Tuesday, November 12, 2013

Paul Matthysse ‘P-Funk’ akionesha jeraha alilolipata kichwani baada ya kuanguka chooni.
P alidamka alfajiri kwenda msalani kujisevu mambo ya short-call, akiwa huko alishikwa na kizunguzungu cha ghafla kisha akaanguka kama mzigo.
Ajali hiyo, ilimkuta P alfajiri ya Ijumaa iliyopita na kuhusu hilo, mwenyewe alifunguka: “Nilishangaa sana, unajua siku hiyo sikuwa nimekunywa pombe kusema labda nilikuwa nimelewa, nilishangaa tu napatwa na kizunguzungu kisha nikaanguka.”
Chooni alipodondoka P-Funky.
HAIKUWA AJALI NDOGO
Stori kwamba mtu kaanguka chooni, inaweza kuchukuliwa ni ndogo lakini inabainishwa ukubwa wake kutokana na athari ya baadaye.
KWANZA; Kichwa kimepasuka sehemu ya usoni, juu ya macho na alipofikishwa Hospitali ya Aga Khan, alishonwa nyuzi 12.
PILI; Pale chooni, sehemu aliyoangukia, imepasuka. Hii ni kuonesha kuwa kishindo kilikuwa kikubwa. Inafahamika kuwa sinki la choo ni gumu sana kwa sababu hutengenezwa na malighafi imara.
‘P-Funk’ akiwa na jeraha kichwani baada ya kuanguka chooni.
BAADA YA KUANGUKA ALIZIMIA
Japokuwa P a.k.a Majani alikuwa hataki kulizungumzia hili lakini alipobanwa sana na Showbiz alisema: “Baada ya kuanguka pale chooni, nilizimika kabisa. Nikawa sijitambui kwa dakika kadhaa, zinaweza kuwa 10 mpaka 20. Nilipozinduka nilikuwa na maumivu makali.

“Nilipata kampani ya nyumbani, tukaenda Aga Khan ambako nilipewa matibabu. Nilishangaa baada ya kushtukia nimeshonwa nyuzi 12.”
HII INAMAANISHA NINI KWA P?
Hana tatizo lolote la kiafya linaloweza kumlazimisha kuanguka ghafla, zaidi kwa siku hiyo hakuwa amelewa, hii inamaanisha nini?


P anajibu: “Sijui nimepatwa na nini, inabidi nifanye uchunguzi zaidi kubaini tatizo hasa linalonikabili. Ni vizuri kulishughulikia mapema.”
Hata hivyo, wakati P akisema anataka kufanya uchunguzi zaidi kuhusiana na afya yake, Showbiz linazo data kuwa katika siku za karibuni Majani amekuwa mwenye pilika nyingi, akifanya kazi kwa muda mrefu bila kupumzika.

Uchunguzi umebaini kuwa prodyuza huyo yupo resi na kazi zake za uprodyuza, akifanya kazi mpaka usiku wa manane, vilevile akidili mstari wa mbele na uanzishwaji wa Chama cha Maprodyuza wa Mapigo ya Muziki Tanzania (TSPA), yeye akiwa ndiye mwenyekiti.

Majani anakiri hilo: “Ni kweli, daha! Mzee katika siku za karibuni nimekuwa bize sana, inawezekana hilo nalo likawa tatizo.”
AAMUA KWENDA MAREKANI
Kuhusu uchunguzi wa afya yake, Majani ambaye ni Mkurugenzi wa Studio ya Bongo Records, alisema: “Japo kwa sasa naendelea vizuri ila nina safari ya Marekani very soon, huko nitafanya checkup ya uhakika, ili kama kuna matatizo ya kichwa au mishipa ya fahamu nipate tiba haraka.”

Wakazi wa mtaa wa migombani kata ya segerea wakiwahoji matapeli ambao walikua wakijaribu kumfanyia utapeli dada mmoja na hatimaye kushindwa kutimiza lengo lao mara baada ya dada huyo kushtukia mbinu zao na kuomba msaada kwa wananchi na ndipo hapo walipotiwa nguvuni na kupelekwa katika ofisi za serikali ya mtaa wa migombani
Matapeli (mwenye shati la draft) wakipewa kichapo mara baada ya kushindwa kujibu maswali ya wananchi waliowakamata leo katika kituo cha daladala cha Segerea
Mmoja wa watumishi wa serikali ya Mtaa wa Migombani Kata ya segerea Mfaume (wa kwanza kushoto Mwenye fulana ya njano) akijaribu kuwakata wananchi hao kujichukulia sheria Mikononi mara baada ya kuwatia nguvuni matapeli hao leo katika kituo cha daladala cha Tabata Segerea
Mmoja wa matapeli akijizuia kichwani mara baada ya wananchi wenye hasira kali wakiendelea kushusha kipigo kitakatifu, katika tukio la kujaribu utapeli lililotokea muda mfupi katika kituo cha daladala cha segerea mwisho 
Hapa tapeli wa pili (aliyeinamishwa kichwa) akiendelea kupokea maumivu kutoka kwa wakazi wa segerea mara baada ya kukamatwa wakati wakitaka kujaribu kutapeli 
kipigo kikiendelea kutolewa kwa matapeli hao
Matapeli wakiwa ndani ya ofisi ya serikali ya mtaa wa migombani mara baada ya kupokea kipigo cha mbwa mwizi muda mfupi uliopita katika kituo cha daladala cha segerea mwisho wakati wakijaribu kutapeli
Baadhi ya wakazi wa mtaa wa migombani kata ya segerea wakichungulia dirishani katika ofisi za serikali ya mtaa wa migombani kwaajili ya kushuhudia matapeli waliopokea kichapo cha mbwa mwizi mara baada ya mbinu zao kufua dafu na kushtukiwa
Weekend iliyopita msanii wa muda mrefu wa muziki wa Dancehall Hard Mad ametoa wimbo mpya ambao ni jibu la hit song ya Lady JayDee ‘Yahaya’. Swali la Jide “Yahaya unaishi wapi” ndio limezaa jina la wimbo wa Hard Mad aliyejibu ‘Naishi Ghetto’, na mambo mengine yote yaliyoimbwa katika wimbo huo ni majibu ya maswali ya ‘Yahaya’.

Hard Mad
Hard Mad amezungumzia jinsi wazo la kufanya wimbo wenye majibu ya ‘Yahaya’ lilivyopatikana, na kudai kuwa alilipata baada ya kukutana na mtu aitwaye Yahaya anayeishi Kinondoni kama ilivyotajwa katika wimbo wa Jide.
Idea ilikuja kama hivi, kuna mshikaji mmoja amekuja kutoka Dar es salaam ambaye yeye ni mwana sana katika upande wa filamu…yeye ndio alinipa hiyo idea bwana blaza eeh mimi naitwa Yahaya naishi Kinondoni , sasa naona kama hii ngoma imenilenga nini nikamwambia hamna labda katika art tu ya mtu na nini na nini sababu wale Yahaya wanaoishi Kinondoni bado ni wengi”. Hard Mad alizungumza jana kupitia Showtime NewChapter ya Radio Free Africa, Mwanza na Renatus Kiluvia aka Bizzo.
Hard Mad aliendelea kusimulia kuwa baada ya Yahaya kumfuata alimwambia wimbo wa Jide umemsababishia awe na wakati mgumu kutokana na jinsi watu wanavyomchukulia sasa wakidhani anayeimbwa ni yeye kutokana na mambo mengi yaliyoimbwa yanamhusu moja kwa moja.
Akaniambia ndio lakini inaniuma sana lakini mimi nilikuwa naishi na watu vizuri naendesha mandinga ndinga za watu wananiamini lakini saizi naona kila mtu ninaemfuata ananiambia we Yahaya tu unajua zile.” Alisema.
Alivyokuja ndio akaniambia bwana blaza mi sio msanii lakini hii idea unaweza kuifanyia kitu flani kwasababu wewe ni msanii wa zamani na sikuwaza kama nitakutana na wewe studio kama hivi nilikuwa nakusikia tu kwenye radio na kukuona kwenye TV nashukuru nimekuona labda unaweza ukanifanyia kitu kuhusiana na hili ili roho yangu na mimi isuuzike.
Hard Mad ameendelea kusema kuwa baada ya kupewa idea na Yahaya aliusikiliza vizuri wimbo na kujaribu kuanza kutengeneza jibu,
“Kwahiyo ndio hivyo idea ilivyokuja na mimi nikakaa nikaisikiliza nikajaribu kufanya kitu naona na kitu kikakua na pia katika upande mmoja au mwingine nikawa nimeona kama ni art pia kwasababu hata ukisikiliza miziki ya zamani ya kina Marijani Rajab, Msondo ukisikiliza Juwata Jazz kuna design flani walikuwa wanafanya ya music, kwamba huyu anaweza akatoa swali mwingine akajibu na ndo kitu ambacho kilikuwa kinafanya hasa ukue katika kiwango kikubwa sana hapa nchini.
Lakini sikuhizi naona hicho kitu kinaenda kinakufa hata watu wakijibu wanakuwa yani hata kama mtu ameuliza swali wengine wanaogopa kujibu wanaona kama watabeef, lakini mi nahisi sio kubeef ni kwamba unafanya sanaa inakuwa na changamoto.” Alisema Hard Mad.

Msikilize Hard Mad hapa

man-water Man Water kushoto
Ukiskiliza vizuri beat ya ‘Naishi Ghetto’ ni kama ile ile ya Yahaya lakini imepigwa upya, producer wa ‘Yahaya’ ya Anaconda, Man Water wa Combination Sounds pia amezungumzia wimbo huo na kudai kuwa yeye hajahusishwa kwa namna yoyote katika kuombwa idhini ya kutumiwa kwa ubunifu wa kazi yake katika wimbo wa Hard Mad.
Maoni yangu na kwa jinsi nilivyoiskiliza kwanza kitu kimenishangaza isipokuwa huwa najua harakati za kuna vitu vinaitwa riddim, yaani mtu unaweza ukaendeleza idea au ukaonesha unashow love kwenye idea ambayo watu wameshaianzisha. Lakini hii naona iko tofauti kwasababu hakuna taarifa yoyote lakini kwasababu hata kama utapata go ahead kutoka kwa msanii bado unatakiwa upate Baraka zote kutoka kwa producer kwasabbau hata Jide mwenyewe Yahaya ni kwamba aliikuta beat si kwamba alikuja akaniimbia ili nitengeneze beat.” Alisema Water
Mi naona kilichofanyika si sawa kwasababu hakukuwa na mawasiliano, unaweza ukapewa go ahead kwamba poa baada ya kusikiliza unataka kuimba nini lakini naweza nikakubali hayo yote sababu pengine ni namna ya mtu kutafuta namna ya kutoka, na wakati mwingine tukiwa tunazizungumzia mambo haya kama hivi ndio tunazidi kumpa mtu credit, lakini mi naona bigup apewe yule mtu ambaye alianzisha idea big up to Lady JayDee afu big up to Combination Sounds Kombinenga.” Aliongeza Man Maji wa Kombinenga
Water amesema kuwa nyimbo kama hizo huwa ni za kiharakati tu na hazistahili kuchezwa kwenye radio bali zinafaa kusambazwa katika mitandao ya kijamii peke zaidi.
Man Water aliulizwa juu ya hatua anazopanga kuchukua baada ya kuusikia wimbo huo wa Hard Mad:
Haya mambo ya haki miliki bado vitu vingi havijakaa sawaswa watu wengi sana wanauchezea muziki wanachezea pia kazi za watu wengi sana. Kwahili siwezi kusema chochote ni mapema sana kwasababu track nimeisikia leo, sijazungumza na Jide kama kuna taarifa zozote lakini ninauhakika kwasababu track haijatendewa haki kama vile iko chini ya kiwango sisemi kwa ubaya lakini ukizi compare unaweza ukaona mmoja anaeleweka anaongea nini mwingine haeleweki.
Water ameonesha kutokuwa na tatizo na Hard Mad kwasababu wanafahamiana vizuri, isipokuwa amesisitiza kitu ambacho hakubaliani nacho ni kitendo cha kutopewa taarifa mapema na wahusika.
Lakini pia Hardmad ni mwanangu hata hivyo nimeshangaa kwasababu Hard Mad kwanini asizungumze na mimi afu ni mshikaji wangu sana tena sio kitoto kiasi kwamba hata akisikia mimi nazungumza nay eye kupitia media kama hivi anaweza na yeye akashtuka kidogo lakini ni mtu ambaye tuko naye Kino tunaweza tukazungumza….tukatoa Baraka za ile go ahead ya kufanya anachokifikiria kufanya, lakini sivyo hivi alivyofanya sababu yeye kama ni msanii mkubwa sijui analeta picha gani kwa wasanii ambao wanachipukia wanaweza wakaona hii ndio njia sahihi ya kutoa track.
Msikilize Man Water
MSIMAMO ULIVYO KWA SASA:
2013-2014 Barclays Premier League Table
  Overall
Home
Away
 
POS
TEAMPWDLFA
WDLFA
WDLFA
GDPts
1 Arsenal 11 8 1 2 22 10
4 0 1 11 5
4 1 1 11 5
12 25
2 Liverpool 11 7 2 2 21 10
5 0 1 13 3
2 2 1 8 7
11 23
3 Southampton 11 6 4 1 15 5
4 2 0 11 2
2 2 1 4 3
10 22
4 Chelsea 11 6 3 2 18 10
5 1 0 14 5
1 2 2 4 5
8 21
5 Manchester United 11 6 2 3 18 13
3 2 1 8 5
3 0 2 10 8
5 20
6 Everton 11 5 5 1 14 10
3 2 0 6 3
2 3 1 8 7
4 20
7 Tottenham Hotspur 11 6 2 3 9 6
3 1 2 5 5
3 1 1 4 1
3 20
8 Manchester City 11 6 1 4 28 12
5 0 0 20 2
1 1 4 8 10
16 19
9 Newcastle United 11 5 2 4 15 16
2 2 1 7 5
3 0 3 8 11
-1 17
10 West Bromwich Albion 11 3 5 3 12 12
2 1 2 6 4
1 4 1 6 8
0 14
11 Aston Villa 11 4 2 5 11 12
2 0 4 6 9
2 2 1 5 3
-1 14
12 Hull City 11 4 2 5 9 14
3 2 0 4 1
1 0 5 5 13
-5 14
13 Swansea City 11 3 3 5 15 15
1 3 2 11 11
2 0 3 4 4
0 12
14 Cardiff City 11 3 3 5 9 15
2 1 2 5 5
1 2 3 4 10
-6 12
15 Norwich City 11 3 2 6 9 21
2 2 2 7 7
1 0 4 2 14
-12 11
16 West Ham United 11 2 4 5 9 11
1 1 3 5 7
1 3 2 4 4
-2 10
17 Stoke City 11 2 4 5 10 14
1 3 1 3 3
1 1 4 7 11
-4 10
18 Fulham 11 3 1 7 10 19
1 1 3 5 9
2 0 4 5 10
-9 10
19 Sunderland 11 2 1 8 8 22
2 0 4 6 10
0 1 4 2 12
-14 7
20 Crystal Palace 11 1 1 9 6 21
1 1 4 4 10
0 0 5 2 11
-15 4
Stori: Musa Mateja    
RAIS wa Wasafi Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond’, juzikati alifunguka kuwa kwenye maisha yake ya ndoa atakayoingia siku chache zijazo, aliyekuwa mchumba wake wakamwagana na kurejeana hivi karibuni, Wema Sepetu asitegemee kuolewa naye.

Diamond ambaye ni staa wa Bongo Fleva aliyasema hayo mbele ya paparazi wetu Novemba 7, mwaka huu jijini Dar kufuatia kuulizwa anamchagua nani wa kumuoa kati ya Wema Sepetu na mchumba wake wa sasa, Penniel Mungilwa ‘Penny’.

Swali kwa Diamond liliibuka baada ya kuzagaa kwa tetesi kwenye mitandao ya kijamii kwamba yu mbioni kumvisha pete ya uchumba mmoja wa mademu zake.

Swali hilo lilimfanya Diamond afunguke kwa kusema kwamba anachokijua yeye na ambacho kipo kwenye mikakati yake, mke wake mtarajiwa ni Penny.

“Najua wengi wanahisi mimi ninaweza kuoa mwanamke zaidi ya mmoja kutokana na dini yangu kuruhusu lakini jambo hilo mimi silifikirii hata kidogo kwa kuwa kwenye maisha yangu nilishapanga nitaoa mke mmoja tu,” alisema Diamond.

Akaendelea: “Watu wanasema mengi juu yangu na Wema, wengi wao hawajui nafsi yangu inataka mwanamke yupi, ninachoweza kusema na watu wakasikia na kunielewa basi wajue kwamba Penny ndiye mke wangu, Wema asitegemee kuolewa na mimi.”

Diamond alikwenda mbele zaidi kwa kumwanika Penny kwamba ana sifa ya kuwa mke kwani ni mvumilivu sana na anaonesha upendo wa dhati kwake.

“Kwa maana hii basi hakuna mwanamke mwenye jina  kubwa wala sura nzuri zaidi ya Penny ninayeweza kumwita mke wangu. Najua kila mtu ana namna yake ya kuchagua ampendaye, ndiyo maana utaona watu wanasema hili mara lile, lakini hawajui nafsi yangu inataka mwanamke wa aina gani,” alisema Diamond na kuongeza:

Kama kuna demu anayejipa matumaini hayo basi asitegemee hata siku moja kwa sababu kuoa kwangu kutazingatia mke mwema na si bora mke, Penny pekee ndiye mwenye sifa za kuwa mke wangu,” alisema Diamond.

Juzi Ijumaa Wikienda lilimpigia simu Penny ili kutaka kupata maoni yake kuhusu tamko la Diamond, lakini muda mrefu simu hiyo ilikuwa ikiita bila kupokelewa.

Baada ya kumkosa Penny, Ijumaa Wikienda lilimtwangia simu Wema, naye kama Penny, simu yake iliita mara kadhaa lakini haikupokelewa.
Chanzo:Global Publishers
Mwanamuziki nyota wa muziki wa kizazi kipya usiku wa kuamkia Jumatatu alionja joto ya kiwe baada ya kutekwa na kusurubiwa kisha kunyang'anywa kila kitu pamoja na gari yake.


Mwanamuziki huyo akiwa kwenye viunga vya Club ya usiku ya Kibo iliyopo Tegeta Jijini Dar pamoja masisita du wakila bata ghafra kundi la watu watano lilimvamia na kumkamta msobe msobe hadi nje ya ukumbi pamoja na kumrukisha kichurachura huku wakina dada waliokuwa wamendamana nao wakilia kwa uchungu kwa kumuonea huruma.

Habari zaidi toka kwa chanzo chetu kilichoshuhudia timbwiri hilo kilisema kuwa chanzo cha tukio hilo ni kudaiwa kwa Matonya na mtoto wa mjini aliyefahamika kwa jina la Evance" Huyu Evance ni mtoto wa mjini na huwa anawakopesha pesa wanamuziki mbalimbali pamoja na wasanii wa bongo movie hivyo miezi ya hivi karibuni alimkopesha shilingi laki nne msanii huyo kwa madai kuwa hakuwa na pesa ya kula bata wikiendi ambapo baada ya kumkopesha msanii alianza kuzungusha kurudisha hali iliyomfanya Evance kuchukua hatua za kumfanyia unyambilisi huo" Kilisema chanzo chetu

Hata hivyo baada ya kumkamata msanii huyo Evance alimpelekwa Oysterbay ambapo aliiacha gari na simu kwa makubaliano atakapoleta pesa hiyo atapewa gari yake.
Kijana anayefanya vizuri kwenye muziki wa Bongo Fleva Diamond Platnumz mambo si mabaya kwake baada ya kuonyesha mjengo wake mwingine wa hatari ambao bado upo katika ujenzi. 

 
Kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram,Diamond jana ame-share picha ya nyumba hiyo na chini akatia neno..Shuka nayo.

''Toa kitu weka kitu...! Ndio tulivyo funzwa...stareh tunawaachia wajanja wa mji... #WCB #Wasafi for the Fkn Life!''

Haijajulikana mjengo huu uko maeneo gani wala umegharimu kiasi gani
ila inaendelea kudhihirisha mafanikio anayoendelea kuyapata Diamond.
MSANII wa filamu wa kike Bongo Irene Uwoya yupo katika maandalizi ya kuanza mazoezi ya ngumi baada ya kumpata mwalimu ambaye ni Bondia maarufu Rashid Matumla ‘Snake Boy’ akiongea na FC Irene kasema kuwa ameamua kufanya mazoezi kwa ajili ya kujiweka vema na kulinda nafasi yake ya uigizaji kwani amegundua wasanii wengi wanapoteza mvuto kwa kujiachia kwa unene.

Irene Uwoya, Rashid Matumla, Francis Cheka, Lumole Matovolwa
Irene Uwoya akiwa na timu ya mabondia na Biggie
Irene Uwoya, Rashid Matumla
Irene Uwoya akiwa na Mwalimu wake Snake Boy kwa ajili ya kujifua.
Nimejipanga kwa kufanya mazoezi ya nguvu chini ya mwalimu wangu Rashid Matumla na nipo fiti kwa ajili ya kujifua najua kuigiza ndio ajira yangu lakini nikijiachia na kunenepa bila mpango nitaanza kucheza nafasi za akina bibi muda si mrefu na najiona mwili
unavyoninyemelea sitaki manyama uzembe,
anasema Irene Uwoya.
Irene ni moja kati ya wasanii wakali wanaofanya vizuri katika tasnia ya filamau Bongo huku pia akiwa ni moja kati ya watayarishaji wa filamu wanadada akiwa ameandaa filamu la Apple filamu iliyotengenezwa kwa gharama kubwa na kuwashirikisha wasanii kama Patcho Mwamba, Baba Haji na wasanii wengine wanaofanya vizuri katika tasnia ya filamu Bongo.

MSAADA
Nakukubali sana, napenda unipe nafasi niwe chini ya lebo yako. Geofrey, Kibaha, 0713434329
BOB JUNIOR: Njoo studio kwangu (Sharobaro) nikusikilize kama unafaa basi nitakuchukua tufanye kazi pamoja.

ANATOKA NA AUNT LULU?
Bob Junior nataka kujua, eti wewe unatoka kimapenzi na Aunt Lulu (Lulu Mathias), mlimbwende wa Kimwana Manywele? Salim Liundi, Dar, 0658110395
BOB JUNIOR: Hapana.


KWA NINI AMEACHANA NA MKEWE?
Bob Junior upo fresh kwenye gemu lakini mbona umemuacha mkeo na kuanza kumsifia Vanessa Mdee kwenye media? Unataka kumuoa? Mama Un, Dar, 0757715360
BOB JUNIOR: Mke wangu nimeachana naye kwa sababu za kifamilia, Vanessa ni mwanamke mzuri anapaswa kusifiwa.

KUUZA SURA
Kwa nini wasanii wengi wanaotolea nyimbo kwako unataka mpaka na wewe uuze sura kwenye video? Jakobo, Dar, 0689619817
BOB JUNIOR: Mara nyingi huwa naweka lebo yangu kutokana na wasanii wenyewe kutaka nifanye hivyo.

AMEZAA NJE YA NDOA?
Bob Junior uko vizuri sana hasa kwenye kuimba. Mtaani kuna tetesi kuwa una mtoto mwingine wa kike nje ya ndoa. Je, ni kweli? Raphael, Morogoro, 0713850820
BOB JUNIOR: Hapana mimi nina mtoto mmoja tu niliyempata ndani ya ndoa.

HUYU ANATAKA KUJUA

Bob Junior mtoto wako anaitwa nani na mnaishi wapi? Msomaji, 0682022412
BOB JUNIOR: Mtoto wangu anaitwa Rummy, ninaishi Magomeni-Mapipa, Dar.

YEYE NA WEMA VIPI?
Bob Junior uliwahi kutoka kimalavidavi na Wema na kumsababishia kipigo kutoka kwa Diamond (Nasibu Abdul). Erasto, Dar, 0765302086
BOB JUNIOR: Sina jibu.

BIFU NA DIAMOND
Nasikia wewe na Diamond mna bifu la chini kwa chini, ni kweli? Davy Ruta, Mwanza, 0769666622
BOB JUNIOR:

STAILI YA MUZIKI

Nakupa big up Bob Junior kwa kuwa mfano bora, vipi mipango yako ya baadaye hufikirii kubadili aina ya uimbaji wako ukaanza kuchana? Msomaji, 0719041057
BOB JUNIOR: Asante, sina mpango huo kwa sababu kuchana hakuna biashara.

NI KWELI DIAMOND ALIMPIGIA MAGOTI?

Bob Junior napenda sana staili yako ya uimbaji. Je, ni kweli Diamond alikuja kupiga magoti kwako? Fred Boy, Dar, 0656552592
BOB JUNIOR: Kweli alishaomba msamaha.

ANA MARINGO?
Nakupenda sana Bob Junior ila unachonikera ni maringo tu, jaribu kuwa kama JB (Steven Jacob) mbona utakuwa poa tu! Msomaji, 0655542810
BOB JUNIOR: Mimi sina maringo huo ni mtazamo wako tu.

MAUNO JUKWAANI

Kwa nini Bob Junior unapenda kukatika mauno jukwaani? Msomaji, 0753630184
BOB JUNIOR: Ninakata mauno kwa sababu muziki wangu unaruhusu.

waliotembelea blog