa kwa pamoja na Freconic Ideaz na C&G Solutions, imedhaminiwa na Millard Ayo, Morena Hotel, Shabiby Bus Service na Clouds FM.


KOMBE LA DUNIA kwa Klabu linaanza huko Japan Alhamisi Desemba 10.
Washiriki wa Mashindano haya ni Barcelona, Mabingwa wa Ulaya, River Plate, Mabingwa wa Marekani ya Kusini, America ambao ni Mabingwa wa Nchi za Marekani ya Kati na Kaskazini na Visiwa vya Carribean, Mabingwa wa Afrika TP Mazembe, Guangzhou Evergrande, Mabingwa wa Asia na Bingwa wa Kanda ya Oceania.
Pia wapo Sanfrecce Hiroshima, Klabu Bingwa ya Japan, inayoshiriki kama Wenyeji wa Mashindano.
Wakati Barcelona wakiwa ndio wanategemewa kutwaa Kombe hili wakijivunia Kikosi chenye Masupasta Lionel Messi wa Argentina, Nahodha wa Brazil Neymar na Straika wa Uruguay Luis Suarez, Tanzania itaikodolea macho TP Mazembe yenye Mastraika Wawili mahiri kutoka Nchi hiyo, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu.
Mwaka 2010, TP Mazembe ilifika Fainali ya michuano hii na kufungwa na Inter Milan.

Klabu ya China, Guangzhou Evergrande, pia itakodolewa macho kwa vile Kocha wao ni Mbrazil Luiz Felipe Scolari ambae aliisaidia kutwaa Ubingwa wa Asia.
Mechi ya ufunguzi ya Alhamisi ni kati ya Wenyeji Sanfrecce Hiroshima ikicheza na Auckland City katika Raundi ya Awali ambapo Mshindi atatinga Robo Fainali kucheza na TP Mazembe, inayoanzia hatua hii na Mechi hii itachezwa Jumapili huko Osaka.
Mshindi wa Robo Fainali hii atatinga Nusu Fainali kucheza na River Plate itakayoanzia hapo.
Katika Robo Fainali nyingine hapo Jumapili America itaivaa Guangzhou Evergrande na Mshindi wake kwenda Nusu Fainali kuikabili Barcelona itakayoanzia hapo.


Willian akishangilia bao lake baada ya kuifunga Timu ya FC Porto ikiwa ni bao la pili Jose Mourinho chini akiendesha mapambano ya kuwakumbusha wachezaji wake Willian alifunga bao la pili kwa shuti kaliDiego Costa akipongezwa na Hazard Diego aliachia shuti kali ambalo lilizaa bao la kujifunga wao wenyewe FC Porto mbele ya Mlinda mlango wao Casillas.


SAFU ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONS LIGI, UCL, imekamilika Jana na Timu za England, Arsenal na Chelsea, zilishinda hapo Jana na kutinga Mtoano.
Timu hizo zinaungana na Chelsea iliyofuzu mapema ikiwa na Mechi 2 mkononi.

Juzi Man United ilitolewa UCL na kutupwa UEFA EUROPA LIGI baada ya kumaliza Nafasi ya 3 kwenye Kundi B.
Man United sasa itacheza Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya Kombe hilo.
Droo za kupanga Mechi za Raundi ya Mtoano ya UCL na ile ya EUROPA LIGI itafanyika Desemba 14.
Giroud akishangilia mbele ya Meneja Wenger
Olivier Giroud alifungia Arsenal mabao matatu kwa mara yake ya kwanza na kuhakikisha Gunners wanaendeleza rekodi yao nzuri Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya na kufika hatua ya 16 bora kwa kulaza Olympiakos.
Arsenal walihitaji kushinda kwa mabao mawili wazi lakini walipata mabao hata zaidi na kumaliza wa pili Kundi F.
Giroud alianza kwa kufunga kwa kichwa kipindi cha kwanza, kisha akafunga la pili kipindi cha pili kwa usaidizi kutoka kwa Joel Campbell.
Mfaransa huyo alihakikisha Arsenal wanafuzu kwa kufunga la tatu kupitia penalti.
Man Utd kucheza Europa League
Arsenal hawajawahi kukosa kufika hatua ya muondoano Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya tangu kuanza kwa mfumo wa sasa 2003-4, na walionyesha uzofu wa kusakata gozi katika jukwaa kuu Ulaya kwa kung’aa Athens.

Takwimu muhimu:
Olivier Giroud ndiye mchezaji wa nne kufungia Arsenal hat-trick kwenye Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya (baada ya Thierry Henry, Nicklas Bendtner na Danny Welbeck).
Vijana wa Arsene Wenger wameshinda mechi yao ya kwanza Ugiriki tangu Desemba 1998 (3-1 dhidi ya Panathinaikos).
Giroud ndiye mchezaji was aba wa Arsenal kufikisha magoli kumi Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya (wengine wakiwa Henry, van Persie, Ljungberg, Fabregas, Walcott na Pires the others).
Matokeo ya Jumatano yalifikisha kikomo msururu wa kutoshindwa wa Olympiakos wa mechi sita katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya timu za Uingereza(Kushinda 5, Sare 1)
Arsenal walikuwa wameshindwa mechi tatu zao za awali ugenini dhidi ya Olympiakos zote katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, zote katika mechi ya sita hatua ya makundi.Bao hilo lilifungwa kwa kupitia mkwaju wa penatiKipa Roberto hakuona ndaniGiroud akishangilia bao lakeGiroud pia ndie aliyefunga bao la pili na kufanya 2-0Pongezi zikiambatana na mshangao!Meneja Arsene WengerFlamini na Kassami wakigombea mpira wa kichwaKikosi cha ArsenalArsene Wenger na Msaidizi wake Kabla ya Mechi!
 


Garry Monk.
Klabu ya Swensea City imemtupia virago kocha wake Garry Monk baada ya kushinda mchezo mmoja kati ya 11 ambayo ameingoza Swansea kwenye ligi ya England msimu huu.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 36 amekuwa kwenye kikosi hicho kwa zaidi ya miaka 11 akianza kama mchezaji lakini baadae mwaka 2014 akabidhiwa timu hiyo kama kocha mkuu akichukua nafasi ya Michael Laudrup.
Kipigo cha Jumamosi iliyopita cha magoli 3-0 dhidi ya Leicester City ulikuwa ndio mchezo wake wa mwisho kama kocha na amekiacha kikosi hicho kikiwa nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi.
Waving goodbye: Garry MonkKocha huyo alijiunga na Swansea City kama mchezaji mwezi June mwaka 2004, akaisaidia Swansea kupanda daraja kucheza ligi kuu mwaka 2011 akiwa nahodha wa timu hiyo.
February 2014 aliteuliwa kuwa kocha wa muda lakini May 2014 akapewa nafasi hiyo kama kocha mkuu.
Mwezi August 2014 Swansea ilipata ushindi wa ugeni I dhidi ya Manchester United na huo ukawa ni ushindi wa kwanza kwa Swansea kwenye uwanja wa Old Trafford.
Swansea ilimaliza katika nafasi ya juu kwenye ligi msimu wa 2014-15 ikiwa nafasi ya nane kwa kufikisha jumla ya ponti 58.

waliotembelea blog