Monday, March 10, 2014

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger na wachezaji wake leo hii asubuhi kwenye mazoeziKocha wa Arsenal, Arsene Wenger
Arsene Wenger akihakikisha timu yake inafanya mazoezi ya kutosha.Mertesacker na KoscielnyKocha nae ni mchezaji bwana....Wachezaji kutoka Ujerumani hawa....wakiteta hapa...Podolski na OzilOzil na Podolski
UEFA CHAMPIONS LIGI
Raundi ya Mtoano ya Timu 16
MARUDIANO

Jumanne Machi 11
22:45 Bayern Munich v Arsenal FC (2-0)
22:45 Atletico de Madrid v AC Milan (1-0)
Jumatano Machi 12
22:45 FC Barcelona v Manchester City (2-0)
22:45 Paris Saint-Germain v Bayer 04 Leverkusen (4-0)
Jumanne Machi 18
22:45 Chelsea FC v Galatasaray Spor Kulübü [1-1]
22:45 Real Madrid CF v Schalke 04 [1-6]
Jumatano Machi 19
22:45 BV Borussia Dortmund v Zenit St. Petersburg [4-2]
22:45 Manchester United v Olympiacos CFP [0-2]

    Arsenal na Bayern Munich nanone



     


    Pichani ni baadhi ya wachezi wa Arsenal na Bayern Munich.
    Michuano ya kuwania kombe la klabu bingwa barani Ulaya kuendelea leo usiku huku kukiwa na mechi mbili.
    Arsenal, inaelekea, Bonn, kutoana jasho na mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munichambayo ilishinda mechi ya raundi ya kwanza kwa mabao mawili kwa nunge katika uga wa Emirates.
    Hata hivyo Arsenal itakosa huduma za mcheza kiungo wake Kieran Gibbs ambaye kwa sasa anauguza jeraha la mkuu na mshambulizi Yaya Sanogo, lakini mlinda lango Laurent Koscielny, ambaye alikuwa akiuguza jeraha la pajaanatarajiwa kurejea.

    Kipa Lukasz Fabianski naye atachukuwa mahala pa Wojciech Szczesny, ambaye amesimamishwa kucheza kwa muda baada ya kupewa kadi nyekundu wakati wa mechi ya raundi ya kwanza.
    Mwaka uliopita Arsenal iliishinda Bayern kwa magoli mawili kwa bila katika mechi ya marudiano lakini ilibanduliwa nje ya mashindano hayo baada ya kupoteza raundi ya kwanza 3-1.
    Katika mechi nyingine ya marudiano leo usiku itakuwa kati ya Atletico Madrid na AC Milan. Madrid ilishinda awamu ya kwanza kwa bao moja kwa bila.
    Mario Balotelli huenda akajumuishwa kwenye kikosi cha wachezaji kumi na mmoja wa AC Millan, baada ya kuuguza jeraha la mgongo alilopata siku ya Jumamosi dhidi ya klabu ya Unidese.
    Atletico nayo inamkaribisha mchezaji wake aliyefunga idadi kubwa yua magoli Diego Costa huku ikijaribu kufunzu kwa robo fainali ya kombe hilo kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya miaka kumi na saba iliyopita.
    Na ili kufuzu, mabingwa hao mara saba wa Ulaya ni sharti waandikishe historia ya kuwa timu ya tatu katika historia ya kombe hilo kuwahi kushindwa nyubani katika mechi ya raundi ya kwanza na ishinde mechi ya marudiano ugenini.


    Kwa mujibu wa mtandao wa Goal.com, nahodha wa timu ya taifa ya Ureno na mwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo ndio mwanasoka tajiri zaidi duniani.

    Katika listi hiyo iliyotangazwa leo, Ronaldo amerithi nafasi ya kwanza iliyokuwa ikishikiliwa na David Beckham kwa muda mrefu kaba ya kustaafu msimu uliopita. Ronaldo ambaye alisaini mkataba mnono zaidi na Real Madrid miezi kadhaa iliyopita amempita mshindani wake Lionel Messi na mwanasoka anayelipwa zaidi kimshahara Wayne Rooney.

    Samuel Eto'o ndio muafrika pekee aliyeweza kuingia kwenye listi ya wanasoka matajiri zaidi duniani.

    LISTI KAMILI
    1. Cristiano Ronaldo £122m
    2. Lionel Messi £120.5m
    3. Samuel Eto'o £70m
    4. Wayne Rooney £69m
    5. Kaka £67.5m
    6. The Neymar family £66m
    7. Ronaldinho £64m
    8. Zlatan Ibrahimovic £57m
    9. Gianluigi Buffon £52m
    10. Thierry Henry £47m
    SOURCE: Goal.com




    NA
    TIMU
    P
    W
    D
    L
    GD
    PTS
    1
    Azam FC
    18
    11
    7
    0
    23
    40
    2 
    Mbeya City
    21
    10
    9
    2
    10
    39
    3 
    Yanga SC
    17
    11
    5
    1
    29
    38
    4
    Simba SC
    21
    9
    9
    3
    17
    36
    5
    Kagera Sugar
    20
    7
    8
    5
    2
    29
    6
    Ruvu Shooting
    20
    7
    7
    6
    -4
    28
    7
    Coastal Union
    20
    5
    11
    4
    5
    26
    8
    Mtibwa Sugar
    20
    6
    7
    7
    -1
    25
    9
    JKT Ruvu
    21
    8
    1
    12
    -13
    25
    10
    Prisons FC
    19
    3
    10
    6
    -3
    19
    11
    Mgambo JKT
    20
    4
    6
    10
    -17
    18
    12
    Ashanti United
    21
    4
    6
    11
    -18
    18
    13
    JKT Oljoro
    21
    2
    9
    10
    -16
    15
    14
    Rhino Rangers
    21
    2
    7
    12
    -14
    13
    RATIBA MECHI ZIJAZO:
    Jumatano Machi 12

    Simba v Coastal Union
    Mgambo JKT v Mtibwa Sugar
    Jumamosi Machi 15
    Azam FC v Coastal Union
    Mtibwa Sugar v Yanga
    Ruvu Shooting v Ashanti United
    Kagera Sugar v Tanzania Prisons
    Jumapili Machi 16

    JKT Ruvu v Mbeya City
    Jumatano Machi 19
    Yanga v Azam FC

    DSC_0166 
    Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka (kushoto), akimsikiliza Mkuu wa Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT), Dkt. Zakaria Mganilwa ofisini kwake kabla ya kupokea magari mawili ambayo yamekabidhiwa kwa chuo hicho na Shirika la Transaid la nchini Uingereza, hafla ya kukabidhi magari hayo imefanyika leo asubuhi katika viwanja vya NIT.
    DSC_0171 
    Taswira ya tanker trailer la futi 40 na Folk Lift ambayo yamekabidhiwa kwa Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT) na Kampuni ya Transaid leo asubuhi katika viwanja vya chuo hicho. Magari hayo yatasaidia wanafunzi wanaosoma kozi za udereva chuoni hapo.
    DSC_0173 
    Sehemu ya Wafanyakazi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), wakimsikiliza Mgeni Rasmi (hayupo pichani), wakati wa hafla fupi ya kukabidhi magari mawili kwa ajili ya kufundishia mafunzo ya udereva chuoni hapo, magari hayo yalimekabidhiwa leo asubuhi na Shirika la Transaid la nchini Uingereza.
    DSC_0183     Mkurugenzi wa Mradi ya Usalama Barabarani wa Shirika la Transaid la Nchini Uingereza, Mr. Neil Rettie (mwenye tai ya blue) akimkabidhi funguo za gari aina ya Iveco kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt Shaaban Mwinjaka kwa ajili ya mafunzo ya Udereva yanayotolewa na Chuo Cha Taifa Cha Usafirhsaji (NIT), Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya chuo hicho leo Asubuhi.
    DSC_0185 
    Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka akiwasha gari ya kuinulia mizigo focal lift kama ishara ya kupokea moja ya magari mawili yaliyokabidhiwa na Shirika la Transaid la nchini Uingereza kwa Chuo cha Taifa cha Usafirshaji (NIT), leo asubuhi. Anayeshuhudia ni Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Dkt.  Zakaria Mganilwa
    DSC_0192 
    Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt Shaaban Mwinjaka, akiwasha gari aina ya Folk Lift lililokabidhiwa kwa Chuo Cha Taifa Cha Usarifshaji (NIT), kwa ajili ya wanafunzi wataochukua mafunzo ya udereva chuoni hapo. Magari hayo yamekabidhiwa leo asubuhi katika viwanja vya Chuo hicho.

    kiti 11 
    Na Boniface Wambura
    Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) tunalaani vikali fujo na uhabirifu wa mali unaofanywa na washabiki viwanjani wakati mechi mbalimbali zikiwemo zile za kimataifa na ligi za hapa nchini.
    Tunaiomba radhi Serikali kwa uharibifu wa viti uliotokea kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga ya Tanzania na Al Ahly ya Misri iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Uharibifu huo wa viti umesababisha hasara ya sh. milioni 15 kwa wamiliki wa uwanja huo ambao ni Serikali. TFF tutalipa fedha hizo kwa Serikali kutokana na uharibifu huo.
    kusoma zaidi bofya hapa chini

    Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Kebwe Kebwe akihutubia kwa niaba ya 
    Makamu wa Rais Dk. Mohamed Garib Bilal aliyekuwa mgeni rasmi wa ufunguzi wa kituo hicho.
    Ofisa Rasilimali Watu na Utawala wa Bohari ya Dawa (MSD), Shangwe Stephen akiwa kwenye hafla hiyo.
    Mbunge wa Muleba Kaskazini, Profesa Anna Tibaijuka. (kulia), akiteta jambo na Meneja wa MSD, Kanda ya Mwanza ambaye pia anahudumia kituo hicho cha Muleba, Dyekwifo Sabura.

    Wananchi mbalimbali wa wilayani Mulena na mkoa wa Kagera wakiwa katika hafla hiyo.
    Na Mwandishi Wetu, Muleba
    SERIKALI imeipongeza Bohari ya Dawa (MSD) kwa kuanzisha utaratibu wa kuweka alama ya GOT katika dawa inazosambaza jambo litakalo saidia dawa za serikali kutambulika kirahisi kwa wananchi hivyo kupunguza vitendo vya wizi.
    Pongezi hizo zilitolewa na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Kebwe Kebwe kwa niaba ya Makamu wa Rais Dk.Mohamed Gharib Bilali ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Kituo cha Usambazaji dawa cha MSD wilayani Muleba mkoani Kagera kilicho zinduliwa mwishoni mwa wiki.
    “Naamini utaratibu huu wa kuweka alama hiyo umeanza kufanyika hivyo naagiza utekelezwe haraka na dawa zote ziwekewe alama hiyo ili kuepusha upotevu wa dawa za Serikali” alisema Kebwe.
    Kebwe alisema Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na Bohari ya Dawa imekuwa na ushirikiano mzuri  na  wadau mbalimbali wa maendeleo kama vile; Mfuko wa Kimataifa wa Kupambana na UKIMWI, Malaria na Kifua Kikuu (Global Fund) na Shirika la Misaada la Maendeleo la Marekani (USAID) ambao tayari wamekwishatoa msaada mkubwa wa ujenzi wa maghala ya kisasa ya kuhifadhia dawa katika mikoa mbalimbali nchini.
    Waziri Kebwe alitoa ushauri ushirikiano huo uendelezwe ili wadau hao waweze pia kutoa msaada wa ujenzi wa ghala la kisasa katika Halmashauri ya Muleba la kuhifadhia dawa na vifaa tiba.
    Alisema ufunguzi wa kituo hicho cha kusambazia dawa mkoani Kagera, ni mchango tosha katika kutekeleza Malengo ya Milenia hususan, kupunguza vifo vya akina mama na watoto, na kupambana na UKIMWI na Malaria.
    ” Kituo hiki kitatumika kuongeza ufanisi wa mfumo kufikisha dawa karibu na wananchi na kwa wakati ili kufanikisha lengo hilo mahsusi” alisema Dk. Kebwe.
    Alisema Serikali ilianzisha Bohari ya Dawa ili kufanikisha majukumu ya kununua, kuhifadhi na kusambaza dawa na vifaa tiba katika vituo vya umma vya kutolea huduma ya afya hapa nchini.
    Aliongeza kuwa pamoja na juhudi kubwa ambazo Serikali inafanya kupitia MSD ili kufanikisha upatikanaji endelevu wa dawa na vifaa tiba, bado vituo vingi vya kutolea huduma ya afya hasa vijijini vimekuwa na tatizo sugu la uhaba wa dawa muhimu hivyo Serikali itaendeleza juhudi hizo ili tatizo hilo liweze kupungua au kudhibitiwa kabisa.
    Alisema kwa sasa Bohari ya Dawa inawajibika kufikisha dawa na vifaa tiba moja kwa moja hadi kituo husika cha huduma ya afya badala ya kuishia kwa Mganga Mkuu wa Wilaya kama ilivyokuwa hapo awali.
    Kebwe alisema mfumo huu wa ufikishaji dawa moja kwa moja hadi katika vituo vya huduma na hospitali kwa kiasi kikubwa umesaidia sana upatikanaji wa dawa katika vituo vya umma vya kutolea huduma ya afya hasa vijijini.
    “Naagiza kuwepo ushirikiano wa karibu kati ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii (kupitia Bohari ya Dawa) na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu) ili kuhakikisha ufanisi katika jambo hili” alisema Kebwe.
    Katika hatua nyingine Dk. Kebwe amesema anatambua tatizo la dawa na vifaa tiba vya Serikali kupatikana katika maduka ya dawa ya watu binafsi jambo linaloikera sana Serikali hivyo ameiagiza Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kufanya msako endelevu ili kuwafichua na kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaopatikana na dawa za Serikali kinyume cha Sheria.
    Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini (MSD), Profesa Idris Mtulia alisema mkakati wa kushirikisha sekta binafsi ili kufanikisha upatikanaji wa dawa pindi Bohari ya Dawa inapokuwa na upungufu, unaendelea kutekelezwa sanjari na halmashauri zote nchini kuhimizwa kununua dawa kutoka MSD kwa kutumia vyanzo vingine vya fedha (kama vile Basket Fund, NHIF, Tele kwa Tele)
    Alisema pamoja na changamoto mbalimbali inazokabiliana nazo, Bohari ya Dawa kwa kushirikiana na Serikali na wadau wengine, itaendelea kutoa huduma bora na kuhakikisha kuwa dawa zenye ubora na bei nafuu zinakuwepo wakati wote kwa manufaa ya Watanzania.

    Ukikutana tu na picha hizi kwa mara ya kwanza, lazima kitakachokujia kichwani ni collable ya wawili hawa ambao ni ndugu, Queen Darleen na Diamond wameanza kupost picha hizi kupitia katika acc zao za mitandao mbali mbali ya kijamii bila ya kutoa information yoyote juu yake.



    katika Status ya picha hizi wawili hao wamekuwa wakiandika "Queen Darleen +Diamond= ?, status iliyowaacha wengi wakijiuliza ni ngoma au ni kitu gani
    .Mpaka sasa wawili hao hawajaongea chochote kuhusu hilo, we unaonaje? ni collable au?


    bunge_1e51a.jpg
    Rais Uhuru Kenyatta, atapunguziwa mshahara wake kwa Sh 248,000 za Kenya karibu sawa na dola 3,000, na naibu rais William Ruto anapunguziwa Sh210,000. mawaziri na makatibu wakuu wote wanapunguziwa pia mishahara yao kwa asili mia 10.
    Rais Kenyatta alitangaza uwamuzi huo siku ya Alhamisi baada ya mkutano na maafisa wa juu wa serikali na wajumbe wa kamati ya bajeti ya bunge mjini Nyanyuki, na kueleza kwamba serikali hivi sasa inatafakari na kujadili kupunguza matumizi ya safari za kigeni katika lengo la kupunguza matumizi na kuweza kupata fedha kutumika kwa miradi ya maendeleo.
    Akizungumza na waandishi habari baada ya mkutano huo, Rais Kenyatta alisema serikali inatafakari pia juu ya kufutilioa mbali matumizi ya umaa mabayo hayaleti faidi au kuimarisha maisha ya wakenya.
    Wachambuzi wa kisiasa wanasema uwamuzi huo wa kihistoria unaonekana umechukuliwa kwa lengo la kuanzisha mjadala wa kitaifa juu ya kupanga upya mishahara ya watumishi wa serikali na matumizi, juhudi zinazoongozwa na Tume ya Mishahara na Matumizi, inayojaribu kupunguza bajeti ya mishahara ambayo inafikia $ bilioni 5 kwa mwaka.
    Siku ya Jumatatu tume hiyo itakua na mjadala wa umaa juu ya mswada wa mishahara ya serikali katika ukumbi wa jengo mikutano ya kimataifa ya Kenyata KCC mjini Nairobi.


    kikwete_116dd.jpg
    Rais Jakaya Kikwete akiongoza Kikao cha Ujumbe wa Mawaziri na Wakuu wa Taasisi za Uhifadhi nchini kabla ya kuanza rasmi kwa Mkutano wa Kimataifa wa Kuzuia Biashara Haramu ya Wanyamapori jijini London, Uingereza.
    Mkutano wa Kimataifa kuhusu Biashara Haramu ya Wanyamapori (Conference on Illegal Wildlife Trade) unaanza rasmi leo katika ukumbi wa Lancaster House.
    Mkutano huu utakaohudhuriwa na jumla ya mataifa 47 na Mashirika 13 ya Kimataifa umeitishwa na Serikali ya Uingereza kwa lengo la kujadiliwa na masuala maalum matatu kuhusiana na biashara haramu ya wanyamapori. Masuala maalum uyanayotarajiwa kujadiliwa ni Jinsi ya Kuimarisha Usimamizi wa Sheria (Law Enforcement) na mchango wa mfumo mzima wa sheria za jinai (criminal justice system) katika kukabiliana na biashara hiyo.
    Aidha, utajadili Jinsi ya kupunguza hitaji la bidhaa zinazotokana na wanyamapori (demand for wildlife products) na Jinsi ya kusaidia Maendeleo Endelevu kwa Jamii zilizoathiriwa na biashara hiyo haramu.
    Mkutano huu utazungumzia wanyama aina ya tembo, faru na tiger. Wanyama hawa wamechaguliwa kwa kuzingatia jinsi wanavyoshambuliwa zaidi na makundi ya wawindaji haramu kwa lengo la kuu pembe na ngozi zao.
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete tayari ameshawasili Uingereza akiongoza ujumbe wa maafisa kutoka Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kushiriki Mkutano huu.



    Mjumbe wa bunge Maalum la Katiba Bw.  Augustino Mrema akimweleza jambo Mjumbe mwenzie Bw. Islaim Aden Rage leo Mjini Dodoma.

    Wajumbe wa Bunge Maalumla Katiba na Wajumbe wa kamati ya kuandaa rasimu ya kanuni zitakazotumika katika Bunge maalum la Katiba Bw. Prof. Costa Mahalu (Kulia) na Tundu Lissu wakielekea katika ukumbi wa bunge kwa ajili ya semina ya kuandaa kanuni zitazotumika katika bunge maalum la katiba, leo Mjini Dodoma.

    Wajumbe wa Bunge maalum la katiba Bw. Hamadi Rashidi (kushoto) Juma Alawi (katikati) na Thumwein Thuwein wakielekea katika ukumbi wa bunge kwa ajili ya semina ya kuandaa kanuni zitazotumika katika bunge maalum la katiba, leo Mjini Dodoma.

    Mjumbe wa Bunge maalum la katiba Bw. Ally Kessy akiwaeleza jambo jambo Wajumbe wenzie Bw. Edward Lowassa (katikati) na Almas Maige ndani ya ukumbi wa bunge leo mjini Dodoma.

    Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samwel Sitta (kulia) akimweleza jambo Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda ndani ya ukumbi wa bunge leo mjini Dodoma.

    Mjumbe wa bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya kuandaa rasimu ya kanuni zitakazotumika katika Bunge maalum la Katiba Bw. Prof. Costa Mahalu akiwaeleza jambo wajumbe wa bunge hilo wakati wa semina ya kuandaa kanuni zitazotumika katika bunge maalum la katiba, leo Mjini Dodoma.

    waliotembelea blog