Thursday, December 31, 2015


 Msanii Tekno Miles (wa kwanza kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla iliyomtambulisha rasmi kwa waandishi wa habari iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam. Msanii huyo anatarajiwa kuburudisha katika Tamasha la mwisho la “Grown and Sexy, the Gold finale” litakalofanyika katika ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga karibu na Best Bite katika mkesha wa mwaka mpya ambapo pia atafunga rasmi mfululizo wa matamasha hayo ya Grown And Sexy tokea kuanzishwa kwake.
Dj rasmi wa msanii Jay Z wa Marekani al maarufu kama “Young Guru” akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam ya kumtambulisha rasmi Msanii Tekno Miles (Katikati) ambaye anatarajiwa kuburudisha katika Tamasha la mwisho la “Grown and Sexy, the Gold finale” litakalofanyika katika ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga karibu na Best Bite katika mkesha wa mwaka mpya. Dj huyo atasimamia vilivyo kazi yake katika shughuli nzima ya Tamasha hilo. 
Meneja Chapa (pombe kali) wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Shomari Shija (Kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Msanii Tekno Miles (wa kwanza kushoto) na Dj rasmi wa msanii Jay Z wa Marekani al maarufu kama “Young Guru” wakati wa hafla iliyomtambulisha Msanii Tekno Miles kwa waandishi wa habari iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam. Msanii huyo anatarajiwa kuburudisha katika Tamasha la mwisho la “Grown and Sexy, the Gold finale” litakalofanyika katika ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga karibu na Best Bite katika mkesha wa mwaka mpya ambapo pia atafunga rasmi mfululizo wa matamasha hayo ya Grown And Sexy tokea kuanzishwa kwake. 


Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia kwa umakini mkutano wa kumtambulisha Msanii maarufu Tekno Miles kutoka Nigeria uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam ambaye anatarajiwa kutumbuiza katika mkesha wa Tamasha la Grown and Sexy the Gold finale litakalofanyika katika ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga karibu na Best Bite jijini Dar es salaam.



Maandalizi ya Tamasha maarufu la Johnnie Walker “Grown and Sexy The Gold finale” kwa ajili ya kuuaga mwaka na kuukaribisha mwaka mpya yanaendelea vizuri ambapo kwa mujibu wa waandaaji wa Tamasha hilo, “Capital events” kupitia wadhamini wao “Johnnie Walker” chapa maarufu ya pombe kali inayosambazwa na Kampuni ya bia ya Serengeti wamemleta Msanii Tekno Miles kutoka Nigeria kutumbuiza laivu katika Tamasha hilo ambalo litakua la mwisho kabisa katika historia ya matamasha ya Grown and Sexy nchini Tanzania.

Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari, uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam,Meneja chapa wa pombe kali SBL Shomari Shija alisema, “Tumeamua kulidhamini Tamasha hili kama njia mojawapo ya kujumuika na kufurahi kwa pamoja na wateja wetu wa chapa za Johnnie Walker katika kuuaga rasmi mwaka huu wa 2015.
Bw. Shija aliongeza kuwa katika Tamasha la mwaka huu ambalo ni la mwisho katika historia ya mfululizo wa matamasha ya Grown and Sexy waliona ni vema kumleta msanii maarufu toka Nigeria “Tekno Miles” ambaye aliwasili jana usiku mida ya saa nane akitokea Nigeria tayari kwa kulipamba Tamasha hilo. Msanii huyo ambaye anatamba na vibao mbalimbali kwenye anga ya muziki hivi sasa kama Shoki, Duro na Wash atatumbuiza laivu kwenye Tamasha hilo ambalo litafanyika siku ya mkesha wa mwaka mpya katika ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga, Msasani karibu na Best Bite.
Sambamba na uwepo wa msanii huyo wengine wataopamba Tamasha hilo ni Dj Maarufu “Young Guru” ambaye ni Dj rasmi wa msanii Jay Z toka Marekani ambaye ataisimamia shoo hiyo vilivyo pamoja na malkia wa uswazi mwanadada “Shaa” kisura wa Tamasha hilo ambaye atasherehesha shughuli nzima katika usiku wa tukio.
Kwa upande wake Msanii Tekno alisema anafurahia kusherekea mkesha wa mwaka mpya akiwa Tanzania na kuahidi kuporomosha burudani ya nguvu kwa mashabiki wake watakaojitokeza kushuhudia Tamasha hilo la kufunga mwaka.



Naye Mwakilishi wa Capital events waandaaji wa Tamasha hilo Bw. Justin Massawe alisema “Tunawakaribisha wapenzi wote wa burudani na chapa ya Johnnie Walker kujitokeza kwa wingi kushuhudia Tamasha letu la mwisho la Grown & Sexy na kuahidi kuwa litakuwa la kufana zaidi kwani wamejipanga kutoa burudani ya nguvu na kuwafurahisha mashabiki mbalimbali.

“Ningependa kuwashukuru wadhamini wetu mbalimbali katika kipindi chote cha mfululizo wa matamasha haya tokea yalipoanzishwa rasmi kwa ushirikiano mzuri ambao wametupatia hadi hii leo tunapofunga rasmi tamasha hili la mwisho la Grown and Sexy the Gold finale.”
Bw. Justin hakusita pia kuwashukuru Johnnie Walker kwa kuhakikisha wanakamilisha mikataba yote ya kumleta msanii Tekno Miles pamoja na Dj Young Guru hapa nchini na kwa kuhakikisha kwamba tamasha la mwisho linakamilika kwa mafanikio” makubwa zaidi.
JANA Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp ilibidi atulizwe munkari na Polisi ya kumpandishia Meneja mwenzake wa Sunderland Sam Allardyce wakati wa Mechi ya Ligi Kuu England Uwanjani Stadium of Light.
Klopp alipandwa na jazba wakati Jeremiah Lens wa Sunderland alipomchezea rafu mbaya Beki wa Liverpool Mamadou Sakho.
Wakati huo Liverpool walikuwa tayari washafunga Bao lao pekee na la ushindi kupitia Christian Benteke aliefunga Dakika ya 53.
Klopp aliamini Sakho ameumia vibaya na Lens alipaswa kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu lakini Refa alimpa Kadi ya Njano.
Hapo ndipo Klopp alipoanza kumbatukia Sam Allardyce, maarufu kama Big Sam, na munkari ulipopanda Polisi waliingia kati kumtuliza Klopp.
Baadae, Allardyce alisema Klopp alitumia maneno mabovu na ya matusi na kumweleza Meneja huyo wa Liverpool kama 'Mjerumani laini'.
Hata hivyo, bifu halikuendelea kwani mwishoni Mameneja hao walipeana mikono kama ilivyo desturi Mechi ikimalizika.

Wednesday, December 30, 2015

LA LIGA: ..FC BARCELONA 4 v 0 REAL BETIS

Barcelona wamerejea tena kileleni mwa La Liga baada ya Timu za Jiji la Madrid, Real Madrid na Atletico Madrid, mapema kupokezana kukaa juu,
Barcelona, wakicheza kwao Nou Camp, waliitwanga Real Bertis 4-0 na kuongoza La Liga wakiwa na Pointi 38 kwa Mechi 16 wakifuata Atletico wenye Pointi 38 kwa Mechi 17 na Real wakiwa wa 3 na Pointi zao 36 kwa Mechi 17.
Bao za Barca zilifungwa na Westerman, aliejifunga mwenyewe katika Dakika ya 29, Lionel Messi, dakika ya 33 na Luis Suarez, Dakika za 46 na 83.
Mapema Leo, Real Madrid iliichapa Real Sociedad 3-1 na kutwaa uongozi.

Nao Atletico Madrid walibanwa na Rayo Vallecano hadi mwishoni ambapo Bao za Angel Correa, Dakika ya 88 na Antoine Griezmann, Dakika ya 90, ziliwapa ushindi wa 2-0.



ENGLAND imeanika Listi ya Wagombea wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka kwa Nchi yao ambapo pia ipo Tuzo kwa Chipukizi Vijana wa chini wa Miaka 21, U-21.
Kepteni wa England, Wayne Rooney, ambae alishinda Tuzo hiyo Mwaka Jana, ni miongoni mwa Wachezaji Watano wanaogombea.
Rooney Mwaka huu aliiongoza England kufuzu kuingia Fainali za Mataifa ya Ulaya, EURO 2016, ambazo zitachezwa huko France Mwezi Juni huku akihakikisha England inashinda Mechi zao zote 10 za Kundi lao.

Pia, Mwaka huu, Rooney aliivunja Rekodi ya Sir Bobby Charlton ya Ufungaji Bora katika Historia ya England kwa kufunga Bao 50 Rekodi ambayo iliwekwa na Charlton Mwaka 1968 alipofunga Bao lake la 49. 

Wagombea Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka:

Joe Hart (Manchester City)
Gary Cahill (Chelsea)
Raheem Sterling (Manchester City)
Wayne Rooney (Manchester United)
Harry Kane (Tottenham Hotspur)

Kwa Vijana wa U-21, Straika wa Man United, Jesse Lingard, yumo kwenye Listi ya Wagombea Watano na huenda akashinda baada ya kung’’aa alipoichezea England U-21 Mwezi Juni Mwaka huu huko Czech Republic kwenye Fainali za Ulaya za U-21.

Wagombea Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka kwa U-21:

Jack Butland (Stoke City)
Carl Jenkinson (West Ham United)
James Ward-Prowse (Southampton)
Jesse Lingard (Manchester United)
Nathan Redmond (Norwich City)

Kura kwa Wagombea hawa zitapigwa Mtandaoni na Masapota wa England na upigaji utafungwa Jumapili Januari 3.


Ronaldo akishangilia moja ya  bao lakeLeo La Liga imerejea tena na ndani ya Santiago Bernabeu, Mchezaji Bora Duniani Cristiano Ronaldo aliiongoza Real Madrid kuichapa Real Sociedad Bao 3-1 na kuongoza Ligi hii ya Spain pengine kwa muda tu hadi baadae Usiku huu.
Ronaldo alikosa kuipa Real Bao wakati walipopewa Penati na yeye kuipaisha juu lakini Dakika ya 42 wakapata Penati nyingine na yeye kupiga tena na kufunga.
Hadi Mapumziko, Real 1 Sociedad 0.
Dakika 4 tu baada ya Kipindi cha Pili kuanza Real Sociedad wakasawazisha kwa Bao la Armindo Bruma lakini Ronaldo akaipa Real Bao la Pili alipounganisha Kona ya Marcelo.

Bao la 3 kwa Real lilifungwa na Lucas Vazquez, alieingizwa Kipindi cha Pili kumbadili Karim Benzema, na hilo kuwa Bao lake la kwanza kabisa kwa Real.

waliotembelea blog